TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 24,891
- 11,288
naungamkono hoja... nadhani haijalishi kama watu wanakaa mbali au karibu... periodic testic ni nzuri hasa kwa watoto na couples wenyewe kwani wanweza kujipanga zaidi na hata kuepusha maabukizi zaidi (kama yapo)De Novo kutokana na takwimu kutuonyesha kuwa wanandoa wanaongoza kwa UKIMWi, huoni kama kuna umuhimu wa kubadilika kwa kuweka utaratibu maalumu wa kupima kila baada ya muda flani? Maana slogani za badili tabia naona kama zimegonga mwamba kwa maana kuwa watu wameamua kufanya kuwa ni hulka yetu kumega/gwa nje ya mahusiano yetu ya ndoa wakenya wanasema mpango wa nje!
cha maana sasa ni advocacy na uamsho wa ziada watu kukubali kupima. Now the question still lingers; hivi ni kweli kwamba wanaohitaji sensitization ni wanaume pekee?
Je kwanini tusiweke sheria kwamba kupima ni lazma?
Kuna mradi wa PITC (provider initiated testing and counselling)... hapa nadhani tungetilia mkazo kiasi kwamba hata kama unaenda kutibiwa kidonda uwe unapata test; watoto wa nursery wote wapimwe ili kujiandaa kuwalea vizuri na hata wanaotafuta medical clearance nao wapimwe... mwanzo utakua mgumu lakini baada ya 2 years tutazoea tu