Je, TANESCO wanaruhusu kugawana umeme kwa nyumba za taasisi?

Tilalilala

Member
Nov 30, 2014
78
66
Naomba kuuliza swali mimi nakaa kwenye nyumba ya taasisi ila nyumba yangu ina umeme ya jirani yangu ipo kama mita 70 hivi haina umeme ila nataka kutoa waya kutoka kwenye extension yangu mpka kwake ili aweze kutumia kwa matumiz madgo madgo kama kuchaj simu n.k

JE, HII INARUHUSIWA MAANA NI NYUMBA YA SERIKALI NA MITA INASOMA JINA LA TAASISI?
 
Naomba kuuliza swali mimi nakaa kwenye nyumba ya taasisi ila nyumba yangu ina umeme ya jirani yangu ipo kama mita 70 hivi haina umeme ila nataka kutoa waya kutoka kwenye extension yangu mpka kwake ili aweze kutumia kwa matumiz madgo madgo kama kuchaj simu n.k JE HII INARUHUSIWA MAANA NI NYUMBA YA SERIKALI NA MITA INASOMA JINA LA TAASISI?
Kama mita namba na namba za nyumba si tofauti? Hairuhusiwi.
 
Acha perecheche

Unaishi nyumba ya serikali bure halafu unakuwa kilomolomo?

Ngoja wake wakutoe kwenye nyumba hiyo🙏🏌️
 
Adhabu yake endapo utabainika ni faini ya million 5 au jera miaka 3 au vyote kwa pamoja
 
Umeme uliopita kwenye mita Yako...una haki ya kutumia utakavyo. Hata kumpa jirani. Ila umeme ambao haujapita kwenye mita huo ni haramu kama madawa ya kulevya.
 
Vile Tanesco wanausoma huu uzi

images - 2023-10-13T081703.230.jpeg
 
Umeme uliopita kwenye mita Yako...una haki ya kutumia utakavyo. Hata kumpa jirani. Ila umeme ambao haujapita kwenye mita huo ni haramu kama madawa ya kulevya.
Acha kumdanganya hilo ni kosa kubwa sana, kinacho ruhusiwa ni kama nyumba zipo kwenye kiwanja kimoja, tu, na iwe na matumizi madogo ya umeme, kwani kama ni nyumba yenye matumizi makubwa, inaweza leta tatizo kutokana na ukubwa wa waya unaoleta umeme tika kwenye nguzo kuleta kwenye mita kuzidiwa. Yaani ikibainika umempa jirani yako umeme, adhabu yake ya kwanza ni kuondoa mita hiyo kwako.
 
Acha uoga mpe mwenzako umeme ila asiwe mropokaji atulize mshono watu wanaiba mabilioni ya hela kila siku kwenye ripoti wanatajwa lakini hawafanywi chochote ww unaogopa nn
 
Back
Top Bottom