Niongezee chagizo kwenye mjadala huu:
1. Kijana umeoa, bahati mbaya mzazi wako hakuwa na 'mali' za kuendeleza, kwangu mie natafsiri mali za kuendelezwa kama biashara, sio mna nyumba ya kuishi, mko humo ukoo mzima mnasema mnaendeleza....sina uhakika mnaendeleza nini humo ndani. Sana sana mnagombania urithi wa hiyo nyumba, na akili za haraka haraka huwa iuzwe ili mgawane. Kijana ukapambana kwa jasho na damu, ukaanzisha biashara kedekede, mambo safi bin murua....sasa je, ndio hizi zinazouliziwa hapa kuwa ziachiwe nani, mke, watoto au familia alikotoka mume?
2. Kijana umetoka familia Alhamdulilah....mzee alikuwa na mali kedekede za kuendelezwa na akashirikisha vijana wake (wake kwa waume) katika kuendeleza mali zake. Mzee huyu asipokuwepo tena kwenye uso wa dunia, automatically, vijana wake wataendeleza kwa nguvu ile ile (assuming sio wale waliokuwa wanasubiri mzee avute ali waponde mali kufa kwaja). Sasa kijana mmojawapo aliyekuwa na familia (mke na watoto), naye akatangulia...nafasi ya mke na watoto wake kwenye huo mwendelezo ikoje?