Je, ni kweli ukimruka mtoto anakuwa mfupi?

Swali la siku PLAT2.jpg

Jamii zetu zimekuwa zikiamini nadharia mbalimbali, moja ya nadharia hizo ni kama hii ya kwamba UKIMRUKA MTORO ANAKUWA MFUPI.

Je, mdau wetu una maoni gani kuhusu nadharia hii?

Shiriki nasi kwenye kufanya uhakiki wa Nadharia hii iliyopo kwenye Jamii zetu.

Tuandikie unachokiamini pamoja na sababu za kwanini unaamini hivyo.
 
Labda kama sijaelewa swali but kwanini umruke mtoto?

Unamruka unaenda wapi ina maana alipokaa ni njia nyembamba sana kiasi huwezi kumnyanyua pembeni ukapita kisha ukamrudisha alipokuwa amekaa?
 
Hii nadharia ipo sana na watu wanaiamini mno, japo kwa upande wangu siamni na nlhaina ujusiano wowote kati ya urefu wa mtu na kurukwa kwake.

Nakumbuka Wakati wa utoto nilokuwa nacheza kwa jirani mama akaniita, Nikiwa nakimbia kuitikia wito nikamruka mtoto wa jirani yetu aliyekuwa kakaa njiani halafu nikakimbia nyumbani.

Yule mama wa jirani alikuja kunifata kwa jazba nirudi nikamruke tena kwa kurudi upande niliotikea ili kumuepusha kuwa mfupi, kwa kuwa nilikuwa mtoto nilitii nokamruka tena.

Natamani kumuona kama ni mrefu au mfupi kwa sasa sema sijui anaishi wapi.
 
Labda kama sijaelewa swali but kwanini umruke mtoto?

Unamruka unaenda wapi ina maana alipokaa ni njia nyembamba sana kiasi huwezi kumnyanyua pembeni ukapita kisha ukamrudisha alipokuwa amekaa?
Hayo umewaza ukiwa tayari umekuwa, lakini watoto ni sehemu ya mchezo wanafanya.

Mmoja anaweza kuwa kakaa chini mwenzake akaruka juu
 
Hizo zilikuwa tu mbinu za wazee. Waliona ukiacha watoto warukane wanaweza kuumizana au hata wewe ukimruka mtoto unaweza kumkanyaga bahati mbaya. Wakaamua waje na hiyo mbinu.
 
Hii nadhari imekuwepo kwenye jamii Kwa muda mrefu hasa Kwa sisi tuliozaliwa miaka ya zamani.

Ilikuwa inatumika Kwa lengo la kuondoa hatari iliyopo ya kumruka mtoto na bahati mbaya ukamkanyaka.

Kujibu swali lako, hakuna uhusiano wa kumruka mtoto na kutokuwa kwake mrefu.

Sayansi inaonesha Mtoto hurithi Maumbile ya Urefu/Ufupi kutoka Kwa Wazazi wake na sio kwasababu ya kurukwa.

Mtu Mume (Mrefu) akizaa na Mtu Mke (Mrefu) Wana asilimia 100 kuzaa mtoto mrefu.

Mtu Mume mfupi akizaa na Mtu Mke Mrefu Wana asilimia 75 ya kuzaa watoto warefu

Mtu Mke mfupi akizaa na Mtu Mume (mfupi) Wana asilimia 100 kuzaa watoto wafupi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom