Je, Tanga imeondelewa hadhi ya jiji?

Je, Tanga imeondelewa hadhi ya jiji?

Tanga sio jiji , bajeti ya mwaka 2025/2026 katika miundombinu ya majiji haikuhusishwa hasa barabara kubwa ,na bajeti ya juzi ya mwaka 2026/2027 napo pia haipo kwenye list yaani mpaka Njombe ndani ikiungajishwa na Mbeya ila Tanga hola.

Kwenye bajeti za flyover waziri wa ulega alitaja watajenga flyover kwenye majiji ma 4 Tanga haikutajwa, pia nakumbuka alitaja mradi wa mwendo kasi katika majiji alitaka yote ila Tanga kaiacha, na kwenye mambo mengi tu,

Je, Tanga imeondolewa kwenye orodha ya majiji ila serikali haitaki kusema?
Tatizo ni kutokuwepo akina January, yule dada aliyekuwa waziri wa afya, mtasubiri mpaka wapatikane watu kama hao. Ndivyo nchii hii na CCM walivyo.
 
Kwa definition za Jiji Tanga ni proper jiji kushinda majiji mengi Nchi hii. Unless hujui jiji ni nini.
Sio kweli.Jiji gani ina hotel moja tu ya hadhi(Tanga beach)?.Ikifika saa mbili usiku huduma kibao hupati , washafunga.Tanga na Mbeya hamna majiji hapo.
 
Sio kweli.Jiji gani ina hotel moja tu ya hadhi(Tanga beach)?.Ikifika saa mbili usiku huduma kibao hupati , washafunga.Tanga na Mbeya hamna majiji hapo.
Tanga beach Yenyewe Hotel ya juzi Tu hapa, ukiona MTU anasema Tanga Beach ndio hotel kubwa Tanga ujue hana analojua.

1. Hotel kubwa Kabisa Tanga na kongwe miaka nenda miaka rudi ni Mkonge Hotel sio Tanga beach, ina vyumba na service za kisasa kabisa.

2. Ukitoa Mkonge kuna Hotel Nyingi mno, Mwambani Beach Villa, Villa Matalai, Peponi etc. long story Short Ukanda wote wa Pwani kuanzia Tanga Hadi pangani Una Hotel Nyingi mno kuna Access Hadi za surfing, kwa Tanzania bara hakuna kama Tanga kwenye hizo issue, japo Nchi kama Nchi haitangazi huo utalii, wazungu wengi wanapenda so wanakuja kwa wingi mno na kuna uwekezaji mkubwa wa Hotel hio pwani nzima.

3. Unaweza ukataja hizo Huduma saa 2 usiku hupati na kwengine unapata?
 
Back
Top Bottom