Je, Ridhwan Kikwete naye ni fisadi?

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
45
Jamani!

Eti mi niliwahi kuandika hapa vijana ambao mmoja wao anatarajiwa kuwa Rais wa Tanzania wa baadaye. Nilimtaja Zitto, Mwanakijiji, Kitila, Ridhwan Kikwete nk. Madela wa Madilu naye akaiongeza mwenyewe kwenye orodha. Nimesikitika leo Ridhwan Kikwete ametajwa naye na gazeti la Mwanahalisi kuhusika na ufisadi wa Deep Green. Hivi ni kweli jamani kuwa na yeye ni fisadi? Kama ni kweli si anachafua jitihada za Rais Kikwete za kupambana na ufisadi Tanzania? Sasa nani watanzania tumwamini kumpa uongozi wa nchi yetu siku za baadaye?

Asha
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka na mtoto wa fisadi ni fisadi. Kama pesa za BOT ziliingia kwenye kampeni ya Kikwete wakati wa uchaguzi wa 2005 via Kagoda farm,na yeye alitumia hizo pesa na sasa anatumia jaja ya nyani kuunda tume ya kurecover hizo pesa na hili tusijue kama CCM ilipata mgao wa BOT,naye ni fisadi. Hivyo sishangai kuona ridhwan naye yumo kwenye hizi scandal.
 
Jk knows Richmond scums, sababu alimuondoa mwane kwenye hiyo deal, so don't tell me he is clean.
 
Haya mambo yataendelea kufichuka polepole hadi itafika mahali watashindwa kuwa na ground ya kukana. Tungoje tu, Mungu hamfichi mnafiki. Kama waliiba watabainika wote, kuanzia babu mpaka mjukuu
 
kalini ni kweli hivi sasa inaonekana karibu wote ni wachafu sasa wasiwasi wangu ni kwamba nani atakayewahukumu maana hata huyo wa kuhukumu mwisho utasikia naye ni mchafu au labda tutaliomba jeshi liingilie kati?nalo tayari pale keshawekwa mwinyi na huyo mpiga filimbi wa sisiem ambaye sikutarajia kabisa kama angeweza kuchukua nafasi nyeti namna hiyo serikalini kweli siasa mchezo mchafu
 
[
B]Hivi ni kweli jamani kuwa na yeye ni fisadi? Kama ni kweli [/B]

Bibi Asha,

Heshima mbele, je umeshakuwa na uhakika iwapo swali lako hapo juu limejibiwa kwanza? Mimi nilifkiri kwanza inahitajika ku-establish kama kweli kijana ni fisadi as of your swali, lakini badala yake naona tumeshaanza na hukumu moja kwa moja, kulikoni wakuu?

Swali lahoja ya msingi ni kama ni kweli kijana ni fisadi au?
 
Bado najiuliza. Ametajwa kushiriki kwa mgongo wa IMMA advocates. Ni kweli? Rais Kikwete mwenyewe anaonyesha kuchukia rushwa

Asha
 
Swali lahoja ya msingi ni kama ni kweli kijana ni fisadi au?

Kuna strong circumstacial evidence kuonyesha kuwa kijana naye ni fisadi. Yaliyotokea yameshamwekea label hiyo.
Hakwenda pale kwenye kampuni ya mawakili kwa bahati mbaya. Hiyo kampuni ndiyo iliyohusika kusajili Deep Green ambayo nayo imeiba mabilioni kutoka serikalini. Kampuni hiyo hiyo ndiyo ilishughulika kuifilisi Deep Green baada ya malengo yake kukamilika. Tunajua kuwa miradi kama Deep Green ndiyo ilitumika kupata fedha za kampeni. Ilikuwa lazima katika mradi mkubwa na muhimu kama huo kuwa na mtu wa karibu atakayechunga maslahi. Ndio maana aliajiriwa hapo hata kabla hajamaliza shule.
 
Bado najiuliza.

Rais Kikwete mwenyewe anaonyesha kuchukia rushwa

Asha

Ok, anaweza kuonyesha hivyo, lakini je ni kweli kwamba anachukia? Nauliza hivi kwa sababu tunajua kuwa mtazamo na matendo ya mtu sio mara zote yanaendana. Kwa maoni yangu tatizo moja la Rais wetu ni kwamba anavyofikiri sivyo anavyosema na anavyosema sivyo anavyotenda! Kwa maneno mengine ni kwamba Rais wetu anatenda anayoyafikiri na sio anayoyasema. Bahati mbaya ni kwamba hatuwezi kujua anayoyafikiri!
 
Swali lahoja ya msingi ni kama ni kweli kijana ni fisadi au?

Kuna strong circumstacial evidence kuonyesha kuwa kijana naye ni fisadi. Yaliyotokea yameshamwekea label hiyo.
Hakwenda pale kwenye kampuni ya mawakili kwa bahati mbaya. Hiyo kampuni ndiyo iliyohusika kusajili Deep Green ambayo nayo imeiba mabilioni kutoka serikalini. Kampuni hiyo hiyo ndiyo ilishughulika kuifilisi Deep Green baada ya malengo yake kukamilika. Tunajua kuwa miradi kama Deep Green ndiyo ilitumika kupata fedha za kampeni. Ilikuwa lazima katika mradi mkubwa na muhimu kama huo kuwa na mtu wa karibu atakayechunga maslahi. Ndio maana aliajiriwa hapo hata kabla hajamaliza shule.

Navyofahamu mimi Ridhwani hakuajiriwa Imma kabla hajamaliza shule,bali alikwenda pale kama mwanafunzi katika program ya internship,na baada ya kumaliza wakambakiza pale yeye na wenzake wawili.Hata hivyo tuhuma za ufisadi dhidi yake zinapaswa kuchunguzwa zaidi ili tujiridhishe kuhusika kwake,na kama kweli kampuni ya Imma inahusika na moja ya bogus contracts basi labda ndio maana jamaa(JK) akaamua kulipa fadhila kwa kumteua masha kuwa waziri,maana kwanza alimuajiri mtoto wake yaani ridhwani na pili hiyo mikataba.Hizi facts zinatakiwa kuwa corroborated hebu mwenye facts azishushe zaidi hapa kabla hatujaamua kutoa hitimisho
 
Huyu kijana amekuwa anatumia nafasi za CCM vibaya tangia akiwa Hull University .Mikutano kibao ya CCM kuitwa kushiriki majuu yeye alienda kwa jina la vijana wa CCM .Huu pia ni ufisadi .Nasikia alinunua gari kuuuubwa la gharama kuuuubwa Baba yake akalikataa .Swali anafanya kazi wapi kwa mshahara upi na aine ile ya gari ?
 
Navyofahamu mimi Ridhwani hakuajiriwa Imma kabla hajamaliza shule,bali alikwenda pale kama mwanafunzi katika program ya internship,na baada ya kumaliza wakambakiza pale yeye na wenzake wawili.Hata hivyo tuhuma za ufisadi dhidi yake zinapaswa kuchunguzwa zaidi ili tujiridhishe kuhusika kwake,na kama kweli kampuni ya Imma inahusika na moja ya bogus contracts basi labda ndio maana jamaa(JK) akaamua kulipa fadhila kwa kumteua masha kuwa waziri,maana kwanza alimuajiri mtoto wake yaani ridhwani na pili hiyo mikataba.Hizi facts zinatakiwa kuwa corroborated hebu mwenye facts azishushe zaidi hapa kabla hatujaamua kutoa hitimisho

Ni kweli jamani, hebu mnaojua mtueleze:

Ridhwan Kikwete amehusika na kashfa ya Richmond?

Ridhwan Kikwete aliajiriwa IMMA kabla ya kumaliza shule?

Ridhwan Kikwete alikwenda kusomeshwa Hull kwa mchango wa IMMA?

Ridhwan Kikwete aliwasaidia IMMA kwa namna yoyote katika suala la Deep Green?

Ridhwan Kikwete alifahamu chochote kuhusu Deep Green wakati wa kampeni?

Ridhwan Kikwete anaukaribu gani na Masha wa kibiashara?

Ridhwan Kikwete ni kiunganishi kati ya Kikwete na ile Kampuni ya kina Masha ya Madini ule Mererani?

Ridhwan Kikwete alishiriki kufanikisha Kikwete kuchangiwa kwenye kampeni na yale makampuni ya madini kule Mererani?

Ridhwan Kikwete alisadia vipi IMMA kupewa tenda za uwakala na masuala ya mikataba ya makampuni makubwa ya madini? Je, ni wakati Masha akiwa naibu waziri wa wizara husika, kabla au baada?

Ridhwan Kikwete ana nafasi gani IMMA, ni mtumishi wa kawaida au ni partner?

Je- anafaa kuwa Rais wa Tanzania katika miaka ijayo ukimlinganisha na Zitto, Kitila, Mwanakijiji na Madela wa Madilu?

Asha
 
associate...............ni kama patner au..;patner ..wameshindwa tu kubadili jina ili kuongezea jina lake kwenye initial za kampuni
 
associate...............ni kama patner au..;patner ..wameshindwa tu kubadili jina ili kuongezea jina lake kwenye initial za kampuni

Kwa hiyo ni IMMMAK au KIMMMA? Magai, Mujilizi, Ishengoma, Masha, Kikwete na nani? Je, kuingia kwake kama partner- be it associate or full kumetokana na nini? Bado nahitaji majibu ya maswali yangu. Nina mawazo mengi sana, I still have some faith on this boy. Can he be our next president?

Kikwete kumteua Mujilizi kuwa Jaji wa Tanzania kuna uhusiano wowote na mtoto wa Kikwete kuwepo pale?

Je, yaliyoandikwa na MWANAHALISI leo yana ukweli wowote? Je, ni kweli amehusika na Deep Green? Kwanza Deep Green ni wakina nani na walifanya nini kustahili malipo yale toka serikalini mwaka 2005?

Asha
 
Jamani naomba nichangie:
IMMA wanaonekana kuwa wanawatumia watoto wa vigogo ili kuwa karibu nao. Sikujua kuwa Ridhwan ni associate pale lakini najua wamemchukua Fatma Karume kama associate!!!!

Do you see the pattern?

Mimi nadhani Masha na wenzake lazima wachunguzwe tena kwa karibu sana. Something IS definitely wrong
 
Bado najiuliza. Ametajwa kushiriki kwa mgongo wa IMMA advocates. Ni kweli? Rais Kikwete mwenyewe anaonyesha kuchukia rushwa

Asha

BI ASHA,

KUNA WANAOJIFANYA WANACHUKIA KITIMOTO WANAPOKUWA NA WANAOKICHUKIA KWELI KWELI, LAKINI WANAPO KUWA NA WATUMIAJI WAKE NAO N WATUMIAJI. NAONA TUPATE UKWELI KWANZA. TUSISEME BABA YAKE ANAONEKANA ANACHUIA RUSHWA BILA KUWA NA UHAKUKA.

LONG LIVE TANZANIA.
 
Ridhwani anatafuta umaarufu,Hakuna uhusiano wowote na sula la DEEP Green,hawa jamaa wa mwanahalisi na wenyewe wananunuliwa
Rishwan kamaliza Mlimani Mwaka 2005 yaani mwaka wa chuo 2004/2005 na kaanz akazi pale IMMA baada ya Uchaguzi.

hii yote ni danganya toto ya kufuta mambo yote ya Lowassa,Kwani Kubenea Hamumjui anasimamia wapi???

tusimame pamoja kwa maendeleo ya kweli,Mwanasiasa wa ukweli ni MMoja tu na nitakuja kumtaja baadaye,Juzi nimepewa kuhusu yote yahusuyo Upinzani na nikiyasema aki ya mbongo nakuamini utabadili muelekeo wako,

hakuana cha Chadema wala nini

CCM ni taifa kubwa
 
Back
Top Bottom