Je, ni wakati wa Makamu wa Rais Mpango kuacha unyonge na kusimamia mikopo ya nchi?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,609
8,753
VP Mpango tuna kuhitaji kusimama na kumsaidia Raisi kwenye masuala ya mikopo ya nchi na wizara ya fedha badala ya kukaa kinyonge nyonge kila siku.

Hauja chaguliwa kwasababu ya upole pekee lakini ni kwasababu ya uwezo wako mkubwa kwenye miradi na kujua fedha sasa hata kwenye miradi na mikutano umekuwa unaikimbia au kukimbizwa kama hayakuhusu.

Watanzania tusiogope kumlaulu huyu VP.
 
VP Mpango tuna kuhitaji kusimama na kumsaidia Raisi kwenye masuala ya mikopo ya nchi na wizara ya fedha badala ya kukaa kinyonge nyonge kila siku...
Mkuu huyu ana mipaka yake ya kazi. Hawezi kujipangia kazi mwenyewe bila maelekezo kutoka kwa bosi wake ambaye ni Rais.

Sana sana anaweza kushughulikia mambo ya mazingira na kero za JMT ambazo zinahusiana na wizara ambazo zipo chini yake moja kwa moja. Kwa nafasi hii aliyokuwanayo kikatiba, ni tahadhari tu kama bendera itapepea nusu mlingoti, ili apate kuwa ndiye mrithi.
 
Ni kama alishinikizwa hivi kuwa makamu wa Rais..hicho cheo kingempendeza sana kinana then mpango angebaki kwenye uwaziri wake wa fedha.
 
ungelijua makamu waraisi ni kama kopo tu na mzigo jinsi katiba inavosema mpaka asubiri raisi kufa ndio nguvu upatikana.
badili katiba
 
VP Mpango tuna kuhitaji kusimama na kumsaidia Raisi kwenye masuala ya mikopo ya nchi na wizara ya fedha badala ya kukaa kinyonge nyonge kila siku...
Yaani huyo jamaa kwa sasa kazi yake ni uzinduzi tu wa hapa na pale, na pia kuwa mgeni rasmi kwenye makongamano mbalimbali. Inawezekana hata vyeti vyake kwa sasa amevifungia kabatini.

Kwa sasa kichwa kinachomshauri bi mkubwa kinajilikana. Na ndiyo maana haishanzai mchele kuuzwa elfu 3 kwa kilo, na hakuna hatua zozote zinazo chukuliwa. Yaani kama wananchi tunakomeshwa vile.
 
VP Mpango tuna kuhitaji kusimama na kumsaidia Raisi kwenye masuala ya mikopo ya nchi na wizara ya fedha badala ya kukaa kinyonge nyonge kila siku...
Hivyo sio huyu aliyetuingiza kwenye mikopo ya kibiashara akiwa na Jiwe huku wakidai wanajenga kwa fedha za ndani?
 
Back
Top Bottom