Wanaume Wa Kisukuma na Ulimbukeni Wa Mapenzi Ya Wanawake Wengi. Kumbe Mume/Mke Mmoja Inawezekana!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325
WanaMMU,

Hili ni bandiko la kuhamasisha utulivu ndani ya ndoa kwa baadhi ya makabila, ambayo wanaume wao kuchepuka, ndoa za mitala na kuwa na wanawake wengi wanaona sifa bila kujua kuwa sio tuu wanawasononesha wake zao na wengine hadi kuwadhalilisha kwa kuwa na msusuru wa wanawake na watoto wa nje, bali pia kunahatarisha usalama wa familia enzi hizi za ukimwi.

Declaration of interest

Mimi ni Msukuma japo sio kutoka a typical Sukuma traditional ya chapa ng'ombe, but from a mixed familiy ya Baba Msukuma, (Rip Mzee Mayalla), na mama kutoka moja ya makabila yenye wanawake weupe ambao ndio ugonjwa na udhaifu mkubwa wa wanaume wa Kisukuma, nimezaliwa mjini, nimekulia mjini, nimesomea mjini, ninaishi mjini, hivyo mimi ni Msukuma wa mjini, ila pamoja na yote haya, genes za ushamba na ulimbukeni wa Kisukuma, nimejikuta ninazo!.

Traditional Sukuma Man ni Poligamist By Nature, Hatosheki na Mke Mmoja!.
Kwa nini Wanaume wa Kisukuma hupenda kuwa na wanawake wengi?, sababu halisi ni wale Wasukuma wa asili, ,chapa ng'ombe walikuwa very energetic with very high sex drive kutokana na kula natural foods za wakati huo, hivyo mke anayeolewa na Msukuma wa type hii, ni mke ndie anayemuomba mumewe amtafutie wenzake wakusaidiana naye maana jamaa walikuwa ni wale wa 24/7, 7 days a week, 30 days a month (isipokuwa zile siku), na 365 days a year, mtu peke yako ungeweza?. Tena kama mwanamume atachelewa kuleta wanawake wa kumsaidia, then ni mke mwenyewe anatafuta msaidizi na kumleta, ili amsaidie. Hizo ni enzi za zamani, Wasukuma wa siku hizi hawa wa chips kuku, hawana tena nguvu zile wala uwezo ule, hivyo hii tabia ya Wasukuma wa sasa kupenda wanawake wengi ni kujiendekeza tuu, na kupenda weupe ni kasumba tuu!.Wanawake ni wanawake tuu, na wote wako sawa kabisa, rangi has nothing to do with performance, tena hawajui kuwa light skinned, wear and tear ni kubwa zaidi, na endurance ya mechi ndefu hawahimili sana kama dark skinned!.

Wasukuma wa Sasa kupenda Wanawake Wengi na Kupenda Weupe ni kasumba tuu na Ulimbukeni!.
Wanaume wa Kisukuma wana hulka ya kutawaliwa na mfumo dume, wanaume hujiona wao ndio kila kila, wanapenda kuwa na wanawake wengi kwa masifa tuu!. Kwa mtu aliyeolewa na mwanaume wa Kisukuma, kwa mume wa Kisukuma kutoka nje ya ndoa ni kawaida sana katika makuzi yetu kwa baba zangu wadogo, taarifa za kutapakaa wanawake, nyumba ndogo na watoto wa nje kuletwa ndani ni kawaida sana, hivyo kwa mwanamume wa Kisukuma, kwake kupenda wengi ni halali, na kutoka nje ya ndoa hata kuzaa nje ya ndoa sio issue kuubwa kivile, tatizo kubwa la wanaume wa Kisukuma ni ulimbukeni wa mapenzi ambao ni udhaifu wa ajabu wa kupenda ch.ni, hivyo kutongoza kila mwanamke mweupe atakayepita mbele ya macho yake bila kujali umri au status kama ameolewa au la, Msukuma atatongoza tuu!. Hii ni tabia mbaya kwa wanaume wa Kisukuma na lazima tabia hii ikemewe ili kuwapunguzia mateso wanawake wa makabila mengine walioolewa na wanaume wa Kisukuma. Kwa wanawake wa Kisukuma, tabia hii ya wanaume wa Kisukuma kuwa na wanawake kibao na watoto wa nje kibao, sio tatizo kwao kwa sababu wao wamezoea, ndio asili yao. Japo Wasukuma ni watongozaji sana, ila wakikataliwa, hawamaind, hivyo sio ma minder!.

Nilipotangaza Kuoa, Mama Akanisihi Nisiwe na Tabia Mbaya za Kisukuma!.
Kiukweli wanawake wa Kitanzania ni wavumilivu sana, na hata ikitokea baba ana tabia za ajabu, mama hawezi kusema. Kama nilivyoeleza tabia za wababa wa Kisukuma kuleta ndani watoto wa nje, lakini kwetu kwa vile mama sio Msukuma, baba hakuleta watoto wa nje, ila alipofariki, kwenye msiba, ndipo nikatambua Msukuma ni Msukuma tuu, kwenye msiba kuliibuka watoto, and no way out, huwezi kuikataa damu yenu, hivyo mpaka leo kujikuta unalazimika kusaidia baadhi ya ndugu zako ambao hukutambua uwepo wao kabla hadi mhusika alipotangulia mbele ya haki. Tabia hii sio tuu inawatesa wamama, bali inabebesha mzigo wa ziada kulea too extended family. Hivyo nilipotangaza kuoa, mama alinihusia katika ndoa yangu, nijitahidi sana, nisiwe na tabia mbaya za wanaume wa Kisukuma, na mimi nikaahidi, sio tuu sitathubutu kuzaa mtoto nje ya ndoa, niliahidi kuwa sitatoka nje ya ndoa maisha yangu yote!.

Kumbe mambo mengine jamani sio makosa yetu ni asili yetu!, genes za Kisukuma ziko ndani yetu, na sex drive zetu ni kubwa!. Kilichotokea kwenye ndoa yangu saa hizi its a history ila by now nina watoto 8, na ni wamama 3 wamesaidiana!. Its not me, its the Sukuma nature, na ikitokea idadi kuongezeka, natoa taarifa na kuleta kutambulisha sio kusubiri surprises za sherehe ya tatu!.

A Good Example of Typical Tradinal Sukuma Familiy ya Mke Mmoja, Mume Mmoja!.
Ili kuwasaidia wanaume wa Kisukuma kuacha tabia zao mbaya za penda penda na zaa zaa, naomba niwape simulizi za hii modal Sukuma family ya mume mmoja, mke mmoja na mtoto mmoja, ambayo ni typical kwa familia za kizungu tuu, but not za Kiafrika and to be specific not za Kisukuma, kufuatia wanaume wengi wa Kisukuma kuwa na ulimbukeni sana wa mapenzi ya wanawake wengi, wao wanaona ni sifa lakini kiukweli ni ulimbukeni tuu wa mapenzi, na ushamba wa kupenda wanawake weupe, kwa sababu kumbe kuna Wasukuma wa kisasa ana mke mmoja na mume mmoja na kujaaliwa mtoto mmoja, na imewezekana!.

Familia za Kisukuma za Mke Moja, Mume Mmoja Zinahesabika Lakini Zipo!.
Kuna familia fulani ya Kisukuma imenigusa sana jinsi ilivyo na upendo wa kweli kwa kuwa na mume mmoja, mke mmoja, na imebahatika kupata mtoto wao mmoja tuu wa pekee, na imebarikiwa sana!.

Kwa kawaida wanaume wa Kisukuma wengi ni malimbukeni wa mapenzi, japo ndilo kabila ambalo wanaume wake wanaongoza kwa kupenda sana, pia wana honga sana tatizo ni ushamba, ulimbukeni na masifa ya kuwa na wanawake wengi sambamba na kupenda kuzaa watoto wengi. (mimi binafsi nina watoto 8, wamama watatu wamesaidiana).

Kiukweli wanaume wa Kisukuma ni washamba wa mapenzi ila pia bado wametawaliwa na mfumo dume ambao baba ndio kila kitu.

Inapotokea Msukuma ameoa halafu familia hiyo kuchelewa kupata mtoto, matatizo yote ya kutopata mtoto na kunyoosheana vidole, huelekezwa kwa mwanamke tuu, kwa sababu katakana na ushamba wa Kisukuma, wanaume wote hujiona ni dume la mbegu, hivyo matatizo yoyote ya uzazi na kotopata mtoto, huelekezwa kwa mwanamke tuu.

Na kunapotokea ndoa ikachelewa kujibu kwa muda mrefu, mwanamke hupata masimango na manyanyaso sana haswa kutoka kwa mawifi, mashemeji na wakwe wa kuumeni, ambapo humshinikiza mwanao aoea mke mwingine ili amzalie watoto!. Hivyo baba huhalalisha kuoa mke mwingine ili kutafuta mtoto .

Lakini kwa upande wa familia ya mfano ninayoizungumzia hapa, licha ya kuchelewa kupata mtoto kwa kipindi kirefu baba wa familia hiyo alikuwa na upendo wa ajabu, alishikilia msimamo kushikamana na mkewe bila kutafuta mwanamke mwingine bali wote wawili walijikabidhi kwa Mungu mpaka Mungu alipojibu maombi yao wakafanikiwa kupata mtoto mmoja wa pekee na baada ya kuzaliwa, walisema asante Mungu, na kukikabidhi kichanga hicho mikoni mwa Mungu kiwe mali yake!, na kweli ikaja kutokea, mtoto huyo amekuja kuwa na bahati ya ajabu, ambayo ni uthibitisho alizaliwa na kismati.

Kwa kawaida zingekuwa ni ndoa nyingine, wanandoa wanapokosa mtoto, sio tuu lawama zote huelekezwa kwa mwanamke, bali pia baba wa kwenye família kama hizo huwa anakuwa very bize hujitahidi sana kucheza vijimechi vingi vingi vya nje na ugenini ili kujaribu mashuti kama yanaweza kufunga goli, ukijikuta hujabahatisha hata kufunga bao la kuotea au la kusingiziwa, inakubidi wewe baba kuwa mdogo tuu na kujituliza kimya kwa kukabidhi tuu Mungu kusubiria muujiza!.

Huku katika kusubiri huko mama kamwe hawezi hata kuthubutu kumshauri baba nae akapime huenda tatizo ni kwa mwanaume, bali mama yeye kwa kutumia akili za kike za kuzaliwa, hutumia mbinu mbalimbali za medani, kujipima kama jee kweli tatizo ni yeye au yeye anaweza kuwa ni mzima, hivyo tatizo linaweza kuwa kwa baba? .

Ni katika kuhangaika huku mara ikatokea, Mungu akajibu maombi, mama akashika ujauzito hivyo kuleta furaha ya pekee kwenye familia za aina hiyo ambayo hatimaye ikafanikiwa kupata mtoto, unadhani kunaweza tena kuendelea kujiuliza kama kulikuwa na tatizo, au tatizo ni la nani?, maadam, mama kashika ujauzito, hiyo inabakia kuwa ni mibaraka ya Mungu.

Kiukweli kwa jinsi wanaume wa Kisukuma walivyo, jinsi wanapenda wanawake wengi, it's very unusual kutokea mwanaume wa Kisukuma aliyekosa mtoto kwa muda mrefu kumtegemea Mungu tuu na sio kujaribu mashuti ya pembeni, na hata baada ya kufanikiwa kumpata huyo mtoto mmoja wa ngama, baba huyo hakujaribu tena kutafuta mtoto mwingine kwa mwanamke mwingine yoyote, bali alitulia tuu na mkwewe kudhihirisha upendo wa dhati.

Hii ni modal family ya Kisukuma ambayo imeonyesha utofauti mkubwa na the normal traditional Sukuma ways kwa kuonyesha upendo wa hali ya juu na kumtegemea Mungu, inatupa uthibisho kuwa hata kwa Wasukuma wa kisasa, ndoa za mke mmoja zinawezekana, na wanaume wa Kisukuma bila kuwa na wanawake wengi inawezeka.

Swali, ni wanaume wangapi, wanaupendo mkubwa namna hii kwa wake zao, hata wakichelewa kupata watoto kwa miaka mingapi, watavumilia tuu, na kuwa very faithful for each other, bila kujaribu mashuti ya pembeni?.

Wanawake wangapi, wanaweza kuvumilia kuchelewa kupata watoto, huku wakinyooshewa vidole wao ndio chanzo cha tatizo, bila kuchukua initiatives za kujaribu pembeni kama wanashika au laa?!.
Hitimisho.
Wanaume wenzangu wa Kisukuma, tubadilike!, hii tabia ya kupenda wanawake wengi na kushobokea wanawake weupe hadi kutoka nje ya ndoa kwa ajili ya kufuata rangi tuu, tuiache!, sio tuu inawadhalilisha wake zetu, bali its a threath kwa usalama wa familia kwenye enzi hizi za ukimwi!.

Hongera sana kwa familia hii ya mfano na wito kwa Wasukuma wengine tuinge mfano wa familia hii, zile sifa za ulimbukeni wa mapenzi, na mapenzi ya masifa ya kuwa na wanawake wengi, zimepitwa na wakati, tubadilike!.
Paskali.
 
Mkuu hiyo research umeifanyia wapi,MBNA unatusingizia mchana kweupe!! Ni kweli tunapenda watoto wengi,lakin issue ya wake wengi,hapo mkuu unatuonea buree!!!

Au labda sijaelewa bandiko vizuri,ngoja niludie kusoma..
 
Unamuzungumzia PM Mbona wapo wengi sana wa hivyo mkuu, kuna wale wenye imani za dini wakristo , wale waliostarabika na kadhalika hivyo usichukulie wasukuma wote kuwa wanaoa wanawake wengi
 
Jambo unalosema kwa kiasi fulani ni la kweli ila kwa dunia ya sasa wamebadilika kama ilivyo kwa makabila mengine. Hizo tabia za kuonga,kupenda sana na kuzaa watoto wengi ni tabia au ufahali wa makabila mengi na jamii duniani hivyo basi sio jambo la kushangaa au kusikitika.
Ushamba, mfumo dume bado upo na utaendelea kuwepo sio tu kwa wasukuma bali kwa jamii mbalimbali hapa Tanzania na duniani simply because kila jamii ina mila na desturi za kuzitunza na kuzitii.
Leo unaeza ona na kuamini haki sawa ni jambo zuri lakini ukifanya utafiti kidogo unaeza gundua madhara makubwa na kujiuliza je ni sahihi au sawa kwa wanawake kufanya kila jambo mwanaume anafanya au haki sawa ni really a reality or just an illusion.
 
Nilikua nakuamini Sana! Sijui wasukuma wamekukosea nini? Ni wao tu wenye tabia hiyo? Ngoja nisome maranyingi labda kunakitu nnakipita!
 
Unamuzungumzia PM Mbona wapo wengi sana wa hivyo mkuu, kuna wale wenye imani za dini wakristo , wale waliostarabika na kadhalika hivyo usichukulie wasukuma wote kuwa wanaoa wanawake wengi

Mnasingizia Wasukuma uongo, Watu wa Mara ndo wenye kawaida ya kuwa na mke zaidi ya mmoja, hata kama ni Pastor(mchungaji - with lame excuse ya divorce) lazima wewe na mke zaidi ya mmoja!! I stand to be corrected.
 
Back
Top Bottom