IslamTZ
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 309
- 182
Jamaa yangu mmoja alioa akapata watoto watatu katika ndoa ya kwanza kisha wakatalikiana na mkewe kwa sababu zisizoweza kuzuilika.
Baada ya muda, jamaa akaoa tena. Mke mpya ana wivu balaa. Sasa imefika wakati mke anataka mume afute kumbukumbu zote za picha za familia yake ya kwanza kwenye laptop zake.
Ingawa lengo ni kumfuta yule mke wa kwanza, lakini unakuta picha nyingi ni za kifamilia ambapo kuna jamaa, mkewe huyo wa zamani na watoto. Baadhi ya picha ni za harusi yao.
Presha ya kutakiwa afute, aziharibu picha ni kubwa lakini jamaa anasita kwa sababu hizi ni kumbukumbu ya maisha yake. Jamaa ana stress balaa. Hebu tumshauri.