tusaidiane uelewa kidogo, suala aliloibua mkaguzi hasa unaosemekana ni upotevu wa matrilioni ya kodi na kutamka kuwa kuna udhaifu bungeni ni janga kubwa sana la kitaifa sababu nadharia ya separation of power na checks and balance ya bongo mimi kama msomi wa Mlimani wa dhana hiyo naamini hiyo ishu imebaki vitabuni tu tangu kuanzishwa kwake kwa maslahi ya watawala na maisha yameendelea sasa huyu bwana mkubwa ameamsha popo! sasa hapa tunapoteza muda tu kujadili, sababu tukikubali izungumzwe ina maana tunahitaji kufumua nchi! hiyo ikimaanisha bunge kwanza liwe laivu kwakuwa ni kituko kukutuma ukaniwakilishe (mpiga kura) halafu eti unafanya siri yale unayoniwakilisha (mbunge) na pia bunge litahitaji kuwa na wabunge angalau wenye digrii na uelewa wa kutosha kiakili (miswada mingine ni mizito inahitaji wasomi tu ) bunge litahitaji wabunge wenye kuwajibika kwa wananchi na sio executive ( wanaosema ndiooooooo!) , bunge litahitajika kuibana serikali kisawasawa ikiwepo kupiga kura za kutokuwa na imani na waheshimiwa ikibidi , bunge likianzisha maazimio ya kukataa kupitisha bajeti za executive wasizozielewa na kuhoji na kupeleka mahakamani taarifa za upotevu wa pesa za umma unaosomeka kwenye ripoti za CAG na pia mahakama itahitaji kuwaburuza mahakamani na kuwatupa jela watendaji wote wa executive wanaofanya matumizi mabaya ya pesa za umma, wanaotumia vibaya madaraka yao na wanaovunja katiba na sheria za nchi na hasa ukwiukwaji wa haki za binadamu bila kuangalia vyeo vyao na mamlaka zao! Habari njema ni kuwa mambo hayo yatawezekana katika kipindi cha miaka 60 toka sasa baada ya genge zima la watu fulani wenye athari za utawala wa kikoloni wote kutimkia kwenye udongo!!
hili aliloibua mkaguzi ni jambo zito mno kwa maslahi ya nchi kwa wasiojua!!
ni vizuri sana Mzee akikaa pembeni sasa kwa maana pongezi kwake yeye mwenye hofu ya Mungu.