BADILI TABIA nina waasiwasi na kauli yako, inamaana mimi Mtambuzi nikipata Ukuu wa Wilaya utakuwa na roho nyeupeeee kabisa.......................
Tatizo hapa "kijicho" ni nini exactly? wivu wa maendeleo? wivu usio na maendeleo? Kajicho kadogo? maana Kijicho could mean a small small eye
BADILI TABIA mimi ni mmoja wa wakuu wa wilaya wapya walioteuliwa na mkuu wa kaya hivi karibuni nikiwazkilisha wilaya mpya ya Kideleko ................Nipongeze basi..................LOLsana tena nitakuombea ufanikiwe zaidi
Msaada tafadhali ni ipi hiyo BADILI TABIA
mmmmmmh huijui maana nyingine? Kweli? Loh
Kweli tena BADILI TABIA.....msaada tafadhali,,,,hata PM tu
hihihigihiiii nitakunong'oneza....
Ha ha haaaaaUkitaka kujua kuwa wewe ni mwenye kijicho dhidi ya mafanikio au jitihada za wenzio, jiulize maswali machache yafuatayo:
Je unaposikia jirani kanunua gari, kajenga nyumba, kafungua biashara kubwa au mwanae kapata nafasi ya kusoma nje ya nchi na mengine mengi kama hayo maadamu yawe mafanikio, unajisikiaje moyoni?
Au jirani yako anapokuomba ushauri wa kuanzisha biashara, kununua shamba, gari au nyumba, unampa ushauri kwa moyo mweupe au unatoa ushauri usiofaa?
Kwa vyovyote vile, majibu ya maswali hayo hapo juu yanatosha kukujulisha iwapo una kijicho dhidi ya mafanikio ya mwenzio au la.
Hebu tusiwe wanafiki, tujifanyie tathmini ili tujijue tuko upande gani
Nani athubutu?
Mtambuzi, uzi wako siyo watu wanakwepa ila mada uliyoiweka imekuwa na changamoto kwenye kuichangia. Kwa upande wangu mimi suala la kuwa na kijicho au kutokuwa na kijicho inategemea na ukaribu wa huyo mtu ambaye anamuonea kijicho/asiyemuonea kijicho mwenzie.
Kwa mfano si rahisi, mtu akigombana na mwenzake, kwa vyovyote vile, hatapenda kuona mwenzake (huyo mgomvi wake) anafanikiwa kwa yale atakayokuwa anayafanya. Hii ni nature ya binadamu na ndiyo maana kuna msemo unasema adui yako muombee njaa, na huwa hawasemi muombee mafanikio!!!
Lakini ktk hali ya kawaida, huwezi kuwa na kijicho kwa yule mtu ambaye una mahusiano naye mazuri. Kwa mfano rafiki zako, ndugu zako, jamaa zako wa karibu nk nk huwezi kuwaonea kijicho wanapofanikiwa na kama ikitokeo hivyo, basi wewe utakuwa na matatizo au una ile kitu inayoitwa ROHO MBAYA! :confused2:
Yaani umesema sahihi kabisa..........
Lakini kuna namna nzuri ya kuondokana na hiyo dhana ya "adui yako muombee njaa"
Ninaandaa makala juu namna ya kuondokana na kijicho chenye kisirani............................!