Simba imeenda kuutumia uwanja wa Jamhuri bila kuujaribu

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,193
8,010
Hii timu kimya kimya bila mbwembwe niliacha kuiangalia, nafuatilia tu matokeo yake kutokana na kwamba kuna upuuzi mwingi sana ambao lawama zote zinaangukia katika uongozi.

Simba iliuchagua uwanja wa Jamhuri Morogoro kama uwanja wake wa nyumbani ila cha kushangaza, wachezaji wa Simba wameenda kwenye mechi ya leo dhidi ya Prisons huku wakiwa hawajafanya mazoezi kabisa katika uwanja huo. Timu kubwa itafanyaje kosa kubwa la kiufundi kama hilo?

Baada ya kuwatesa vya kutosha mashabiki wa Dar es Salaam hadi mpaka leo wengi sana wameikatia timu tamaa, sasa uongozi umeamua kuwapelekea uchungu mashabiki wa Simba wa mikoani. Sababu ya kuukimbia Chamazi siyo ishu za kuhujumiwa kama wanavyodai, ni kwa sababu mashabiki wa Dar hawana mwamko sana na hii timu kwa sasa. Bado huko mikoani unaweza kuwaokota okota wakajaza uwanja ila.....

Tukiendelea hivi, na hao wa mikoani nao watakata tamaa na hii timu na baada ya miaka 2 Simba itakuwa timu ya kawaida sana katika ligi.
 
Ni ya kawaida mpaka ikifungwa 5 yanalipiwa mabango na kuku zinapikwa na chapati.
Kiredio anakushangaa
 

Attachments

  • FB_IMG_17097394475222637.jpg
    FB_IMG_17097394475222637.jpg
    144.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom