Je, ni kweli nyumba mnazoziita contemporary (Hidden roof ) zinapunguza gharama ya kupaua?

Nani alikwambia ni gharama nafuu? Kwanza hizo nyumba huwa na madoido mengi na zinatumia Sana saruji so gharama huwa ni zaidi ya zile traditional houses.
Si kweli.....paa was so over priced......bati kila mtu alitaka Nabaki Africa,then nenda uguse uone moto wake...to avoid all those,watu wanamaliza na box.....

Paa was so ridiculously over priced
 
Screenshot_20221019-141112.png
 
Ni ujenzi wa kizembe tu ndio inapelekea hizi nyumba kuonekana changamoto ila ni ujenzi mzuri plus zina muonekano wa kisasa sana na hata finishing yake huwa inakuwa tamu sana.
Moja ya nyumba zenye art matata Sana,ila Kamwe usije kujenga kwa vishoka au ukajatibu kubadili ramani ya kawaida iwe contemporary lazima utapuyanga na matokeo yake unaanza kulaumu eti zinavuja.
 
Naiandaa Uzi kuhusu contemporary I hope utasaidia kuwapa wadau wanaozipenda hints chache kabla ya kuamua kuzijenga
 
Hidden roof houses ni Kama hizi hapa

View attachment 2387836View attachment 2387839View attachment 2387840

View attachment 2387836View attachment 2387839View attachment 2387840

Ni kweli kabisa hidden roofing hupunguza gharama ya mbao kwa zaidi ya 80% na hupunguza pia gharama ya bati kwa zaidi ya 70%.
Endapo idadi ya mbao inapopungua basi pia gharama za misumari bati na misumari mbao hupungua kwa asilimia zile zile pia.

Kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa Cha mbao na bati gharama ya fundi mpauaji nayo itapungua.

NAMNA YA KUJENGA NYUMBA ZA AINA HII

1. Hidden roof maandalizi yake yanaanzia tangu pale msingi unapojengwa.
  • zitaandaliwa mapema kabisa njia za kupitisha pipe za maji
  • Mchoro lazima uoneshe mapokeo ya maji Toka kwenye bati (gata)
  • Hidden roof jengo lake linakuwa na vikolombwezo vingi, ambavyo vinahitaji umakini mkubwa kuvijenga.
2. Gata. HII ni mifereji ya kupitisha maji inayojengwa dalini. NA HAPA NDIO PANAHITAJI UMAKINI MKUBWA SANA. ukikosea hapa utaichukia nyumba Yako mile.
Ili nyumba hii isivuje lazima paa zake ziwe ndogo ngogo, na ili paa ziwe ndogo dogo ni lazima mizunguko ya gata iwe ya kutosha. Kuweka mizunguko ya kutosha ya gata ni gharama na inahitaji maarifa makubwa.

CHANGAMOTO
1. Gharama ya kujenga boma huongezeka tofauti na nyumba ya kawaida.
Sababu ya kuongezeka gharama ya ujenzi ni kutokana na ujenzi wa gata, boma kuwa refu kwenda juu na nk.
- Materials huongezeka mf. Tofali,mondo,cement nk.
-Labour charge huongezeka kwasababu ya complexity ya ujenzi wake. (HAPAHITAJI FUNDI NJAA HAPA)

2. Fundi lazima awe mbobezi. ZINGATIA HILI

3. Kuvuja. KAMA UTADHARAU KIMOJAWAPO NILICHOKUELEZA HAPO JUU. basi jua kuwa lazima nyumba Yako ivuje.

KARIBUNI SANA
0655173113
Fundi mahiri wa ujenzi
Email: pmoses@gmail.com
Ahsante.

Pamoja na yote hayo, bado nyumba itavuja, ingawa itategemea na umakini uliousema. Na sehemu ambazo ni critical ni kwenye muunganiko wa kuta na bati. Sababu kubwa ni weather effects. Kwamba kule juu, juwa huwa ni kali na kisha kuna vumbi na umande. Muunganiko wa mambo hayo huleta reactions ambazo husabisha tofali au Cement mortar au bati kuoza baada ya muda angalau kuanzia miaka miwili au mitatu. Kwa hiyo kama hautazingatia mambo hayo ujue kweli utaichukia nyumba yako, kwani ule unyevu kwenye ukuta( siyo lazima ivuje kwanza) ila leakage hupausha rangi, huozesha ukuta kwa ndani na kuweka mabaka au doa kubwa kwenye dari( ceiling)
 
Kinachofanya gharama ya kupaua ni bati kukatwa (kuchinjwa) na kenchi kuwa na kona kibao. Ni kweli huo ni ujenzi rahisi
 
Back
Top Bottom