SoC03 Malezi ya Mtoto hutoa mwelekeo katika maisha yake

Stories of Change - 2023 Competition

Thomson001

New Member
Jul 23, 2023
1
1
Mtoto ni hazina ya taifa.
Malezi ya mtoto huanza pale anapozaliwa na kuanza kujenga uhusiano baina ya mtoto na mzazi au mlezi wake.
Naposema malezi bora aidha kutoka kwa mzazi wake au mlezi hupelekea mwelekeo au dira ya mtoto kama wahenga walivyosema "mtoto umleavyo ndivyo akuavyo" hapa tunaongelea jinsi malezi yanaweza kuchagiza kwa namna fulani katika maendeleo yake ukubwani ikiwa pamoja na kiakili, kijamii, kibayolojia, kisaikolojia na kiafya.
Hii inasaidia kwenye kumjengea mtoto uwezo wa kujiamini, kujielezea mbele ya umati, kushirikiana na wenzake katika kazi za kijamii, kuweza kuelezea mambo yanayomsibu ama anayokumbana nayo kwenye maisha yake.
Mara nyingi baadhi ya wazazi au walezi wanaopewa mtoto ili wamlee wamekuwa wanatengeneza uhusiano usio sahihi baina yake na mtoto mfano kumfokea bila sababu ya msingi, kumtukana na pengine kumpa vitisho vikali.
Hii inamjengea saikolojia ya uwoga, hofu na wasiwasi pale anapotaka kumueleza mzazi au mlezi wake mambo yanayomsibu.

Kwanini baadhi ya watoto wanajiamini na wana ujasiri mkubwa kuliko wengine?
Katika kufuatilia kwa nini baadhi ya watu wanakosa ujasiri wa kuongea mbele ya umati na kwa nini wengine wanaweza bila shida yoyote, utagundua historia yake ya nyuma utotoni jinsi alivyolelelewa yaani kajengewa mazingira ya hofu au woga. Hii inapelekea ugumu wa kubadilika anapokuwa mkubwa maana saikolojia yake imeharibika anahisi yeye ni wa kuwa hivo tu!.
Vitendo vingi vya unyanyasaji anavyopata mtoto wakati wa ukuaji kuna uwezekano mkubwa wa kubaki kwenye kumbukumbu zake hivyo anapokumbuka anakuwa na majonzi na muda mwingine kupelekea kufanya maamuzi ya magumu kama vile kufanya uhalifu, kukata tamaa ya maisha au kukatisha uhai wake.
Watoto wananyimwa nafasi ya kusikilizwa na kutoa maoni katika kile wanachokiamini. Hii inapelekea mtoto kuhisi yeye si kitu chochote katika jamii kwahiyo wanapokua ile dhana iliyojengeka inabaki kwenye fikra zao.

Je, nini kifanyike?
Mzazi anatakiwa kuhakikisha anatengeneza uhusiano mzuri na mtoto hili kumtengenezea ujasiri wa kujiamini, kumshirikisha mtoto kwenye mambo madogomadogo ya kifamilia, hii itasaidia kumjengea ujuzi na ukomavu wa kiakili anapokua.
Walezi wa watoto wanaopewa jukumu aidha na wazazi wa hao watoto au jamii pale wazazi wanapokuwa wamefariki, wakumbuke kujali utu na umri wa mtoto kwenye malezi!. Maranyingi walezi wanajisahau kutoa malezi bora hivyokuharibu saikolojia ya mtoto inayopelekea chuki, kisasi na kukata tamaa kwa hawa watoto wanapokuwa wakubwa.
Serikali kuunga mkono kwenye mapambano dhidi ya uwajibikaji katika kuhakikisha mtoto anakuwa na mahitaji pamoja na malezi bora kutoka kwa wazazi au walezi ikiwemo kutoa adhabu kali kwa wanaokiuka haki za watoto ili kujenga taifa lenye nguvu na kujiamini.
Kuunda taasisi zenye kusimamia na kuhakikisha uwajibikaji katika misingi ya ukuaji wa watoto inatekelezwa katika jamii.
Taasisi za dini kuhamasisha waumini wao katika kujali, mapendo na mahusiano bora katika jamii kulingana na vitabu vya kidini vinavyoelekeza ili kuwa na hofu ya Mungu. Viongozi wa dini wahubiri maadili na upendo katika jamii.
Kujenga ukaribu na mtoto ili endapo atafanyiwa ukatili au unyasasaji wa aina yoyote iwe rahisi kwa mtoto kufikisha taarifa kwa mzazi au mlezi wake.
Jamii ipewe elimu juu ya swala la malezi ya watoto kwa sababu zoezi la malezi ya watoto ni jukumu la jamii nzima. Watoto wafundishwe maadili mema ya kuishi na kucheza na wenzao.

Watoto ni taifa la kesho, hivyo ni jukumu letu sote kama jamii kujenga taifa bora!!!.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom