Je, Simba SC inaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana?

Uchumi wa Mifugo

JF-Expert Member
May 20, 2021
345
575
Tangu jana mwekezaji wa Simba alipopost kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa amesikia kilio cha mashabiki wa Simba cha kutaka klabu yao iwe na uwanja wake wa kuchezea mechi za nyumbani na kuahidi kuchangia bilioni 2 kumeibuka mijadala kwenye redio na mitandao ya kijamii,kama ilivyo kawaida yetu Waafrika weusi wengine wanaunga mkono, wengine wanapinga, wengine wanaona haiwezekani na wengine wanadhihaki.

Wachambuzi wengi wa redio niliowasikiliza tangu jana na leo wanasema hakuna uwanja uliojengwa kwa fedha za harambee lakini viwanja vya CCM kama Kirumba, Majimaji, Sokoine, Ali Hassan Mwinyi na vinginevyo vilijengwa kwa wananchi kuchangishwa fedha, wafanyakazi walikatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao na wananchi wengine walichangia kwa njia nyingine. Majengo na ofisi za TANU na CCM wananchi walichangishwa, majengo ya makao makuu ya Simba na Yanga wanachama na wapenzi wa timu hizo walichangishana na kujenga majengo hayo.

Wachambuzi wetu wanadai Simba inatakiwa iende kwenye makampuni na kuingia ubia au kuuza jina la uwanja kama walivyofanya Arsenal kwa Emirates,hii njia inaweza ikawa ngumu kuliko kuchangishana, makampuni na mashirika mengi yamepitia kipindi kigumu cha mtikisiko wa uchumi uliosababishwa na Covid 19,pia kuna kampuni gani inayoweza kutoa bilioni 50,au 100 kwa ajili ya kujenga uwanja wa Simba, ligi kuu yenyewe kupata mdhamini wa bilioni 3 tu ni kazi kubwa,ukiona kampuni kama Vodacom inajitoa kudhamini ligi kuu ujue bado mpira wetu hauvutii wawekezaji...haulipi.

Pia uchumi wetu hausapoti uwekezaji wa aina hiyo,na ndiyo maana haya mambo ya makampuni kujenga viwanja unayaona Ulaya na Afrika Kusini tu,kwa sababu biashara zao ni kubwa na uchumi wao ni mkubwa.

Simba wanaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana ila wanatakiwa kujua kujenga uwanja si kazi ndogo,wanachotakiwa kufanya ni kujenga kwa awamu huku wakiendelea kuutumia,Simba haiwezi kushindwa kujenga uwanja wa nyasi bandia,wenye taa huku watazamaji wakiwa wamekaa kwenye majukwaa ambayo hayana viti kama wanavyofanya KirumbMa Majimaji, Sokoine,Samora na vingine.Kitu cha muhimu uwanja ujengwe kwa kuruhusu marekebisho, upanuzi nk.

Kitu kingine kwenye kuchangishana wanaweza kukusanya fedha kwa kuweka viwango na motisha fulani kwa wachangiaji mfano wanaweza kusema anayechangia kuanzia 100,000 anapewa cheti kama kumbukumbu na shukrani hii itasaidia watu wengi wapate morali ya kuchangia,pia majina yao yaandikwe na yawekwe nje ya uwanja.Wale wanaotoa kuanzia milioni 10 ,wanapewa viti maalum vya kukaa uwanjani yaani VVIP,nk.

Faida za kumiliki uwanja ni
kupata fedha zaidi,niliwahi kusikia wanalipia milioni 20 kwa kila wanavyocheza mechi uwanja wa Mkapa,wakiwa na uwanja wao hizi fedha hawatalipa.
Wataweza kupata fedha kwa kukodisha majukwaa na mageti kwa ajili ya matangazo,mfano geti A linaweza kukodishwa kwa kampuni X na kuitwa Gate X,badala ya geti A.Jukwaa kuu wanaweza kulikodisha kwa kampuni ya Dcom na wakaliita jukwaa la Dcom nk.

Kwahiyo Simba wanaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana na ninawatakia kila la heri,maneno ya wakosoaji yanatakiwa yawe mbolea ya kuanza kujenga uwanja.
 
WATANZANIA watakusaport sana kwa maneno......but ukija utekelezaji wa takukimbia

Anyway ....khanjibai hawezi kutumia fedha yake kujenga uwanja.....atafilisika
Kama muhindi anaweza kufikisika kwa kujenga uwanja basi jamaa Hana hela huyu, vipi kuhusu gharib aka GSM ye anaweza kujenga uwanja Mkuu?
 
Nimemsikia yule mbwiga Kitenge alivyokuwa anakoroma.Huyu mpuuzi kila linapokuja suala la Simba lazima aliponde tena kwa lugha ya dharau na kejeli nyingi. Kitenge anajifanya kujua kila kitu ilhali tunamjua ni mchicha mwiba.
FB_IMG_1629179437509.jpg

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Mtu anaposema haiwezekani atuambie wapi ilijaribiwa ikashindikana.Eti kisa viwanja vya timu za Ulaya vinajengwa kwa ubia wa makampuni ya ujenzi eti sisi tutashindwa tusipotumia njia hiyo hayo ni mawazo mgando.

Imagine watu milion 5 tu watoe sh 1000 kila mwezi ndani ya miezi 12 ni sh ngapi itakuwa imekusanywa ndo watajua inawezekana au la .Waandishi wetu ni bendera fuata upepo yaani wengi wanaviziana huyu kasema nini na yeye anapita humohumo
 
Hata mimi nipo kwenye kundi la haiwezekani.
Yaani unafananisha ujenzi wa kisiasa huo wa ccm tena wa miaka ile na huu wa sasa mkuu. Na ile ilikua ni ya wananchi wote, sasa hii ya kwenu wanasimba mlio hai mko millioni ngapi ndgu??

Acheni kujifariji ni haiwezekani.
 
Je ? Ikiwezekana utaweka wapi sura yako. Acha kukatisha watu tamaa kwa jambo linalowezekana.........
 
Jambo likichakuwa la watu wengi maneno yanakuwa mengi kuliko vitendo.

Simba ingekuwa club ya mtu binafsi (mfano Mo) angeshajenga uwanja hata kwa kukopa pesa bank.

Mo alikopa bilioni 450 bank of Africa kujenga kiwanda cha sukari.

Sidhani kama angeshindwa kukopa bilioni 50 kujenga uwanja wa club yake binafsi.

Club ya Tp mazembe imewezaje kujenga uwanja wake?
Alikwishalipa?
Kama ndio, basi ana msuli wa pesa

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Kujenga uwanja mbona simpo fyatuen brock zenu 20000 zungushen ukuta weken maget kila shabiki abebe kiti chake frexh mengine mdogo mdogo tena hata m150 haikat tabu yote ya nn kupitisha ma bakuli
 
Wale wachambuzi vilaza ni viwanja gani ccm wamejenga kwa pesa zao zaidi ya wananchi kuchangishwa
Hao wachambuzi uchwara wazo alilotoa Mo lingetoka kwa GSM wangekesha wakilipamba na kuliunga mkono. Tunapowaita vilaza na makanjanja siyo kama tunawadharau bali ndiyo wasifu wao kwani hawajadili hoja kwa mantiki bali wanajadili kwa kuangalia imetolewa na nani. Watu makini hujadili hoja bali watu wa hovyo hujadili watu.
 
Tangu jana mwekezaji wa Simba alipopost kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa amesikia kilio cha mashabiki wa Simba cha kutaka klabu yao iwe na uwanja wake wa kuchezea mechi za nyumbani na kuahidi kuchangia bilioni 2 kumeibuka mijadala kwenye redio na mitandao ya kijamii,kama ilivyo kawaida yetu Waafrika weusi wengine wanaunga mkono, wengine wanapinga, wengine wanaona haiwezekani na wengine wanadhihaki.

Wachambuzi wengi wa redio niliowasikiliza tangu jana na leo wanasema hakuna uwanja uliojengwa kwa fedha za harambee lakini viwanja vya CCM kama Kirumba, Majimaji, Sokoine, Ali Hassan Mwinyi na vinginevyo vilijengwa kwa wananchi kuchangishwa fedha, wafanyakazi walikatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao na wananchi wengine walichangia kwa njia nyingine. Majengo na ofisi za TANU na CCM wananchi walichangishwa, majengo ya makao makuu ya Simba na Yanga wanachama na wapenzi wa timu hizo walichangishana na kujenga majengo hayo.

Wachambuzi wetu wanadai Simba inatakiwa iende kwenye makampuni na kuingia ubia au kuuza jina la uwanja kama walivyofanya Arsenal kwa Emirates,hii njia inaweza ikawa ngumu kuliko kuchangishana, makampuni na mashirika mengi yamepitia kipindi kigumu cha mtikisiko wa uchumi uliosababishwa na Covid 19,pia kuna kampuni gani inayoweza kutoa bilioni 50,au 100 kwa ajili ya kujenga uwanja wa Simba, ligi kuu yenyewe kupata mdhamini wa bilioni 3 tu ni kazi kubwa,ukiona kampuni kama Vodacom inajitoa kudhamini ligi kuu ujue bado mpira wetu hauvutii wawekezaji...haulipi.

Pia uchumi wetu hausapoti uwekezaji wa aina hiyo,na ndiyo maana haya mambo ya makampuni kujenga viwanja unayaona Ulaya na Afrika Kusini tu,kwa sababu biashara zao ni kubwa na uchumi wao ni mkubwa.

Simba wanaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana ila wanatakiwa kujua kujenga uwanja si kazi ndogo,wanachotakiwa kufanya ni kujenga kwa awamu huku wakiendelea kuutumia,Simba haiwezi kushindwa kujenga uwanja wa nyasi bandia,wenye taa huku watazamaji wakiwa wamekaa kwenye majukwaa ambayo hayana viti kama wanavyofanya KirumbMa Majimaji, Sokoine,Samora na vingine.Kitu cha muhimu uwanja ujengwe kwa kuruhusu marekebisho, upanuzi nk.

Kitu kingine kwenye kuchangishana wanaweza kukusanya fedha kwa kuweka viwango na motisha fulani kwa wachangiaji mfano wanaweza kusema anayechangia kuanzia 100,000 anapewa cheti kama kumbukumbu na shukrani hii itasaidia watu wengi wapate morali ya kuchangia,pia majina yao yaandikwe na yawekwe nje ya uwanja.Wale wanaotoa kuanzia milioni 10 ,wanapewa viti maalum vya kukaa uwanjani yaani VVIP,nk.

Faida za kumiliki uwanja ni
kupata fedha zaidi,niliwahi kusikia wanalipia milioni 20 kwa kila wanavyocheza mechi uwanja wa Mkapa,wakiwa na uwanja wao hizi fedha hawatalipa.
Wataweza kupata fedha kwa kukodisha majukwaa na mageti kwa ajili ya matangazo,mfano geti A linaweza kukodishwa kwa kampuni X na kuitwa Gate X,badala ya geti A.Jukwaa kuu wanaweza kulikodisha kwa kampuni ya Dcom na wakaliita jukwaa la Dcom nk.

Kwahiyo Simba wanaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana na ninawatakia kila la heri,maneno ya wakosoaji yanatakiwa yawe mbolea ya kuanza kujenga uwanja.
Kama kuna Simba members na funs kama 10m Tanzania nzima na kila moja akatoa buku kwa mwezi, inamaana mwisho wa mwezi watakuwa na TSH 10b, ikifanyika kwa miezi mitatu inafika 30b. ( Tambua kuna watakaotoa laki moja, milioni moja, elfu kumi na pia wapo ambao hawatoachochote , Kwa wale wahenga hivi ambavyo leo vinaitwa viwanja vya CCM ndivyo vilivyojengwa
 
Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 ulijengwa kwa gharama ya Tsh 128,912,000,000 (129 Billion) Kwa mchango wa 2B inabaki 127B.Je fedha hizi wanasimba wataweza kukamilisha? Nadhani kama Mmiliki wa club angeongeza dau kiasi cha kutosha na wanasimba wachangie kiasi chao ili azma hii iweze kùfanikiwa
 
Jambo likichakuwa la watu wengi maneno yanakuwa mengi kuliko vitendo.

Simba ingekuwa club ya mtu binafsi (mfano Mo) angeshajenga uwanja hata kwa kukopa pesa bank.

Mo alikopa bilioni 450 bank of Africa kujenga kiwanda cha sukari.

Sidhani kama angeshindwa kukopa bilioni 50 kujenga uwanja wa club yake binafsi.

Club ya Tp mazembe imewezaje kujenga uwanja wake?
Bilioni 50 na uwanja utoshe kwa derby ua Simba na Yanga?? Haiwezekani.Iwanja wa Taifa umejengwa kwa Billioni 229 na kuna wakati hautoshi kwa idadi ya mashabiki,Bilioni 50 ni kitu gani??
 
Uwanja wa Taifa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 ulijengwa kwa gharama ya Tsh 128,912,000,000 (129 Billion) Kwa mchango wa 2B inabaki 127B.Je fedha hizi wanasimba wataweza kukamilisha? Nadhani kama Mmiliki wa club angeongeza dau kiasi cha kutosha na wanasimba wachangie kiasi chao ili azma hii iweze kùfanikiwa
Simba hawezi kujenga uwanja wa kuingiza mashabiki 60000 kama cha Mkapa, wao wanasema angalau mashabiki 30000, lakini pia kuna sababu nyingi ambazo zinapelekea kutofautisha gharama za ujenzi, uwanja wa Mkapa umetumia USD 56ml na unaingiza watu 60000 ila ubora wake ni mdogo sana compared na viwanja ambavyo vimecost USD 40 tu huko uarabuni

So kuna viwanja vimetumia less than that na vinaingiza mashabiki wachache zaidi au wengi zaidi, kwhyo inategemea material, design na wajenzi wenyewe plus budget ya wahusika, wanaweza jenga kiwanja kama cha Azam ila tofauti ikaja kwenye capacity tu

Japokuwa kiuhalisia hiyo 2b aliyoahidi Mo bado ni kiasi kidogo Kweli ila inawezekana ni kwa sababu hakuna actual amount ambayo teyari imetolewa kwa kufanya tathmini, maana ata kama watasema wajenge uwanja wa cheapest kabisa gharama inaweza range kwenye 30-40b kwahiyo bado ni ndogo
 
Back
Top Bottom