Gaspar Meing'ati
[28/08 7:48 AM] Gaspar Meing'ati: SIZOFRENIA(Schizophrenia)
1.Ukubwa wa tatizo
Sizofrenia ni ugonjwa mkubwa wa akiliunaothiri karibu mtu mmoja kwa kila watu mia moja. Kote duniani vitanda vingi vya hospitali za magonjwa ya akili vimejazwa na wagonjwa wa zisofrenia kuliko ugonjwa mwingine wowote. Ugonjwa huu una athari za kudumu kwa mgonjwa kwa karibu kila sehemu ya maisha ya mgonjwa, na hugusa na kuathiri pia maisha ya familia ya mgonjwa hasa kwa wale wanaohusika na huduma ya mgonjwa huyu.
2. SIZOFRENIA NI NINI?
(a)Dalili chanya
Ugonjwa wa sizofrenia hutambulika wakati mtu anapohisi dalili fulani za msingi;hizi ni pamoja na aina maalum za mawazo njozi(Hallucinations), imani potofu(delusions) na kuvurugikiwa mawazi
Mawazo njozi(hallucanations) ni mapokeo batili ya mawazo. Muathirika husikia vitu huona vitu, ambavyo watu wengine hawasikii,hawavioni au harufu ambayo wengine hawainusi. Kusikia sauti zinazozungumza na muathirika kwa sautia ya ukali ni dalili ya kawaida kwa mgonjwa wa sizofrenia. Imani potofu(dellusions) ni dalili ya sizofrenia ambayo hujionesha kwa kuwa na imani kali potofu,kwa kawaida ni kuhusu kitu cha ajabu ajabu, na ambayo hung'ang'aniwa sana na muathirika kiasi kwamba hata ukijaribu kuikosoa si rahisi kuisha. Imani hii potofu ni ya kipekee kwa mgonjwa, kwa mantiki kwamba ni yeye peke yake katika jamii anaeamini hivyo. Imani potofu hutofautiana lakini mara nyingi hujumuisha:- Imani kwamba msukumo fulani kutoka nje unachukua usukani wa kuendesha mawazo au mwili wa mgonjwa. Imani kwamba kundi fulani la watu au kikundi fulani kimeamua kumdhuru au kumuangamiza mgonjwa bila sababu yeyote ya msingi. Imani kwamba vitu asomavyo au aonavyo vina maana ya kipekee au vinaweza kuwa na uwezo wa kipekee, na hasa uwezo wa kusoma mawazo au hisia za mtu mwingine,nguvu fulani za miali au vitu fulani kutoka nje ya dunia yetu.
Mvurugiko wa mawazo unahusu hali ya kutokuwa na mpangilio wa mawazo ambayo yanaweza kusbabisha lugha mpya au yenye mtiririko wa ajabu. Aina hii ya dalili huitwa DALILI CHANYA, na zinaweza kumsumbua na kuwa za kutisha kwa yule zinayemsumbua. Mara nyingizinaweza zikaambatana na wasiwasi wa hali ya juu sana pamoja na tabia za ajabu ajabu na hasa kama ni ugonjwa wa nguvu au zinakuja ghafla san.
DALILI HASI.
Tofauti na dalili chanya, ambazo huja kwa ukali na kuleta mabadiliko ya wazi katika tabia na mwenendo wa muathirika. Hizi huitwa hasi kwa sababu husababisha kupungua au kukosekana kwa tabia au mwenendo wa muathirika. Hii ni pamoja na upungufu wa motisha binafsi,upungufu wa utendaji kazi, kupungua katika maongezi na kusema, kujitenga na jamii,dalili wazi za kupungua au kutokuwa au kutokuwa na hisia, upungufu wa mawazo na matatizo ya kuishi na watu vizuri.
Dalili hasi zinaweza kutofautiana katika ukali wake,kati yakuwa kidogo tu hadi kuwa kali kiasi cha kuathiri utendaji kazi na kujihudumia mwenyewe binafsi.
MWENENDO WA MGONJWA:
Ugonjwa wa sizofrenia kwa kawaida humpata mtu wakati wa miaka ya mwisho wa ujana au mwanzoni mwa utu uzima (miaka 15-25). Menendo wa ugonjwa unaweza kutofautiana kati ya mgonjwa na mgonjwa. Ingawa baadhi ya watu wanaweza kupona baada ya shambulio la kwanza,ugonjwa huu mara nyingi hurudia rudia kwa vipindi. Watuwengine hupatwa na mlipuko huu mara kwa mara na dalili hudumu na kulemaza kwa maisha yao yote.
ASILI YA UGONJWA:
Asili au chanzo cha ugonjwa wa sizofrenia bado mpaka sasa ni kitendawili. Inadhaniwa kwamba labda ni katika asili ya maumbile (genetic) na kwamba kuna mvurugiko katika kemikali za ubongo zinazohusika na usambazaji wa taarifa. Pia kuna ushahidi wa dhati kwamba matatizo ya hisia na ya kijamii yanachangia katika mlipuko wa ugonjwa huu.
[28/08 8:44 AM] Gaspar Meing'ati: HUDUMA NA MATIBABU.
Kwa wakati huu hakuna tiba ya kuponya kabisa ugonjwa huu. Madawa makali na yenye nguvu hutumika kuwapoza na kuwatuliza wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa huu. Madawa haya hutumika kwa sababu mbili:- Kupunguza dalili chanya za mgonjwa wakati wa mlipuko au kuzuia mlipuko wakati mgonjwa ametulizana(wakati ana nafuu). Kwa sababu dawa hizi husaidia kuzuia mlipuko mwingine,mara nyingi wagonjwa wa sizofrenia hutumia dawa hizi kwa muda mrefu sana, na ili kuwa na uhakika na utumiaji wa dawa hizi,mara nyingi hutolewa kwa njia ya sindano. Dawa zinaweza kusababisha dalili zisotarajiwa na kwa hio pia zikahitaji matibabu mengine kuzipoza. Dawa mpya zimeaanza kupatikana ambazo athari zake ni ndogo sana na ambazo husaidia kupunguza dalili hasi za mgonjwa.
Mlipuko mkali wa sizofrenia mara nyingi husababisha mgonjwa kulazwa hospitalini kwa matibabu.Wakati ugonjwa umesababisha athari nyingi za kiutendaji au ki-uhusiano kwa mgonjwa, muda mrefu wa marekebisho ya mwenendo wa mgonjwa utahitajika; na ni muhimu kama ilivyo kwa matibabu ya kimwili. Hii inahusisha ngazi mbalimbali za usaidizi kutoka kwa jamii, kama vile kupata mahali pazuri pa kuishi au hata huduma za hospitali za kutwa.Mbinu mbalimbali zimebuniwa kusaidia watu kuboresha uwezo wao wa kuishi maisha ya kujitegemea katika jamii.
Katika kipindi cha miaka ya karibuni matibabu yavkisaikolojia na ya kijamii yamebuniwa. Hii ni pamoja na kusaidia familia kumudu ugonjwa, na hii inaweza kusaidia kupunguza idadi ya milipuko, na matibabu ya mitizamo tabia(Congnitive behavioural) ili kupunguza dalili chanya ving'ang'anizi. Hizi njia ni mpya na za kisasa,lakini zinatoa matumaini makubwa na kuboreaha maisha yamuathirika na hasa zikitumika pamoja na matumizi ya dawa.
Kutokana na ukubwa wa ugonjwa wa sizofrenia pamoja na ulemavu unaosababishwa na ugonjwa huu muathirika ni vizuri apewe uburu wa matumizi ya huduma sahihi ya mfumo wa afya ya akili.
NINI MAANA YA MATIBABU YA MWENENDO NA YA UFAHAMU?
Matibabu ya mwenendo, mataibabu ya ufahamu pamoja na matibabu ya ufahamu mwenendo yana baadgi vitu vitu vinavyofanana.
Misingi yake imejengwa katika utafiti na matokeo ya nadharia maalum. Mkazo wake ni katika hapa na sasa, badala ya yaliyopita, na lengo kuu la matibabu ni kusaidia kuleta mabadiliko katika maisha ya mhusika ambayo yanaweza kupimwa na kutathiminika. Malengo ya mabadiliko ya naweza kuhusishwa :-
JInsi ya kutenda: mfano kuwa mtu mchangamfu na mwenye kushirikiana na watu.
Jinsi ya kuhisi: kwa mfano kutokuwa mwoga au kutokuwa na mfadhaiko.
Jinsi ya kufikiri: kwa mfano kujifunza jinsi ya kutatua matatizo au jinsi au jinsi ya kushinda fikra potofu.
Jinsi ya kushugulikia matatizo ya kimwili au ya kimatibabu: Kwa mfano kupunguza maumivu ya mgongo.
Jinsi ya kujimudu:
Kwa mfano kufundisha mtu mwenye ulemavu fulani jinsi ya kujihudumia.
Matabibu wa ufahamu au mwenendo wanaweza kufanya kazi za watu binafsi ,vikundi au familia na matibabu yana viwango maalum vya muda. Njia hii inaweza kutumika kumsaidia mtu bila kujali akili. Kujifahamu au uwezo mwingine wowote. Mwandishi wako ni mimi Gaspar Machel Meing'ati
Sent using
Jamii Forums mobile app