SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,151
- 7,916
Nimewaza na kuwazua, kwa muda sasa Simba imeweka kambi yake maeneo ya Mbweni na ni umbali mdogo sana kutoka uwanja wa Meja Generali Isamuhyo ulipo. Yaani umbali wake ni mdogo kiasi kwamba katika mechi inayokuja ya JKT vs Simba, Simba wanaweza kuamua siku ya mechi kutembea kwa miguu kutoka kambini hadi uwanjani kama ambavyo Deportivo de Utopolo wanafanyaja kwenye derby kutokea Uhasibu hadi kwa Mkapa.
Mwanzo nilishtushwa na taarifa za mechi ya Simba na JKT kuhamishiwa katika uwanja huu. Nimeangalia video, yaani ni uwanja ambao bado uko katika ujenzi mkubwa na unaweza kusema hata 50% ya ujenzi wanaotegemea kufanya bado haujakamilika. Bado hakuna majukwaa, bado kuta hazijapakwa rangi, sehemu yatakapokaa majukwaa bado ni vumbi tupu hakuna hata pavement, hata mlango wa kuingilia umeegeshwa tu na umefunikwa na plastiki. Kuisalama ungeweza kusema sehemu ile siyo sahihi kupeleka idadi kubwa ya watu bila tahadhari kwa sababu ujenzi unaendelea.
Niliwahi kusema eneo ilipo Simba Mo Arena sina uhakika kama linatosha kujenga uwanja wa mashindano wenye majukwaa hata wa size ya ule wa Azam halafu wakati huo huo ukatimiza malengo ya kuweka pitch za kutosha za mazoezi kwa timu zote za Simba (Senior, Wanawake na za Vijana) maana itabidi kila timu iwe na uwanja wake wa mazoezi ili kutovuruga ratiba za kila timu, hapo hapo uwe na pitch ya nyasi bandia. Viongozi walituambia mipango pia ni kuweka hostel za timu zote hapo hapo na miundombinu mingine ikiwemo gym na parking ya kutosha. Hapo unaona kuwa kujenga uwanja wa mashindano pale inaweza isiwe jambo linalowezekana labda kama eneo litapanuliwa zaidi.
Hivi Simba ikiendelea na mipango mingine ya kuboresha mazingira ya Mo Simba Arena kama hosteli za vijana na wanawake halafu ikaingia ushirikiano na Jeshi kujenga uwanja huu wa Isamuhyo kwa kushare gharama za ujenzi halafu baadae kwa Simba kupeleka mechi zake zote za ligi zitakazoingiza fedha nyingi kwa haraka zaidi, hii inaweza kuwa smart move sana kwa pande zote.
Jeshi pia lina access ya vitu vingi ambavyo Simba itakuwa imetua mzigo wa uendeshaji na usimamizi wa uwanja mfano masuala ya ulinzi wa uwanja na maintenance mbalimbali, nk.
Hili wazo niliwahi kuliwaza kwa uwanja wa Uhuru ila ukitazama lina make sense zaidi kwenye uwanja huu wa Isamuhyo. Ninachoomba tu waweke siti standard kwa mashabiki kama zile za kwa Mkapa au Amaan, siyo mabenchi ya zege au ya mbao kama ya Azam Complex. Siku hizi mchina amerahisisha mambo sana hakuna sababu ya kushindwa kuweka viti vya plastiki katika uwanja wa mpira.