Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 13,226
- 26,048
Amani iwe nanyi wadau
Leo ninakuja na Swali hili, Je, Rais Samia Suluhu Hassan ndo Deng Xiaoping wa Tanzania?
Kwa wale msiojua Deng Xiaoping ni Rais wa China aliyechukua usukani wa Uongozi wa China baada ya kifo cha Rais wa Kwanza wa China Mao Zedong. Mao Zedong alijulikana kwa wachina kama Rais mwenye msimamo mkali usioyumba ambaye hakupatana na Marekani na nchi za Magharibi. Aliiongoza China Kwa mkono wa Chuma ila katika kipindi chake China ilikuwa nchi yenye uchumi mbovu sana kutokana na Sera zake za kukataa uwekezaji kutoka nje na kugombana na nchi za magharibi.
Kwa wachina wengi pamoja na kumuheshimu sana Mao ila wanamchukulia Deng Xiaoping Kama Baba wa Mapinduzi ya Kiuchumi ya China. Hii ni Kwa sababu Deng Xiaoping ndo mtu aliyekuja kutengeneza China yenye siasa za kikomunist Ila yenye uchumi imara wa kibepari ulioongozwa na msemo wake “It doesn’t matter if a cat is white or black , as long as it catches a mice, it’s a good cat”
Kwa wasioelewa kimombo Deng Xiaoping alikuwa anamaanisha haijalishi paka ni mweupe au mweusi Ila ingawa anakamata panya basi huyo ni paka mzuri
Sera hii ya Deng Xiaoping ndo ilisababisha China kuanza kukaribisha uwekezaji mkubwa kutoka Magharibi ulioingiza fedha na mitaji mikubwa nchini China na hatimaye Leo hii China ni Taifa la pili kwa kuwa na uchumi mkubwa na maendeleo duniani na inasemekana ndani ya muda mchache atachukua nafasi ya kwanza na kuizidi Marekani.
Jana nimetoka kuongea na rafiki yangu ambaye ni mkurugenzi wa moja ya mabenki hapa nchini na ameniambia kweli sasa biashara imeanza kupaa. Wiki iliyo pita nilikuwa Mwanza na Arusha na kote wafanyabiashara wa ma hoteli wanasema biashara imeanza kuja juu sana saivi
Leo Hii ninapoandika huu uzi Kuna Rafiki yangu mwingine ameniambia Kuna wawekezaji wamekuja na wana mtaji wa pesa ndefu wameanza taratibu za kufanya uwekezaji wao hapa Tanzania.
Swali langu kwenu nyie wadau leo ni Je Rais Samia Suluhu Hassan ndo Deng Xiaoping wa Tanzania???
Uzi huu nitaufufua 2030 Inshallah tukiwepo Rais Samia akiwa anamaliza Urais wake( hapa naamini Chama chake kitampitisha kugombea tena 2025-2030
Muwe na jioni njema wanabodi!!