Je, ni sahihi kuwaeleza wazazi wako kiasi cha mshahara unachopokea?

Je, ni sahihi kuwaeleza wazazi wako kiasi cha mshahara unachopokea?

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Wakuu, nimepata kazi! 🎉

Lakini baada ya furaha yote, dada yangu ameniambia kuwa ni lazima niwaambie wazazi wetu kiasi cha mshahara wangu ninachopokea. Akaniambia, “La sivyo, itaonekana unawadharau.”

Hapo ndipo swali moja lilipoanza kuzunguka kichwani mwangu… Hofu imenijia: je, ni sahihi kuwaeleza wazazi wangu kiasi cha mshahara wangu? Je, ni sahihi kuwajulisha ni kiasi gani ninacholipwa?

Najaribu kufikiria kuhusu uwazi kwa wazazi wangu pindi ambapo nawafikishia habari hii njema. Lakini pia natambua suala la mipaka.

Vipi, unaweza kuwaambia wazazi wako mshahara wako, au uta-mute? 🤔
 
Wakuu, nimepata kazi! 🎉

Lakini baada ya furaha yote, swali moja limeanza kuzunguka kichwani mwangu… Hofu imenijia, endapo ni sahihi kuwaeleza wazazi wangu kiasi cha mshahara nachopokea? Ni sahihi kuwajulisha unalipwa kiasi gani?

Najaribu kufikiria kuhusu uwazi kwa wazazi wangu pindi ambapo nawafikishia habari hii njema. Lakini pia nitambua suala la mipaka.

Vipi, unaweza kuwaambia wazazi wako mshahara wako, au uta-mute? 🤔
Wazazi wako wanakujua in and out ,siyo mbaya kama ukiwaambia...Hata mkeo ni muhimu kujua unaingiza kiasi gani maana wanaweza kukupa ushauri jinsi ya kufanya kulingana na kipato chako.
 
Kama unalipwa milioni wambie unapokea 600k
Punguza huo mshahara kwa 40% hiyo hata mfuko wako wa kushoto usiijue

Kwa namna ulivyo furahia hiyo kazi inaonyesha kwenu bado hamjajipata na huyo dada yako anakuingiza mkenge ili waanze kukupiga vizinga

Nb: Mshahara wa mtu ni siri.
 
Wakuu, nimepata kazi! 🎉

Lakini baada ya furaha yote, dada yangu ameniambia kuwa ni lazima niwaambie wazazi wetu kiasi cha mshahara wangu ninachopokea. Akaniambia, “La sivyo, itaonekana unawadharau.”

Hapo ndipo swali moja lilipoanza kuzunguka kichwani mwangu… Hofu imenijia: je, ni sahihi kuwaeleza wazazi wangu kiasi cha mshahara wangu? Je, ni sahihi kuwajulisha ni kiasi gani ninacholipwa?

Najaribu kufikiria kuhusu uwazi kwa wazazi wangu pindi ambapo nawafikishia habari hii njema. Lakini pia natambua suala la mipaka.

Vipi, unaweza kuwaambia wazazi wako mshahara wako, au uta-mute? 🤔
Mute
 
Dada yako hana akili usimsikilize, anawaza ki kike kike, kama wewe ni mwanaume hupaswi kumshirikisha mtu mshahara wako, jiulize wewe baba yako alishawahi kukuambia analipwa ama anaingiza pesa ngapi kwa mwezi??!!
 
Mshahara ni taarifa nyeti ya mtu binafsi, hata wafanyakazi wenzako hawatakiwi kujua unalipwa kiasi gani. Ukiruhusu wafanyakazi wenzako wakuchukulie salary slip watajua mshahara wako ni scale gani. Hakunaga mfanyakazi anayetajataja kiasi cha mshahara wake kwa watu hovyohovyo, hizo ni taarifa za faragha
 
Kwenye mishahara ya hovyohovyo bosi anatoa hela mfukoni kwake anakulipa popote mkikutana, huo mshahara unaweza kumuambia mtu maana si mshahara wa maana na wenye heshima ni kama posho ya kibarua tu. Ila ule wa kwenda ATM huo si wa kumuambia mtu ni siri yako
 
Inategemea una wazazi wa aina gani na wewe mwenyewe una umri gani ila ingekuwa kwa upande wangu ningekuwa na maswaali meengi ya kuwauliza ili nijue lengo lao la kuhitaji kujua huo mshahara.
 
Back
Top Bottom