Je uchawi una harufu? Unanuka au unanukia?

Je uchawi una harufu? Unanuka au unanukia?

.
 

Attachments

  • a9c2a2621ad52d802e29d228ea1399e5.jpg
    a9c2a2621ad52d802e29d228ea1399e5.jpg
    112.7 KB · Views: 52
Uchawi uliumbwa pamoja na dunia lakini kwenye ulimwengu wa roho.. Na ni sehemu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu mwenyewe
Uchawi ama wachawi upo wa kila aina kutoka kwa binadamu mpaka wanyama... Kutoka milimani mapangoni misituni angani ardhini mpaka majini
 
Uchawi upo na unafanya kazi na hata katika misahafu inakiri hilo.. Dhana ya kurogwa ni dhana kengeufu iliyokosa uhalisia kwa sehemu kubwa..
Wengi wa wanaoitwa waganga wa kienyeji ni matapeli na wafanya mazingaombwe wanaoganga njaa kiujanjaujanja
Uchawi halisi na waganga wa kweli ni vitu vinavyopotea kwa kasi ya ajabu duniani
 
Wajuzi wa mambo wanasema kwa lugha ya kigeni "There is a parallel universe." Sina hahakika na tafsiri inakuaje ila kwa maana fupi hatupo peke yetu viumbe wenye nyama kwenye hii dunia.
 
Naona kuna shida JF.... Ukireply... Reply haiji na quote
 
Maranyingi huwa ni nyoka hasa wa kijani
 
Nawezaje kumtambuwa mganga wa kweli na mganga matapeLi? Pia naomba kama unawez kunielekeza mahali ambapo naweza kupata kinga, mtu asiweze kudhuru biashara yangu kwanjia za kishirikina
 
Giza haliwezi kutoweshwa kwa kinvuli, ushirikina ni giza unachotakiwa kuwa nacho ni tochi yaani Yesu amulike kwenye biashara yako, familia yako, n.k! Utaliwa mpaka siku huruma ya Mungu ikufikie, na huruma ndizo hizi nikupazo leo mwamini Yesu vitu kama hivyo havitufikirishi usipoamini leo utaamini tu kwani kuokoka ni lazima. Ahsante!
 
Naweka mjadala huu kwa niaba ya mdau wangu aliyeniomba ufafanuzi juu ya hili na akapenda niwashirikishe nanyi...

Je uchawi una harufu gani?
Unanuka?
Unanukia?
Kama unanuka ni harufu ya nini?
Kama unanukia....! Unanukiaje?

Uchawi kwa maana nzima ya dhana ya ulozi ushirikina na shirki... Haunuki, haunukii wala hauna harufu yoyote.. Uchawi ni nguvu roho.. Huwezi kuuona, kuushika, kuusikia wala kuunusa.... Sanasana unaweza kuhisi nguvu yake hasa pale unapofikia mahali ambako pametekwa na hiyo nguvu... Utahisi hali tofauti, mapigo ya moyo kuongezeka, nywele kusimama na mwili kusisimka! Hakuna harufu.....

Kinachonuka ama kunukia ninini sasa?
Kinachonuka ama kunukia ni vitendea kazi!
Kama ni vitu vinavyotokana na binadamu mfano nywele kucha nguo ngozi mate au haja kubwa na ndogo!

Kinachonuka ama kunukia ni mitishamba, mapembe makombe na zanakazi nyingine za kishirikina....

Uchawi kama uchawi hauna harufu kabisa... Ni jambo la kiroho ambayo matokeo yake ndio ithibati pekee tena kwa wale waamini tuu...

Ukiona mtu ananukia sana hizi ni ishu za majini... A ukipita sehemu ukakuta pana harufu nzuri sana... Fahamu kwamba hilo eneo majini wapi tena wale wapendanao harufu nzuri hasa udi na uturi wa harufu kali na mavumba ya kuvukiza...

Ukikutana na ushirikina huku ananukia sana basi huyo ni mojawapo wa wale wajanja wajanja wanaojaribu kufanya kolabo isiyomatch ya vitu viwili tofauti....
Asante sana kwa shule brother...
Ila topic zako huwa natamani sana ziwe ndefu kama kitabu ili nipate vitu vingi vya elimu ya ulimwengu wa roho side B. Nina swali dogo kwako brother Mshana Jr. Una chapisho lolote la kitabu au magazine ya hizi mambo?
 
Back
Top Bottom