Je nimwache?

Je nimwache?

labda anakaa getto watu kibao ndio maana hataki kwani anafanya kazi gani
 
MTU kama huyu usimweke hata kwenye future plan zako,uwazi unasaidia kujua mengi hata kushauri
.
 
Hapa kuna maswali mengi sana ungejaza jaza nyama kidogo siredi yako. Je mna mda gani na uhusiano wenu? Mlikutana katika mazingira gani? Kwanini unataka ujue kwake? Je huwa mnakutana wapi? Yeye anafanya kazi gani na wewe unafanya kazi gani?
Je mnaishi dar? Na kama mnaishi dar maisha ya dar sio kumwonesha mwanamke kilahisi unapoishi maana utakuta baada ya wiki moja anahamia unajikuta umeoa kwa mda bila kupanga.

Ulishawahi kumuuliza historia ya mahusiano. Nyie wanawake mnamaana sasa. Unakuja siku moja unaacha hiki baadae hiki baada ya siku tatu begi zima la kwako limehamia kwake.

Huyo jamaa ni makini anataka akujue tabia yako kwanza ndio akufahamishe anaishi wapi.
 
Sasa ukishapajua anakoishi si ndo utajua na ndugu zake kama anaishi nao inshort huyo kuna jambo anaficha usikute ana mke
Hana mke wala nini! Its 2014, it aint the dark 90s no more! TIMES HAVE CHANGED! Ukiona mwanaume anakupelekea hotel za maana, spending significant amounts on you, anazurura na wewe in public places kama club, joints zote za jiji HUYO NDO ANAKUPENDA KWELI! Yaani anakushowoff hatari kila kona ya jiji, hapo ngangania!
Ila ukiona jamaa hakupeleki kokote, kakomalia njoo kwangu umpikie, kufua na kukzwa bureeeeeee! Jua hapo hamna la maana! Hata out hakutoi, hataki muonekane wote hilo ni KINGI aisee! Kimbia fastaaaa! UNAKOPWA mchana kweupeeeeeee! Aaaaaaaah! Acha kuwa naive unapendwa! TIMES HAVE CHANGED! THINK OUTSIDE THE BOX!
 
siwezi kumuhukumu huyo mtu wako moja kwa moja ila pia yote yanawezekana, nina rafiki yangu 5yrs ago alikuwa na mahusiano na kijana mmoja hivi, huyo kijana walifahamina muda mrefu kidogo na walikuwa marafiki kabla ya kuanza mahusiano, hata mimi nina mfahamu vzr tu baadae ndo mahusiano yao yakaanza, kwa mtazamo ni mwanaume anaeonekana very decent in short ni husband material basi rafiki yangu akajua hapa nimepata mume, hata mimi aliponiambia jamaa amemtaka wawe na mahusinao nilimsapoti kwa asilimia zote amkubali manake namfahamu ni mtu poa sana, tatizo likaanza miezi 6 baada ya mahusiano kuanza, jamaa kila siku anataka wakutanie nyumbani kwa rafiki yangu kisa anadai anaishi kwao kwahiyo hawezi kumpeleka binti.

mwaka ukaisha jamaa bado anadai anaishi kwao, baadae tukaja kupata tetesi wala haishi kwao anaishi kwake, baada ya kubanwa sana na msichana wake akakiri ni kweli anaishi kwake ila hakutaka kumwambia manake anaishi na kaka yake na hakuwa tayari kumwambia manake angetaka kwenda na yeye hakuwa tayari kumtambulisha kwa ndugu, ikapita miaka 2 jamaa excuse haziishi mwisho wa yote rafiki yangu akaja kugundua jamaa hajatulia ana wasichana kila kona, wenye kujitegemea anawafuata kwenye nyumba zao na wasio na nyumba zao makutano ni gesti. So be careful
 
Mmmmmmmmh! Hawezi
kukionesha! Huyo ni mtoto wa mjini perse!
Kuna mshikaji wanhu mmoja kuna getto tunakaaga! Watu wengi tu,
ukijisikia shule imekubana labda unakuja getto kukamua, ukijisikia mumeo
kakukeraa unakuja geto kujipumzisha, ukiwa na mchepuko wako unaaga
unakuja geto afu unachepuka! Ni sehemu iko very busy 24/7. Watu wapo in
transit! Kasoro wakusoma ndo wanakaaga specified time!

Sasa bwana kuna mdada alikuwa na tabia asipate ki bf anamleta getto!
Basi kibingwa tunampisha sebleni tunajibana chumbani! Akawa anatuuliza
mbona nyie hata siku moja hamuwaleti watu wenu hapa! Akajibiwa tu
kiutani tuwalete ili mtege mende (tumchukulie)? Thubutuuuu! Mi nikamjibu
i fancy hotels, maisha yenyewe mafupi, kama naliwa basi its a ritual
nifaidi! (Hahaaaaa! Im grown these days) bottom line is yeye tu ndo
analeta vibuzi pale!

Kilichokuja kumkuta akajua kwanini we dont fancy showing men where you
live! Unakuta mtu wameachana kila siku anakuja kuomba warudiane getto!
Basi wanagongana na mpya! Inakuwa purukushani! Inabidi tuanze kucheza
mipicha kuokoa jahazi! Yaani usumbufu mtu anaibuka tu! Mpaka akahama
pale getto! Tukamwambia huko kwako waoneshe uone kazi! Ujue watu wengine
huwaambii kirahisi rahisi its over! Wanakomaaa!

I respect a guy anaekukaribisha kwake a lot! Ni some sort of heshima! Bt
huys wengine mbwaaa mbwaaa! Nina msela wangu anafundisha chuo, basi ndo
zake, wanafunzi anagongea home! Sasa basi wasichana tulivo naive kila
anaeletwa anajua ndoa inanukia! Na hivi walimu wa vyuo wanalipwa fresh!
Weeee! Sasa mi nilikiwa nikiwa stressed out naenda pale kunywa pombe za
bure, kula, kutia hasara in return nampa pointers za kipata madem, na
mpimp mademu, napika saa ingine, hivo! Wakija wadada anawaambia huyu
dada yangu! Basi wanaliwa hatari! Mda mwengine 2 kwa siku! Nikamuuliza
kwanini unawapanga huofii scandal? Yuko SINA GHARAMA ZA KUCHEZEA KULIPIA
HOTEL ISSUE ZENYEWE NYINGI CHINI YA KIWANGO! Nikimpeleka hotel ale,
aninywee hasara sanaa! Bora hapa anafua, anasafisha, anapika namla vile
vile! Win win kwangu! Hahahahaaaaa! Watu mabandibu! Basi toka hapo
mwanaume akinialika kwake nikienda ujue nimemuheshimu hatari!

wanasemaga ukitaka wakuone expensive make yo self expensive. wadada wengine ni ujinga
 
We ni mwanaume au mwanamke kwanza tujue.
Kama ni mwanamke kwenda kwa mwanaume sawa
Ila kama ni mwanaume kwenda kwa mwanamke unatakiwa kuzingatia ustaarabu wake....Si lazima kufika kwake kwasababu zifuatazo.
Wanaume wengi ni wadanganyifu endapo ukenda kwake leo, kesho, keshokutwa halafu baadae ukamuacha mwanamke itakuwa si vyema kwa upande wa mwanamke hasa katika familia kama anaishi na wadogo zake, au ndugu zake au wazazi. Wanawake ni rahisi sana kuitwa malaya katika jamii akiwa na mwanaume zaidi ya mmoja ila mwanaume haitwi malaya.
Cha msingi ni mwanaume kujihakikishia kuwa mwanamke wake Je yuko single kweli..Labda aende kwa mwanamke once a month kwa kustukiza ila sio kila mara..





Mpenzi wangu hataki nijue anapoishi, ila kwangu ameshafika, nikimuuliza kwanini hajawahi kunionyesha anapoishi, anadai anaishi na wadogo zake kwa hiyo sio vyema wakaniona, hapa nimeona dalili la penzi la kichina.
 
We ni mwanaume au mwanamke kwanza tujue.
Kama ni mwanamke kwenda kwa mwanaume sawa
Ila kama ni mwanaume kwenda kwa mwanamke unatakiwa kuzingatia ustaarabu wake....Si lazima kufika kwake kwasababu zifuatazo.
Wanaume wengi ni wadanganyifu endapo ukenda kwake leo, kesho, keshokutwa halafu baadae ukamuacha mwanamke itakuwa si vyema kwa upande wa mwanamke hasa katika familia kama anaishi na wadogo zake, au ndugu zake au wazazi. Wanawake ni rahisi sana kuitwa malaya katika jamii akiwa na mwanaume zaidi ya mmoja ila mwanaume haitwi malaya.
Cha msingi ni mwanaume kujihakikishia kuwa mwanamke wake Je yuko single kweli..Labda aende kwa mwanamke once a month kwa kustukiza ila sio kila mara..

Mie Mwanamke,Ni vizuri kujua mpenzi wako anaishi wapi,sikuwa na maana anitambulishe kwa ndugu zake hapana,nilipenda tu kujua anakoishi basi,

Ila yeye muda wote anapenda kuja ninapokaa mpaka nikamuuliza mwenzangu kutwaa waja kwangu,mbona kwako hutaki nipajue?? ndio alipojibu kuwa anaishi na wadogoze na sio busara mimi kwenda,..
 
Mpenzi wangu hataki nijue anapoishi, ila kwangu ameshafika, nikimuuliza kwanini hajawahi kunionyesha anapoishi, anadai anaishi na wadogo zake kwa hiyo sio vyema wakaniona, hapa nimeona dalili la penzi la kichina.

sio kila demu anapelekwa nyumbani especially kama unaishi na wadogo zako tena wa kike......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom