Kupanga ni kuchagua, kuchagua ni kupanga

JOVITUS KAMUGISHA

New Member
Mar 13, 2013
4
5
Siku kadhaa zilizopita nilikuwa naongea na mmoja wa marafiki zangu wa karibu nilimuuliza swali hili, “Je ni upi msemo sahihi kati ya kupanga ni kuchagua au kuchagua ni kupanga.” Mara zote nimekuwa nikichanganya katika kutanabaisha usemi upi sahihi. Na akanijibu- yote ni sahihi kwa maana inategemeana.

Na baada ya kuuliza ndipo akili yangu ikawaza vitu vingi juu ya uhalisia wa maisha na jinsi tunavyoishi na mipango tunayoweka juu ya maisha yetu. Uhalisia juu ya maisha ya mtu na kila unapomuuliza juu ya hali yake anasema “Maisha yamebana sana.” Ni ukweli usiopingika kuwa maisha ndivyo yalivyo na inabidi tuyakubali jinsi yalivyo.

Ila swali kubwa ambalo hatujawahi kujiuliza ni kuwa; "Je, si kana kwamba sisi ndio tunaongezea ugumu wa maisha kwa kushindwa kupanga na kufanya uchaguzi sahihi?"

Kuchagua ni Kupanga na tunapochagua namna ya maisha tunayoyataka ndivyo na yenyewe yanatupangia huko mbele. Makosa makubwa tunayoyafanya ni kutokuwa na mpango juu ya maisha yetu. Na hii si kwa kizazi kinachokua tu, pia ni kwa kizazi ambacho kinatulea na tunachokilea sasa.

Hapo zamani kulikuwa kuna elimu ya kujitegemea; ila sijui ni zimwi gani lilikuja kutuchukua na kujikuta tunaondoa Elimu hii. Je, ni nani alaumiwe? Leo tunalalamika kuhusu mambo mengi kama vile ukosefu wa ajira, kuongezeka kwa wimbi la watoto wa mitaani, ndoa zinazovunjika, rushwa na mambo mengine kama hayo tukisahau kuwa tulikosea kwenye kupanga na hivyo kupelekea Kuchagua mtindo wa maisha uliopo sasa.

Katika maisha ya kawaida; ukianza kuiangalia jamii tuliyonayo; inaishi kwa ule msemo wa kizungu wa 'hand-to-mouth life’. Kwa jamii nyingi za Kiafrika; kijana anapomaliza elimu yake ya juu au elimu ya aina yoyote ile anakuwa bado hajajiwekea malengo (hii si kwa wote, bali ni kwa asilimia kubwa) hivyo badala ya kuzalisha mali anatumia kile kidogo ambacho alichonacho. Kwa namna hii hatuwezi kutegemea kuwa atakumbuka kupanga mapema. Utakuta vijana wengi tukiwa na kapesa kidogo kwa akaunti- tutachukua mkopo wa gari ili tupaki kwenye uwanja wa mwenye nyumba tuliyopanga; baadae kidogo utakuta tunapochoka kujipikia wenyewe au kula kwa mama lishe, tutamtafuta shemeji (au wifi) ili apike na kupika. Na ndani ya muda mfupi unakuta harusi hiyo na jamii yetu tukishachangishana milioni kumi za harusi- tunafanya kasherehe ka harusi yetu.

Huo ndio uhalisia wa maisha ya wengi. Na sasa ukioa au kuolewa- haichukui raundi; utaanza kuitwa baba au mama fulani. Na baada ya hapo tunaanza kulia kuwa maisha ni magumu tunasahau kuwa kuwa "KILA MTOTO ANAKUJA NA SAHANI YAKE." Na kitu kingine tunajikuta tunaoana mizigo kwa mizigo (mme mzigo, mke mzigo)!

Kitu ambacho inabidi tutambue ni kuwa kujiendeleza ni kitu muhimu sana; kufanya maamuzi juu ya jambo fulani ni jambo la kipekee kwani ndilo huifanikisha kesho ya mwanadamu yeyote. Kupanga juu ya nini unataka utimize katika maisha yako ni muhimu sana kwa sababu hutengeneza kila uwezekano wa kufurahia maisha yako.

Mipango ya kufanya biashara, masomo, kuwa na familia bora ni machache kati ya mengi ambayo kila mwanadamu anayatamani. Na wengi huwa tunaweza kutimiza mambo hayo kwa kiasi chake lakini tunakosea katika sehemu na sehemu. Mfano halisi ni mama zetu, dada zetu (nasema hivi kwa sababu hutokea mara nyingi) pale wanapoomba mikopo kwa ajili ya kufanyia biashara. Kuna mambo mengi wanayakosea- na hili lipo wazi.

  1. Cha kwanza wengi huingia kwenye vikundi vya mikopo kwa kufuata hulka kutoka kwa wengine bila kujua wakipata mikopo hiyo wanaifanyia nini. Kutokana na mwendo huu wengi wanajikuta wamechukua mikopo na kuanza kuitumia nje ya malengo ya mkopo kwa maana hawana mpango mkakati wa kuendesha biashara zao. Mipango ni muhimu na wanachotakiwa ni kuwa na mipango ya muda mfupi na muda mrefu.
  2. Jambo la pili ni kufanya biashara zinazofanana.Ujasiriamali si jambo baya- na wote walioleta elimu ya ujasiriamali hawakukosea ila kosa linafanywa na wajasiriamali. Labda niulize swali dogo ambalo ni halisi, "Je umeshawahi kufika stendi ya Makumbusho jijini Dar es Salaam ?" Nina imani jibu ni ndiyo- kitu ambacho nimeshuhudia ni mfanano katika biashara. Kila ukipita jioni kila mtu ana biashara moja ya kutengeneza bisi. Ukihesabu haraka haraka utakuta vijana kumi na biashara hiyo. Na hilo si Makumbusho tu pale- bali sehemu nyingi ambazo unakutana na wajasiriamali wadogo wakiwa wamejirundika sehemu moja wakiwa na biashara zinazofanana. Hapo ndipo utakuta wengine wanaanza kukamatana uchawi kwa sababu inawezekana kati ya hao watu kumi ni mmoja tu ndo anafanya biashara. Hii yote ni kutokana na mipango mibovu na badala ya kutengeneza faida, wafanyabiashara wanatengeneza hasara. Naamini sio kila ujasiriamali ni kuanzisha cha kwako. Unaweza kuanzisha biashara sawa sawa na ya mwenzako, ila hakikisha kuwa katika biashara yako kuna kitu cha ziada cha kumvutia mteja anayekuja kwako (jambo hili limesemwa sana kwenye semina za ujasiriamali). Tengeneza kitu tofauti ambacho kitakutoa sehemu moja. Hivyo kwa wale tunaowaita wajasiriamali na wana-mikopo; kuwa na mpango thabiti.
  3. Jambo la tatu ni kukata tamaa mapema. Ukweli uko wazi kuwa wengi waliojipanga wakafanikiwa walianza chini na kwa hasara au kwa hali ngumu. Ni kweli wajasiriamali wengi wanapanga na kuchagua mambo mazuri lakini wanakosa uvumilivu katika kile wanachokifanya. Hawana simile na kusubiri wakati wao kufika.

Unapotaka kufanya kitu kuwa na mpango mzuri katika biashara na kufikiria zaidi ya biashara ambayo kila mmoja hufanya ndiyo huleta faida na kuthibitisha uchaguzi mzuri.
Nakubaliana na Masoud Kipanya aliposema; "SI KILA MMOJA NI MJASIRIAMALI- WENGINE NI WAAJIRIWA." Hivyo usilazimishe kwa kuchagua kitu ambacho si chako.

Je tufanyeje? Hapa chini naelezea machache ambayo tunaweza kudadavua ili kupata njia sahihi ya mipango na chaguzi zetu
  1. Kupanga ni hatua ya kwanza muhimu sana katika kuelekea kwenye mafanikio. Ni kama ramani inayotuongoza katika safari yetu ya maisha. Kupanga kunahusisha kutambua malengo yetu, kutafakari kuhusu njia za kufikia malengo hayo, na hatimaye, kutengeneza mpango wa vitendo. Kupanga huku kunatupa udhibiti na mwongozo wa kile tunachotaka kufanikisha.
  2. Kwa upande mwingine, kuchagua ni utekelezaji wa mipango hiyo. Ni hatua ya kufanya maamuzi yanayolingana na malengo tuliyoweka. Kuchagua kunahusisha kutenga rasilimali zetu, iwe ni muda, fedha, au jitihada, kwa njia ambayo inatupeleka karibu zaidi na malengo yetu. Hivyo basi, kuchagua ni kutekeleza mpango uliowekwa na hivyo kufanya mipango yetu iwe na tija.
  3. Umuhimu wa kupanga ni kama msingi imara ambao unatuwezesha kufanya maamuzi sahihi. Kupanga kunatuwezesha kutambua vipaumbele vyetu na kutenga rasilimali zetu kwa njia inayofaa. Hii inatuwezesha kuepuka kufanya maamuzi ya haraka haraka au kwa hisia za papo kwa papo, ambayo mara nyingi huishia kuwa na matokeo mabaya.
  4. Kwa kuongezea, kupanga kunatuwezesha kuwa na dira na mwelekeo katika maisha yetu. Tunapokuwa na malengo na mipango thabiti, tunajikuta tukifanya maamuzi yenye mantiki na kuepuka kuteleza katika mtego wa hali ya kutokuwa na uhakika.
  5. Kwa upande mwingine, umuhimu wa kuchagua unatuonyesha umuhimu wa kutekeleza mipango tuliyoweka. Kuchagua kunahusisha uamuzi wa vitendo ambavyo vitatupeleka karibu na malengo yetu. Ni kupitia kuchagua ndipo tunapokuwa watendaji, na hatimaye kufikia mafanikio.

Hitimisho:
Kwa hiyo, kupanga ni kama kujenga msingi thabiti wa nyumba yetu ya mafanikio, wakati kuchagua ni kama kuijenga nyumba hiyo kwa kutumia msingi huo. Bila kupanga, kuchagua kunaweza kuwa kama kupoteza njia katika jangwa bila ramani. Na bila kuchagua, kupanga kunaweza kuwa kama kuweka mipango katika rafu bila kuitekeleza.

Hivyo basi, kujua umuhimu wa kupanga ni kama kujua jinsi ya kuunda njia ya mafanikio katika maisha yetu. Ni kujua kwamba hatua zetu za leo zinaathiri sana jinsi tunavyoishi kesho yetu. Na kwa kuelewa umuhimu wa kuchagua, tunajikuta tukiongeza nguvu na uthabiti katika safari yetu ya kufikia malengo yetu.

Kwa hiyo, tunapojikuta tukijikwaa katika safari yetu ya maisha, ni vyema kurudi kwenye msingi wa kupanga na kuelewa kwamba kila uamuzi tunaochukua leo unaathiri sana kesho yetu. Kupanga ni kuchagua, na kuchagua ni kupanga. Na katika kuunganisha hatua hizi mbili, tunaweza kujenga maisha yenye mafanikio na furaha.
 
Maisha yako ya Sasa ndio matokeo ya Maisha yako yajayo
 
Umekosea kudogo mtililiko wako wa uzi ...
KUPANGA NI KUCHAGUA NA KUCHAGUA NI KUBAGUA HAKUNA KUCHAGUA PASIPO KUBAGUA
 
Back
Top Bottom