Je, Tundu Lissu amekumbwa na jinamizi gani mpaka amegeuka kuwa adui wa Rasilimali za nchi hii?

Wadau, kuthibitisha kuwa mkono mtupu haulambwi? Au anaogopa kumuunga mkono Rais Magufuli ili asimpe point?

Mwenye jibu mujarab aje fasta hapa atujuze
Adui mkubwa wq rasimali za taifa hili ni CCM sio Tundu lissu,,,,Tanzania chini ya CCM imesainiwa mikataba mibovu na kama Lowassa n8 fisadi mnasubiri nini kumshitaki??
 
Hata rais anachukua sheria pia katika hili usifikiri atakurupuka,kwani mpka sasa alichokurupuka ni kutoa ripoti?,bado kamati nyingine ya uchumi na sheria haijatoa mapendekezo,tuliza mpira kijana
Hata kilichoandikwa na ulichojibu hujui
 
Tundu Lissu ni level nyingine.

Lissu ni Rasilimali watu inayopotea nchi hii kama ambavyo rasilimali madini inavyopotea katika hii nchi kisa si tu si mwana-CCM hivyo hata mawazo yake mnayapuuza!
kuwatoa wahalifu waliyokwisha kuhukumiwa jela eti fomu ya mashtaka kukosewa kujazwa ndio level. kuropoka ovyo na kutukana mpaka bungeni ndio level. huyu mtu ana matatizo ya akili very complicated/sophisticated. anahitaji msaada.
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Kwa maelezo yake, Tundu Lissu amejipambanua kuwa amepigania rasilimali za nchi hii tangu mwaka 1999. Kwa kipindi chote, ilikuwa ni rahisi kupima uzalendo wa Tundu Lissu hasa dhidi ya wahujumu uchumi wa nchi hii.

Hata hivyo, tangu mwaka 2015 baada ya CHADEMA kumchukia Edward Lowasa licha ya kashfa lukuki za ufisadi dhidi yake, Tundu Lissu kwa sasa amegeuka kuwa mwanasheria wa ajabu kuweza kutokea katika tasnia hiyo hapa nchini. Yeye sasa ni mtetezi wa kila maovu katika nchi hii.

Nilitaraji kuwa katika hili la kuibiwa kwa madini yetu atamuunga mkono Rais Magufuli na kila mwenye nia njema kwa nchi hii.

Najiuliza, ni jinamizi gani limemkumba Tundu Lissu? Ama lile lililotumika kumsafisha Edward Lowasa baada ya kumchafua kwa miaka kadhaa sasa limewaingilia kinyume na matakwa yao? Au ni kuthibitisha kuwa mkono mtupu haulambwi? Au anaogopa kumuunga mkono Rais Magufuli ili asimpe point?

Mwenye jibu mujarab aje fasta hapa atujuze

Umekosa busara sana. Hutaki kutendea haki akili ulizopewa na Mungu
 
Mwanasiasa siku zote anatafuta mianya kwenye kila tukio ili ajijenge.
1999 ulikuwa unagombania mambo ya madini. Hizo siku nyingine ulikuwa wapi hadi uanze upya baada ya mkuu wa nchi kuonyesha nia hii.
mkuu tena umebadilisha avatar picha ya faure rais wa ushelisheli
 
Kwa mawazo yako ni sahihi. Lakini kwa watu wanaoelewa sidhani kama upo sahihi. Mtu mwenye akili huonekana linapotokea tatizo. Approach ya mtu mwenye akili kwenye tatizo fulani ni tofauti kabisa.

Kwanza hapayuki na wala hapigi kelele kama anavyofanya Lissu. Alipayuka hivyo hivyo wakati anamchafua Lowassa, lakini sasa kampokea na ndo mtetezi wake.

Sasa kwa hili la madini, nilitarajia Lissu aonyeshe njia na si kupayuka na kupiga kelele. JPM hatafuti sifa kama Lissu anavyodai.

Kuwa rais wa nchi tu ni sifa na umaarufu wa kutosha. Anayetafuta sifa tena kwa nguvu ni Lissu. Itoshe tu kusema Lissu ni mpiga kelele na ndo hulka yake. Kwa wasiojua watamshabikia tu
Anapayuka mkweo
 
tangia amtukane baba wa taifa kipindi cha katiba mpya, amebaki kuropoka tu. laana hiyo.

Hata ndani ya nafsi yako unafahamu kuwa TL ni level nyingine. Kinachonisikitisha ni vile tu huna jambo lolote la busara linaloweza kuigwa na jamii
 
Hoja za kisheria ni za upande mmoja tu??, Haiwezakani!,
Lissu kwa sasa anaongozwa na chuki, wivu na hasira za kijinga. Tume zimeundwa mbili kwa nini asipeleke maoni yake kwenye tume ya pili??
Umevurugwa wewe siyo bure
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Kwa maelezo yake, Tundu Lissu amejipambanua kuwa amepigania rasilimali za nchi hii tangu mwaka 1999. Kwa kipindi chote, ilikuwa ni rahisi kupima uzalendo wa Tundu Lissu hasa dhidi ya wahujumu uchumi wa nchi hii.

Hata hivyo, tangu mwaka 2015 baada ya CHADEMA kumchukia Edward Lowasa licha ya kashfa lukuki za ufisadi dhidi yake, Tundu Lissu kwa sasa amegeuka kuwa mwanasheria wa ajabu kuweza kutokea katika tasnia hiyo hapa nchini. Yeye sasa ni mtetezi wa kila maovu katika nchi hii.

Nilitaraji kuwa katika hili la kuibiwa kwa madini yetu atamuunga mkono Rais Magufuli na kila mwenye nia njema kwa nchi hii.

Najiuliza, ni jinamizi gani limemkumba Tundu Lissu? Ama lile lililotumika kumsafisha Edward Lowasa baada ya kumchafua kwa miaka kadhaa sasa limewaingilia kinyume na matakwa yao? Au ni kuthibitisha kuwa mkono mtupu haulambwi? Au anaogopa kumuunga mkono Rais Magufuli ili asimpe point?

Mwenye jibu mujarab aje fasta hapa atujuze
yaani wee jaamaa bila kumtaja lowasa hujisikii. Sijui ukiwa unaposti mzee Ngoyai huwa anakupakata
 
Hata Bashite alipoanza Maigizo yake ya kupambana na "unga" wenye busara wachache walipotahadharisha wakabezwa, wakatukanwa na kuitwa sio wazalendo na watetezi wa wauza unga. Mwisho wa lile igizo tukajua nani mzalendo na nani sio mzalendo. Definition ya neno "mzalendo" au "uzalendo" ni kuitikia "ameeeen" kwa kila uamuzi/kauli/tendo linalofanywa na JPM au Bashite. Ni mbaya sana kukaimisha uwezo wako wa kufikiria (reasoning) kwa mtu mwingine yaani mtu mwingine awaze kwa niaba yako. Katika hili la madini, waliotoa angalizo na ushauri wa njia gani tuchukue ili tusipate madhara ni wengi lakini wewe umemuona Lissu tu. Chenge, Masaju, Warioba nk nk nk
 
Back
Top Bottom