Je sio ushamba na ulimbukeni kuona aibu kuongea Lugha ya kabila lako eti kisa uko mjini?

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Kuna makabila ambayo hata wawe wapi wao kunena kwa lugha sio shida.
Mfano;Wajaluo,Wasukuma na Wamasai tena hawa ndio wanaona raha.

Binafsi huwa namkubali sana mtu ambaye anaongea Lugha ya asili hata akiwa kariakoo,Vyuoni,Kwenye ndege, kwenye bus au popote mjini bila wasiwasi.

Kabila hizi ni zetu jamani, Mungu ameipendelea Tanzania kuwa na makabila lukuki.
Kwa mtazamo wangi ni ulimbukeni na ushamba kuogopa kuongea lugha yako ya asili ili uonekane wa mjini.

Tukumbuke jadi zetu jamani, huo ndio uafrika maana nimegundua kiswahili fasaha na kiingeleza bado ni shida kwa wengi.

8878f831614aaa4ee6d61daede08f05d.png
 
kweli mkuu,wengi wanadhani ni ushamba kuzi'expose kabila zao...kikubwa tu isiwe kwa namna ya ubaguzi na uchochezi,otherwise makabila yetu yana sound vizuri sana mtu akiwa anaongea na unamuelewa,mfano langu ni HEHE,i love to hear it all the time
 
Kuna raha yake, mambo ya ukabila na kubaguana kwa misingi ya ukabila ni ushaba na kutokuwa na elimu ya kutosha.
Tufurahie hizi lugha aisee, ndio maana ya nchi kuwa huru,kuna raha zake....
ndio maana ukiingia uganda kampala pale ni lugha gongana kwa kwenda mbele jiji zima.. kiingeleza, kishwahili,Lugha ya kienyeji ya Kiganda ndio kama asilimia 80.
 
kwa bahati mbaya wengine hatujui kikwetu na tulipo hakuna pa kujifunzia je tufanyaje mkuu ila tunapenda sana kuongea kikwetu kama wasandawe hawaoni aibu.nawapenda kwa hilo
 
Si ukaongeleee kijijini kwenu... Mnatupigia mikelele hapa.. Kwani Nyerere hakuwa na akili kufanya kiswahili lugha ya taifa... Acheni uboya.. Tena hasa mimi ndo spend mijitu iongee kiluga mbele yang..mnaleta ukabila hapa
 
Ni ujinga tu; Mimi ukinisemesha kiluga mbele za watu huwa sijibu, ....ni kutaka kuonyesha tunajuana saaaaana! Kilugha kinafaida gani kwenye mchanganyiko Wa watu? Ongeeni kijijini kwenu .....huku mjini kiluga ni UMBEA TU WA KUTETANA.....
 
Si ukaongeleee kijijini kwenu... Mnatupigia mikelele hapa.. Kwani Nyerere hakuwa na akili kufanya kiswahili lugha ya taifa... Acheni uboya.. Tena hasa mimi ndo spend mijitu iongee kiluga mbele yang..mnaleta ukabila hapa
au nawewe hujui kikwenu mkuu au unaogopa kujulikana wewe ni kabila fulani?
 
Back
Top Bottom