Je ni uoga tu au kuna la zaidi?

Don't go too far. Cheating is everywhere; iwe kwenye uchumba au kwenye ndoa. Na siyo wote wanacheat ingawa watu wanaocheat wanasemekana ni wengi. I am not among them.
Ninachomaanisha ni kuwa kuishi single siyo suluhisho la ukimwi na other heart-breaking encounters. Huwezi kuipenda ngoma inayochezwa mbali na hata sauti zake husikii. Kaingie hadi kilingeni ucheze ili uwe na upande. Mimi ninao na ndiyo maana ninaongelea uzoefu wangu. Lakini sina maana kuwa hakuna watu wanaoumia kwenye ndoa kama vile ambavyo kuna wale wanaofurahia. Halafu kwenye ndoa hakuna suala moja tu la ukimwi na DNA. Yapo mengi tu. Ukijenga wasi wasi basi wewe pressure itakaa kwenye 150/120 mmHg milele and your days will be just numbered!

Kama ni uzoefu tu hata mimi naongelea kutokana na uzoefu wangu na niliyoyaona na ninayoendelea kuyaona. Marriage is not thing and I'm not opposed to others getting married. Heck, if they want to...they should knock themselves out.

And everyone's days are numbered irregardless. And I'm curious, where in this thread did you say the foundation of marriage is trust?
 
Exactly. Ndicho ninachosema hapa wajameni......sababu hasa ndiyo italeta maana na nia ya wewe 'kumshauri' akapime.

Lakini sababu yenyewe ikiwa ni eti kwa vile ulikuwa mbali , masomoni, etc, hiyo kwangu haitoshi na inaspell kitu kimoja tu kuwa HUNIAMINI. Na kama huniamini hakuna sababu ya kujifanya kuendelea kuishi kama MUME na MKE. narudia tena UAMINIFU kwa maana ya Dark City ndo msingi wa ndoa wajameni, kama hamuaminiani kwa vile tu wanandoa siku hizi wanaongoza kwa virusi, kwa nini tuoane? tuvunje tu ndoa


Mkuu naona umemaliza kila kitu. Pia inaonekana jana umewahi home ukapata dozi ya kawaida (ya usingizi) kwani sikutegemea uwe sober namna hii.

Mtu ambaye hana imani na mwenzake aanze. Akatafute maisha mbadala. Yakianza kuwa kama yule mwanamke anayelazimishwa tigo halafu hataki kuomba talaka, huo sasa ni ujuha. Ngoja nikapumzike kwanza.
 
Ulete posa kwetu? Heheheheheheeee.....samahani mimi napenda wanawake bana. Mtafute Bwabwa kama unapenda wanaume.....juzijuzi alikuwa anatafuta mpenzi hapa.

Duh ebwaneee samahani Chalii kumbe nimeingia choo cha kike.
Ngoja nijipotezee kabisaaa
 
Kama ni uzoefu tu hata mimi naongelea kutokana na uzoefu wangu na niliyoyaona na ninayoendelea kuyaona. Marriage is not thing and I'm not opposed to others getting married. Heck, if they want to...they should knock themselves out.

And everyone's days are numbered irregardless. And I'm curious, where in this thread did you say the foundation of marriage is trust?

Sawa mkuu.

Kama hata hiyo (red) hujaiona basi naona tuishie hapo. Siyo kwamba ndo nimesema leo, nimekuwa nikisema hivyo siku zote. Hata ikitokea ndoa yangu ikayumba bado nasema hivyo hivyo.
 
Mkuu naona umemaliza kila kitu. Pia inaonekana jana umewahi home ukapata dozi ya kawaida (ya usingizi) kwani sikutegemea uwe sober namna hii.

Mtu ambaye hana imani na mwenzake aanze. Akatafute maisha mbadala. Yakianza kuwa kama yule mwanamke anayelazimishwa tigo halafu hataki kuomba talaka, huo sasa ni ujuha. Ngoja nikapumzike kwanza.

dah, mkuu, unajua vitu vingine basi inabidi kuvirudia2 huenda watu wakaelewa tunamaanisha nini,

na kweli, naona unazungumzie uzoefu wa raha za kwenye ndoa! sio mchezo manake kuwa sober na kwenyewe kwahitaji namna!lol
 
Habari ndugu

naombeni tusaidiane kuelewana kina wapwa na binamu kwa sababu - kwa wanaume rahisi kuwaambia wake zenu mkacheck vinasaba (DNA) kwa watoto wenu at the same time ni ngumu kwenu mkiombwa mkacheck afya zenu (HIV/AIDS/STDs)? hasa pale ambapo kumekuwa na umbali kidogo kati yako na mwenzi wako either due to kika au masomo? (Yaani kama kuna separation ya aina flani)

Na kina dada naambiwa nasi tu wagumu kukubali kucheck vinasaba- pamoja na ukimwi

Je mnataka tuamini ule usemi kuwa wanaume hawawezikukaa bila kumega nje?
Na je mnapomega nje huwa hamtumii kinga? Maana kama mnatumia kwa nini mnaogopa sana kucheck afya?

Nisaidieni tafadhali


Mzee,
  1. Ukimwi ungekuwa kama malaria ambayo inatiba na haunyanyapaliwi kwenye jamii, nadhani isingekuwa hofu kwa watu kupima tena sembuse hakuna gharama zozote za vipimo wala dawa za kubusti maisha.
  2. Ukimwwi hauambukizwa kwa kumegna tu, japo inaaminika kuwa ni asilimia kuwaba,
  3. Tifauti na Ukimwi, DNA, vipimo vya DNA vikigoma kutambua damu yako kwa mtoto/mimba ni dhairi kuwa mama amaemegwa nje lakini lakini vipiimo vya HIV vikisema damu chafu haimaainishi imechafuka kwa kumeaga aua kumegwa nje!
  4. Kuna athari niyingi sana za kujitambua au kutambulika kuwa ni mwathrika na ndo mana watu hawataki /hofu kupima HIV tofauti na DNA.
  5. Kumega/kumegwa nje kwa kutumia kinga haimaniishi kuwa kuwezi kupata maambukizi hata kama unatumia kwa kila tendo.
  6. Kwa akian mama kupima HIV wakati mwingine wana lazimika tu na sio hiyari yao kwa kuwa ni kanuni za Afya hususan wakati mama akiwa mjamzito ili kumlinda mtoto atakayezaliwa dhidi ya UKIMWI. Vinginevyo, hata Mchungaji au Sheikh anayehubiri kuotenda dhambi kila siku ukimweleza kupima HIV anaweza kuingia mitini.
 
hii thread ya leo imeniugusa,MJ1 kupima sio mchezo bwana, ni kotekote kwa wanaume/wanawake...nakumbuka mie wakati ule naambiwa twende mguu kwa mguu tukapime tuendelee na mambo ya uchumba nilijihic kutojielewa, co kwamba mtu hukuwa makini ulikuwa lakini cjui wac/woga hutokea wapi,.lakini ni jambo zuri kujitambua.....

ha ha haaaaaaaaaaa, kweli kabisa Nyamayao. kuna siku nakumbuka nililianzisha twende tukapime HIV ili tuzae. Nilikuwa na confidence sana, nikakuta husband naye akasupport kiurahisiiiiiiiiii. tukaenda kupima, na kesho yake husband akasafiri kikazi. Sheshe ilikuwa kwenda kuchukua majibu sasa, na nilikuwa peke yangu. Nakumbuka nilisali njia nzima mpaka nakutana na Dr bado "Nakemea" tu "Roho ya HIV ishindwe kwa Jina la Yesu"
 
ha ha haaaaaaaaaaa, kweli kabisa Nyamayao. kuna siku nakumbuka nililianzisha twende tukapime HIV ili tuzae. Nilikuwa na confidence sana, nikakuta husband naye akasupport kiurahisiiiiiiiiii. tukaenda kupima, na kesho yake husband akasafiri kikazi. Sheshe ilikuwa kwenda kuchukua majibu sasa, na nilikuwa peke yangu. Nakumbuka nilisali njia nzima mpaka nakutana na Dr bado "Nakemea" tu "Roho ya HIV ishindwe kwa Jina la Yesu"


FP,

Hiyo ilikuwa na sababu ya msingi iliyowafanya kwenda kupima VVU. Lakini bado unaona jinsi ilivyokuwa kasheshe kwenda kuchukua majibu. Binafsi sipendi na nisingeshauri mtu amshinikize mwenzake kwenda kupima bila sababu ya msingi. Kwa mfano mtu kamfumania mwenzake na kwa hiyo anampatia sharti la kupima kwanza ili waweze kurudi katika hali ya kawaida ya kusameheana na kuendelea na unyumba bila kutumia kondomu. Hilo linaeleweka lakini siyo kwa hisia tu kuwa mwenzako anatembea nje.

Kama watu wanaona ni rahisi kihivyo kumweleza mwenzake habari za kupima ukimwi, basi kwa nini hakuna anayeweza kumwambia mwenzake kwamba ametembea nje ya ndoa?
 
Suala la kupima chochote iwe ukimwi, vinasaba au kinginecho ni uamuzi wa mtu binafsi, nadhani kulazimishana si busara!
 
Tatizo kubwa hapa ninaloliona ni kukosa uaminifu ndani ya nyumba. Kwanza ni kwa mtu binafsi(mke/mme) kama si mwaminifu kwenye ndoa yako una kila sababu ya kuwa na mazoea ya kupima. Lakini kutokuwa kwako mwaminifu kusifanye ukashindwa kumuamini mwenzako.

Kama wewe ni mwaminifu na una hakika hujawahi kumega/kumegwa nje na haujafikia hatua ya kuwa na mashaka na mwenzi wako sioni sababu ya kulazimisha kupima kwani jambo hilo litaonyesha kuwa au hujiamini au humwamini mwenzako.

Mimi ninachoshauri ni kuwa ndoa zote ambazo wahusika(mke na mme) hawaaminiani ni muhimu kupima kila baada ya kipindi fulani.

Kwa wale ambao tunaaminiana na tumeamua mioyoni mwetu kuwa hata kama nitaishi zaidi ya mwaka mbali na mme/mke wangu sitamega/kumegwa na mtu mwingine na bado ninaendelea kumuamini mwenzi wangu sina sababu ya kupima HIV wala DNA. Hata hivyo najua siyo rahisi bali kwa neema ya Mungu na kwa maombi inawezekana.

Tuliooa naombeni tuwe waaminifu kwa wake zetu na kamwe wadada warembo wasitutachanganye na kutuingiza kwenye mtego wa kusaliti ndoa zetu. Na wadada/wamama naombeni msiwatie majaribuni waume za watu, mdada/mkaka ukijitunza vizuri naamini Mungu atakuandalia mwenzi aliye mwaminifu. Usipokuwa mwaminifu usitegemee Mungu atakupa aliye mwaminifu.

Mungu atuwezeshe kuwa waaminifu wakati wote na mahali popote.
 
Mimi naweza kuwa mwaminifu sawa; najihakikishiaje uaminifu wa mwenzangu; nadhani ndio tatizo lipo hapo; unasemaje FP?
 
MJ Ni ngumu kujihakikishia uaminifu wa mwenzako hata kama mkipima na mkakutwa mko salama haiamnishi kuwa mwenzako ni mwaminifu 100%. Ninachosema ni kuwa hatua ya kumuambia mkapime maana yake ni kuwa haumuamini kama kweli wewe unajiamini. Na kama yeye ni mwaminifu maana yake utakuwa umempa taarifa kuwa hujiamini na ndiyo maana umemuomba mkapime. Jaribu kufikiri hilo utakaolukuwa umelipanda moyoni mwake/hisia zake.

Sijui kama taaluma ya madakitari inaruhusu kwani ningeshauri kama ni kwa mke uongee na dakitari wake wa kliniki then anapochukua vipimo vingine apime na hiki then from there utajua kama mke yuko salama au la. Na kwa mwanamke unaweza kushauriana na mme wako kuwa mnafanya medical checkup ya familia (mme/mke na watoto) na mmuachie uhuru dakitari awe anapima kila kitu. Huenda hii itasaidia kuliko kuwa straight na kumwambia mke/mme tukapime HIV.
 
Back
Top Bottom