Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,375
Wadau, amani iwe kwenu.
Kwa maelezo yake, Tundu Lissu amejipambanua kuwa amepigania rasilimali za nchi hii tangu mwaka 1999. Kwa kipindi chote, ilikuwa ni rahisi kupima uzalendo wa Tundu Lissu hasa dhidi ya wahujumu uchumi wa nchi hii.
Hata hivyo, tangu mwaka 2015 baada ya CHADEMA kumchukia Edward Lowasa licha ya kashfa lukuki za ufisadi dhidi yake, Tundu Lissu kwa sasa amegeuka kuwa mwanasheria wa ajabu kuweza kutokea katika tasnia hiyo hapa nchini. Yeye sasa ni mtetezi wa kila maovu katika nchi hii.
Nilitaraji kuwa katika hili la kuibiwa kwa madini yetu atamuunga mkono Rais Magufuli na kila mwenye nia njema kwa nchi hii.
Najiuliza, ni jinamizi gani limemkumba Tundu Lissu? Ama lile lililotumika kumsafisha Edward Lowasa baada ya kumchafua kwa miaka kadhaa sasa limewaingilia kinyume na matakwa yao? Au ni kuthibitisha kuwa mkono mtupu haulambwi? Au anaogopa kumuunga mkono Rais Magufuli ili asimpe point?
Mwenye jibu mujarab aje fasta hapa atujuze