Maji kupungua kwenye rejeta(radiator)baada ya service

profesawaaganojipya

JF-Expert Member
Apr 21, 2015
1,485
3,133
Wakuu ni hivi, nilimwanga coolant yote kwenye rejeta, pia nikafunfungu koki kwenye injini na kumwaga yote. Halafu nikajaza upya kama lita 5 hivi, cha ajabu hata nikitembea km 10, nakuta maji yamepungua kidogo kwenye rejeta, shida nini wakuu, msaada tafadhali, gari ni noah, road tourer, engine ni 3s-SR40
 
Ngoja waje ila kama yanapungua sana may be kuna sehemu yanavuja
 
Wakuu ni hivi,nilimwanga coolant yote kwenye rejeta,pia nikafunfungu koki kwenye injini na kumwaga yote.
Alafu nikajaza upya kama lita 5 hivi,cha ajabu hata nikitembea km 10,nakuta maji yamepungua kidogo kwenye rejeta,shida nini wakuu,msaada tafadhali,gari ni noah,road tourer,engine ni,,3s-SR40
Mkuu inaelekea hiyo coolant ilikuwa haijaingia vizuri. Huwa unaongeza kiasi gani
 
Nenda Kwa mafundi Tu hakuna Namna najua wataangalia water pump na mfuniko wa radiator pengine unavujisha
Duh, mtu unapomiliki kitu chochote lazima uwe na ufahamu wa moja, mbili tatu, ikishindikana kabisa ndo unaenda kwa fundi ndio maana halisi ya Jamiiforums, wanakushauri checking points, ikishindikana ndio unamwita fundi mkuu...
 
Mkuu nimesoma ila sijaelewa vizuri. Ulipomwaga coolant ulirudishia coolant au maji?
 
Wakuu ni hivi, nilimwanga coolant yote kwenye rejeta, pia nikafunfungu koki kwenye injini na kumwaga yote. Halafu nikajaza upya kama lita 5 hivi, cha ajabu hata nikitembea km 10, nakuta maji yamepungua kidogo kwenye rejeta, shida nini wakuu, msaada tafadhali, gari ni noah, road tourer, engine ni 3s-SR40
Mkuu usijitese sana hapo shida ni ule mdomo wa rejeta utakuwa umelika au kifuniko kimesha choka gari ikitembea inachemka inasababisha mvuke /vapour kupenya kwenye uwazi, nakupotea na hiyo vepa ndo maji yenyewe yanaondoka mle ndichi.
 
Duu Mimi gari yangu aina ya ipsum kila na to ondoka asubuhi lazima iwe imepungua maji nanaongeza la robo lita hivi kuna shida wazee??
 
Wakuu ni hivi, nilimwanga coolant yote kwenye rejeta, pia nikafunfungu koki kwenye injini na kumwaga yote. Halafu nikajaza upya kama lita 5 hivi, cha ajabu hata nikitembea km 10, nakuta maji yamepungua kidogo kwenye rejeta, shida nini wakuu, msaada tafadhali, gari ni noah, road tourer, engine ni 3s-SR40
Me pia nilikutana na tatzo kama hilo ...nlifungua rejeta kuweka coolant , lkn wakat wa kufunga kumbe mfuniko ule niliufmweka vibaya ....kwahyo kagua mfuniko kwanza utakua unapitisha kias kidog yanapochemka
 
Back
Top Bottom