Hawana hayo majibu na walijaribu kukumbatia nyuki na zimewauma sasa wanakimbia kujaribu kubadili mwelekeo wa mjadala.
tumejaribu kukumbatia Nyuki ,ila naomba upige hii namba na uulize kwa makini kama RIz anahusika na Suala la DEEP Green na Mzee huyu atakupa jibu zuri+255 784 666995
tumejaribu kukumbatia Nyuki ,ila naomba upige hii namba na uulize kwa makini kama RIz anahusika na Suala la DEEP Green na Mzee huyu atakupa jibu zuri +255 784 666995
na picha ya huyo mzee ni hii hapa.
Kwa hiyo siku hizi Dr Slaa ndio amekuwa PRO wa Ridwan? hebu acha utani huko. Jibu maswali jamani
Asha
Muulize Dr. Slaa anawajua au Muulize Lissu.Mie simtetei RIZ ila naeleza ukweli kuhus Riz.
Kwani chadema hamna sera Nzuri zaidi ya kuchukua mabaya ya CCM ili myasemee?tafuteni sera yenau na ndio maana huwa mnashindwa katika uchaguzi wenu!
Mie nitawaunga Mkono kama mkinihaidi yafuatayo.
Mna Mkakati gani wa kuhakisha mnashinda uchguzi wa 2010.,2015 na 2020,Asha naona una mahusiano na RIZ mpoaka kakwambia anataka kugomba 2020?
Sasa unaanza matusi. Usiniweke kundi moja na ma-miss tafadhali. Mimi nilitaja wenye probability au possibility ya kufaaa kuwa Marais mwaka 2020. Kwa hiyo unataka kusema mimi nina mahusiano na Zitto, Mwanakijiji, Kitila nk niliowataja?
Wakishindwa hoja, wanaanza vioja na vihoja.
hebu jibu maswali yangu huko, unazidi kuniondolea imani
Ulianza kwa kasi, sasa kadiri mambo yanavyomwagwa naona unapunguza kasi. Usinyamaze jamani, hebu tueleze ukweli
Asha
It is getting nastier. Hawa jamaa wanatumaliza. Hii habari ni kweli na inaonekana imeshasambaa sana huko nyumbani. Na it seems there is a bigger number of bigger fish that are involved than we already know. Kuna mtu kanitumia email na sehemu inasema hivi:
"Haya kaka, mambo yanazidi kuiva. Hapa kuna kampuni moja lilichota bilioni nane 2005 na kufilisiwa 2006. Waliohusika kulisimamia kampuni hilo ni kampuni ya advocate ambapo ridhiwani kikwete ni mkurugunzi na fatuma karume kaajiriwa. Mmoja wa wakurugenzi ya hiyo law firm kateuliwa kuwa jaji, Mwingine ndo aliteuliwa kuwa mfilisi wa ile kampuni na wengine ni hao watoto wa vigogo".
Hii kampuni tuliwahi kuizungumzia huko nyuma kwamba ni network moja kali sana katika kufanikisha ufisadi.
Nilikuwa sijui kama Mujilizi ameteuliwa kuwa judge.Kuna kaharufu fulani kabaya hapa kanazidi kujidhihirisha.
Ila tunaomba maswali aliyouliza dada Asha yatolewa ufafanuzi, na kwamba baadhi ya wachangiaji hapa kama hawana hoja waache kushinikiza kututoa nje ya mada hii.
Gembe na Kasheshe
Niliwahi kumtaja siku nyingi huko nyuma kwamba namuona kama mmoja wa vijana wanaoweza kuwa marais wa Tanzania siku za usoni. Habari ya leo imenishangaza
Asha
Sikujua kama kuna siku Gembe mchangiaji Mzuri sana wa JF angelikuwa mbogo kiasi hiki. Mkuu Umeshikwa pabaya au nini?
Mkuu nafikiri yamekukuta, tuliza bori mkuu.
Nadhani kichwa cha habari hii kina alama ya kuuliza - hii sio conclusive remark unless una definition tofauti ya hili
Sister Mwafrika
Nakwambia! Tutaona mengi leo. Sasa mpaka GT naye hajui tofauti ya Swali na Conclusion. Mbona jamani mnazidi kunipa shaka kuhusu Ridhwan?
Nipeni majibu ya maswali yangu jamani
Asha
Ahhhaaaa sasa naona tunaanza ku break THROUGH
Inawezekana ikawa mimi nilikuwa na slight oversight kwenye hilo and i will take the responsibility
sasa basi nashauri MODS Wwaihamishe hii thread na kuipeleka kule kwenye forum ya NAULIZA HIVI?
nadhani kule ndiko hii thread inakostahili kuwa
Game Theory sikutegemea utatetea issue ya Ridhwani hivyo! Truly my brother!
Dada Asha hajafanya kitu chochote kibaya. hii habari iko front page ya Mwanahalisi. Sasa hata mimi nilijiuliza maswali mengi na ndo maana dada huyu kaleta mada hapa. Hebu kumbukeni Richmond ilivyokuwa dismissed na hata hii issue ya EPA, lakini kumbe....
Naomba tusitukanane na tusitoke nje ya mada maana I am VERY interested sasa. Kama mtu anachakuchangia kwenye hoja hii aweke otherwise naomba tusipotoshe mada.
Gembe: naomba u-address hii issue ya Fatma Karume na Ridhwan Kikwete kuwa wote associates at IMMA. What is the deal? Alafu IMMA imekiri kuhusika na registration ya Deep Green, kulikoni?
Tatizo sio kutetea bali things dont just add up
Mtu anakuja analeta thread halafu anatuuliza sisi tumpe majibu
wapi na wapi?
Richmond na BOT zote ziliambatana na maelezo ambayo yalikuwa yamejaa vielelezo vingi tuu
hii mzee haijakaa sawa na nadhani ni haki yetu ku scrutinize kabla ya kujua mchele ni upi na pumba ni zipi...hiyo si dhambi