Je, Simba SC inaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana?

umeshachanga?
IMG-20211219-WA0004.jpg
 
Tangu jana mwekezaji wa Simba alipopost kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa amesikia kilio cha mashabiki wa Simba cha kutaka klabu yao iwe na uwanja wake wa kuchezea mechi za nyumbani na kuahidi kuchangia bilioni 2 kumeibuka mijadala kwenye redio na mitandao ya kijamii,kama ilivyo kawaida yetu Waafrika weusi wengine wanaunga mkono, wengine wanapinga, wengine wanaona haiwezekani na wengine wanadhihaki.

Wachambuzi wengi wa redio niliowasikiliza tangu jana na leo wanasema hakuna uwanja uliojengwa kwa fedha za harambee lakini viwanja vya CCM kama Kirumba, Majimaji, Sokoine, Ali Hassan Mwinyi na vinginevyo vilijengwa kwa wananchi kuchangishwa fedha, wafanyakazi walikatwa fedha kutoka kwenye mishahara yao na wananchi wengine walichangia kwa njia nyingine. Majengo na ofisi za TANU na CCM wananchi walichangishwa, majengo ya makao makuu ya Simba na Yanga wanachama na wapenzi wa timu hizo walichangishana na kujenga majengo hayo.

Wachambuzi wetu wanadai Simba inatakiwa iende kwenye makampuni na kuingia ubia au kuuza jina la uwanja kama walivyofanya Arsenal kwa Emirates,hii njia inaweza ikawa ngumu kuliko kuchangishana, makampuni na mashirika mengi yamepitia kipindi kigumu cha mtikisiko wa uchumi uliosababishwa na Covid 19,pia kuna kampuni gani inayoweza kutoa bilioni 50,au 100 kwa ajili ya kujenga uwanja wa Simba, ligi kuu yenyewe kupata mdhamini wa bilioni 3 tu ni kazi kubwa,ukiona kampuni kama Vodacom inajitoa kudhamini ligi kuu ujue bado mpira wetu hauvutii wawekezaji...haulipi.

Pia uchumi wetu hausapoti uwekezaji wa aina hiyo,na ndiyo maana haya mambo ya makampuni kujenga viwanja unayaona Ulaya na Afrika Kusini tu,kwa sababu biashara zao ni kubwa na uchumi wao ni mkubwa.

Simba wanaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana ila wanatakiwa kujua kujenga uwanja si kazi ndogo,wanachotakiwa kufanya ni kujenga kwa awamu huku wakiendelea kuutumia,Simba haiwezi kushindwa kujenga uwanja wa nyasi bandia,wenye taa huku watazamaji wakiwa wamekaa kwenye majukwaa ambayo hayana viti kama wanavyofanya KirumbMa Majimaji, Sokoine,Samora na vingine.Kitu cha muhimu uwanja ujengwe kwa kuruhusu marekebisho, upanuzi nk.

Kitu kingine kwenye kuchangishana wanaweza kukusanya fedha kwa kuweka viwango na motisha fulani kwa wachangiaji mfano wanaweza kusema anayechangia kuanzia 100,000 anapewa cheti kama kumbukumbu na shukrani hii itasaidia watu wengi wapate morali ya kuchangia,pia majina yao yaandikwe na yawekwe nje ya uwanja.Wale wanaotoa kuanzia milioni 10 ,wanapewa viti maalum vya kukaa uwanjani yaani VVIP,nk.

Faida za kumiliki uwanja ni
kupata fedha zaidi,niliwahi kusikia wanalipia milioni 20 kwa kila wanavyocheza mechi uwanja wa Mkapa,wakiwa na uwanja wao hizi fedha hawatalipa.
Wataweza kupata fedha kwa kukodisha majukwaa na mageti kwa ajili ya matangazo,mfano geti A linaweza kukodishwa kwa kampuni X na kuitwa Gate X,badala ya geti A.Jukwaa kuu wanaweza kulikodisha kwa kampuni ya Dcom na wakaliita jukwaa la Dcom nk.

Kwahiyo Simba wanaweza kujenga uwanja kwa njia ya kuchangishana na ninawatakia kila la heri,maneno ya wakosoaji yanatakiwa yawe mbolea ya kuanza kujenga uwanja.
UPIGAJI TU, WAULIZE HADI LEO IMEKUSANYWA SHILINGI NGAPI UONE MAPOVU HAPA...

TRANSPARENCY IKO WAPI KWA CLUB KUBWA KAMA SIMBA?
 
.... Djigui Diara aliondoka akiacha Simba ina point 24

Anarudi anakuta Simba ina point 25

Anajiuliza Ligi ilisimama au???!!
 
Mtu anaposema haiwezekani atuambie wapi ilijaribiwa ikashindikana.Eti kisa viwanja vya timu za Ulaya vinajengwa kwa ubia wa makampuni ya ujenzi eti sisi tutashindwa tusipotumia njia hiyo hayo ni mawazo mgando.

Imagine watu milion 5 tu watoe sh 1000 kila mwezi ndani ya miezi 12 ni sh ngapi itakuwa imekusanywa ndo watajua inawezekana au la .Waandishi wetu ni bendera fuata upepo yaani wengi wanaviziana huyu kasema nini na yeye anapita humohumo
Tupe muendelezo vp tuna sh ngapi mpka sasa
 
Mtu anaposema haiwezekani atuambie wapi ilijaribiwa ikashindikana.Eti kisa viwanja vya timu za Ulaya vinajengwa kwa ubia wa makampuni ya ujenzi eti sisi tutashindwa tusipotumia njia hiyo hayo ni mawazo mgando.

Imagine watu milion 5 tu watoe sh 1000 kila mwezi ndani ya miezi 12 ni sh ngapi itakuwa imekusanywa ndo watajua inawezekana au la .Waandishi wetu ni bendera fuata upepo yaani wengi wanaviziana huyu kasema nini na yeye anapita humohumo
Kilimo cha matikiti
 
Back
Top Bottom