Je Siasa ni ajira ya Ukoo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Siasa ni ajira ya Ukoo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ABEDNEGO, Jan 19, 2010.

 1. ABEDNEGO

  ABEDNEGO Senior Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 109
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wadau nisaidieni katika hili kwani linanitatiza sana,Hivi ni kweli kwamba siasa ni ajira inayoendana na ukoo?Kwani mara nyingi naona kina Kennedys,Bushs,Kenyattas,Kikwetes,Kabilas nk ndiyo wanashika nafasi za kisiasa au madaraka ya kuongoza wengine?Nina uhakika wadau wengi hapa wameelewa ni maana yake.Nihabarisheni......Maana jana nilimtembelea ndugu yangu ambaye ni Mh.Waziri na kumkuta mdogo wake akijitutumua kuwa anaenda kugombea Ubunge hali namjua kuwa kichwani hamnazo kabisaa!!!
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Siasa ni kuongoza watu na ukoo wenu umewahi kuongoza watu wana tabia ya kuamini like father like son/daughter

  Siasa kwa aina ya demo-cracy ni siasa ya kuchaguliwa na watu si kwakuwa unazo ila kama unaweza "kuchaguliwa" na watu..waweza kutumia pesa, jina la ukoo wako, usanii, kununua systems (e.g. NEC) lakini mategemeo yao uwe na akili

  Taratibu za kupata viongozi wa siasa ndio zinakuletea viongozi wabovu...kwasababu wanakuwa wamesoma na kujua tricks of the game! rough or smooth!

  Myself I don't give a damn to demo-cracy..to have a leader! leader mzuri upstairs kuna namna nzuri ya kumpata....siyo uchaguzi...ukitaka darasa ..litaendelea..
   
 3. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa nchi zilizoendelea yawezekana kuwa ni kweli kwa maana ya kuwa uongozi ni kipaji,Hapa kwetu hakika ni tamaa na ujasiria mali wa kufuata mkondo upi unaleta hela kwa wepesi katika familia.Si kweli kuwa viongozi wetu sisi hapa Bongo tunawatambua kwa vipaji vya uongozi ni kinyume chake zaidi,Ndo maana wapo viongozi tuliowachagua kwa haiba zao ,kwa sura zao,kwa utajiri wao,kwa ahadi zao hewa nk.Kwa hali hiyo tumekosa viongozi wabunifu na wenye vipaji vya kuongoza.Sanduku la kura ni hatua ya mwisho tuu ya kuidhinisha viongozi kwani Kiongozi wa kweli huchaguliwa hata kabla ya kupigiwa kura.
   
 4. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,274
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Katibu Mkuu wa CCM, Mh Makamba alishasema kuwa mtoto wa mwanasiasa atakuwa mwanasiasa kwa kuwa anaiga kazi ya baba yake na wa mkata mkonge atakuwa mkata mkonge. sijui wewe baba yako ana kazi gani. Pole sana.
   
 5. Mtabiri

  Mtabiri Senior Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: Jun 23, 2009
  Messages: 152
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Loh, kwa mtaji huo basi tumekwisha!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kwa mahali ambapo hakuna corruption, hiyo inaweza ku'apply, maana mtu wa familia au ukoo wa kiongozi anakuwa kwa kiasi kikubwa anaelewa matatizo anayokumbana nayo mtangulizi wa familia hiyo ndani ya uongozi, kwahiyo ataingia kwa kumaanisha!

  Lkaini kwa sehemu kama huku kwetu, ni kinyume kabisa...mtu anapigania aongoze watu, kitu ambacho kinaleta hisia mbaya sana, na inaonyesha wazi kwamba nia za wengi ni ajira na maslahi!
   
 7. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ulimtembelea waziri gani mkuu?
   
 8. r

  rimbocho Member

  #8
  Jan 19, 2010
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwani mtoto wa marehemu naye si mbunge, eti kisa babaake nae alikuwa mwana siasa. Mtoto wa kikwete si naye mjumbe wa nec, mtoto wa mzindakaya, mtoto wa nauye
   
Loading...