Nadhani hujaelewa hata nilichoandika. Hakuna sehemu hata moja nimeandika mke ni adui kama chui, soma kwa uwazi. Nimelinganisha mifumo ya maisha kwa wana ndoa tu. Hiki ulichoandika ndio huo mfumo wa kizazi kipya chenye ubinafsi
Mali zangu nikifa kama nina mke wakati huo zote anabeba mke, sio ndugu wala nani mwingine, hadi tumependana na kuoana means I trust her 100% na ni my other half, nikiondoka kila kitu anabaki nacho.
Huo ni mtazamo wako ambao ni ule wa haki sawa. Why? Unaposema mkeo ni
other half maana yake yeye si msaidizi tena, ni mwana hisa ambaye amewekeza asilimia 50 kama wewe nsdani ya ndoa. Hiyo haimaanishi hata kidogo kwamba ndio unamwamini zaidi kuliko wale wanaomchukulia mke kama sehemu ya ukoo wao. Tofauti kati ya huo mfumo wako na ule wa awali ni kuwa unajijengea ukoo wako mbali ni kuendeleza ukoo toka kwa wazazi, unakuwa umejitenga na jamii pana. Ni modern view ambapo mwanamke na mwanamume wako sawa kwa kila kitu ingawa hii ina defy natural law.
Kama nina watoto wakati huo najua sitooa jinga la kuwatupa, atawajali vizuri tu, na hakuna kulea watoto waje kua lazy, watoto walee wajue kujitafutia wenyewe, wakifika in their 20s hawahitaji hata hela za wazazi, wanakua na uwezo wa kujianzishia biashara wenyewe.
Hakuna atakaye kuoa mke mjinga, lakini wengi wa mtazamo wako wamekuja kulia majuto makuu. Process ya kupata mke mwema ni zaidi ya kupambana peke yako, inahitaji guidance, tena mke mwema anategemea malezi uliyolelewa ili kuweza kumtambua.
Watoto kufanya biashara wakifika kwenye 20s ni haja ya kila mzazi, ama wapate ajira. Kikubwa ni kuwa wajitegemee, na huo ndio mfumo wa awali ambao kwa kiasi kikubwa ulifanya hayo kwa ufanisi. Leo hii zimebaki wishful thinking tu kwa sababu mfumo wa sasa hausapoti kwa kiasi kikubwa mtazamo huo. Watoto wanafika umri huo wakiwa hawajitambui, hawana mtazamo wa future, wanatamani mwaishi kama kina Ja Rule huku hawana mbele wala nyuma. Wanashindana kukariri mashairi ya hiphop tu.
Unaposema hawahitaji hela za wazazi unakuwa umetoka nje ya mada. Kwani mzazi akifariki akaacha mali zake hupelekwa wapi? Kwenye NGO au kwenye taasisi za watoto yatima? Mtazamo huo ni wa kizazi kipya, disjointed usio na mtazamo mpana wa ukoo. Ni kama mtu anayeishi kisiwa cha peke yake akianzisha uzao wake. Ukweli ni kwamba kuna wakati mali za wazazi itabidi ziendelezwe hasa pale wanapokuwa wameacha mfumo mzuri wa kibiashara.
Swala ni kua na mke mwema tu, ukiwa na kilaza na mwenye tabia za kijinga sijui umeoa kwa sababu ipi. Ndugu watajijua aisee, wao kama walishindwa kunitumia vizuri wakafungua biashara zao wakati mi mzima, wasisumbue familia yangu kabisa nikiwa nimekufa, ni sawa na kusema mzee afe alafu uone ndugu wa baba waje kumsumbua mama, haimake sense kabisa.
Watu mnamuona mke ka chui, kama mwanamke huwezi kumuamini 100% basi usioe. I date a woman I can trust period. Love does exist
Hebu mtazame Bhahresa na mali zake, unadhani anaishi kwa mtazamo wako wewe kuwa watoto watafute mali zake na wamwache yeye wasihubutu kumwingilia? Je, ukoo wa Bharesa hawahusiki kwenye utajjri wake? Hayo ni mawazo ya maskini kuwa nikipata mali mtu asiniingilie. Hakuna anayekuingilia kwenye mali isipokuwa una mtazamo hasi.
Unapokosea ni pale unapotazama habari ya
kugawana urithi, mimi naongelea kuendeleza mali za ukoo. Siku hizi kwa sababu ya ubinafsi kila mtu anajitazama yeye, hata hao watoto wako wanaweza kugombania hizo mali na mama yao kiasi pasibaki hata kijiko. Mzazi mwema ataacha mfumo mzuri wa kibiashara ama mfumo endelevu, ili watoto wafit naturally katika huo. Hakuna habari ya ndugu kurithi mali, bali ni mali iendelezwe. Ndivyo ilivyokuwa, sio kuuza ili wagawane, watoto walisimamia moja kwa moja.
Mambo ya kumwamini mke, yalikuwa na nguvu sana kwa mfumo wa zamani, sasa hivi ni hadithi tu mkuu, wake wa leo hawatoki makwao. Ukifikia kuoa utalijua hili, lakini kubwa zaidi unatafuta mali ili ukiondoka uwaache wanao sehemu nzuri, uache legacy ndani ya ukoo. Kama unaunda ukoo wako kupitia mwanamke basi sawa, lakini kama unaendeleza ukoo, mkeo atakuwa sehemu muhimu ya ukoo wenu, tena hutathubutu kuwaambia ndugu mniache na mke wangu.
Anyway, ni mtazamo wako mkuu ambao ndio modern view.