Je, ni halali mke arithi mali mumewe akitangulia?

Je, ni halali mke arithi mali mumewe akitangulia?

Mke sio wa Ukoo na hayupo kujenga ukoo wa mtu. MKE yupo kwa ajili ya kumsaidia Mwanaume katika kutengeneza Familia yao mpya. Na ndio maana Mungu baada ya kumuumba Adam alimwambia nitakufanyia Msaidizi wa kunana nawe.....

Kwangu mimi mke ni mali yangu na sio ya Ukoo na huwa sisikilizi ushauri wa mtu maana wao sijawahi washauri kuhusu ndoa zao.


Tatizo ni kuwa Umezaliwa leo afu watembea wanataka na wewe utembee kama wao, bila kusahau hata wao walitambaa kwanza
Mke ni wako ila ni lazima atambulike katika ukoo, umeelewa? Angaliahatavitabu vya dini vinamwendelezo wa koo, unapotoka jnapojidangamya unakwenda kuanzisha ukoo wako. Utaanzisha familia ila si ukoo, na mkeo atapaswa kutambuliwa nawana ukoo. Unakujua kuwa wazazi wakikataa kumtambua mkeo ndoa hifungwi?
 
We jamaa lofa sana. Mke wangu anahusika vipi na ukoo, bora ungesema familia niliyozaliwa. Ukoo tena hao ni watu wa kufata kile nisemacho mimina hawawwzi niamlia chochote kile.
Mi mwenyewe similikiwi na mtu sembuse mke wangu
Mke ni wako ila ni lazima atambulike katika ukoo, umeelewa? Angaliahatavitabu vya dini vinamwendelezo wa koo, unapotoka jnapojidangamya unakwenda kuanzisha ukoo wako. Utaanzisha familia ila si ukoo, na mkeo atapaswa kutambuliwa nawana ukoo. Unakujua kuwa wazazi wakikataa kumtambua mkeo ndoa hifungwi?
 
We jamaa lofa sana. Mke wangu anahusika vipi na ukoo, bora ungesema familia niliyozaliwa. Ukoo tena hao ni watu wa kufata kile nisemacho mimina hawawwzi niamlia chochote kile.
Mi mwenyewe similikiwi na mtu sembuse mke wangu

tumuelewage tu hivyo hivyo huyu...sijui ana nini..ila kuna tatizo mahali..hata Wanyama ushaona mnyama anaacha kuprovide kwa 'familia' yake ana provide kwa familia nyingine?..basic instinct tu na sio ufeminist…………..1
 
Kuna shida gani mali kuandikishwa jina la watoto wa marehemu?.
Marehemu tunakuwaga na watoto wengine pia. Tukiandikisha mali zetu majina ya watoto wako, watoto wako watawazingua ndugu zao wengine ambao nao pia ni watoto wetu.

Na pia marehemu wengine wanakuwaga na mke zaidi ya mmoja. Sasa hapo inakuwaje?
 
Halafu kumbukeni, kuna mijitu ni miprofeshno ya kuoa wajane walioachiwa mali na waume zao 😁😁😁

Kwahiyo mali ukimuachia mkeo kuna misela inakuja kumuoa mkeo makusudi ili kutafuna mali za marehemu. Mpaka wanao wakikua wakubwa, misela imeshateketeza au imeshajihamishia mali ulizomuachia mkeo kwake.

Kwa ufupi mfumo wa mirathi wa wazungu kenge sana kwa sisi waafrika.
 
Na mimi nina swali la ziada? Hizo mali unazozizungumzia mwanaume atakuwa ametafuta peke yake au akiwa na mke wake?
 
Nimewezesha familia yangu na iko vema, watoto wangu ni watu wazima sasa hivyo dua lako halipo kwangu. Nzuri zaidi nafuata misingi ya dini kama ilivyo kwa familia yangu hivyo hatuishi kama panya road. Kila mtu anagangaika kujenga pake na pia tunajenga ya ukoo, kama nikitangulia watoto wangu watakuwa kwenye mikono salama. Ukiona unashaka na hilo basi ujue mmeshasambaratika vibaya, mnajiita ukoo kwa kuzaliw tu ila mioyo yenu haiko huko tena. Subiri maoni ya RC yawe sheria nadhani utafanikiwa, but until then, you are wrongly informed!!
Sasa hapa unaizungumzia familia yako kama ndio jamii nzima ilivyo. Maana hata kuoa kwako ni kwa ajili ya ukoo wako na unajinasibu huna hofu na ndugu zako ila unamhofia mkeo. Mke wako ndio mama mzazi wa watoto wako lakini kaka yako ni baba mkubwa wa wanao naye ana watoto wake na mke wake.

Mwanaume kamili hamuogopi mkewe, bali huishi naye kwa akili. Sikulaumu, unazo sababu za kumhofia mkeo maana hukumuoa kwa tafakuri yako bali familia yako.
 
tumuelewage tu hivyo hivyo huyu...sijui ana nini..ila kuna tatizo mahali..hata Wanyama ushaona mnyama anaacha kuprovide kwa 'familia' yake ana provide kwa familia nyingine?..basic instinct tu na sio ufeminist…………..1
Hujaelewa, uko tofauti na nilichosema. Integration sio ku provide. Think big.
 
Sasa hapa unaizungumzia familia yako kama ndio jamii nzima ilivyo. Maana hata kuoa kwako ni kwa ajili ya ukoo wako na unajinasibu huna hofu na ndugu zako ila unamhofia mkeo. Mke wako ndio mama mzazi wa watoto wako lakini kaka yako ni baba mkubwa wa wanao naye ana watoto wake na mke wake.

Mwanaume kamili hamuogopi mkewe, bali huishi naye kwa akili. Sikulaumu, unazo sababu za kumhofia mkeo maana hukumuoa kwa tafakuri yako bali familia yako.
Mwanaume kamili sio effeminate, umepotea. Nazungumzia integration sio hofi. Una mtazamonhasi ndio tatizo lako. Wewe hujakuta ndugu huko kwenu? Tatizo huelewi concept ila unajenga yako kichwani kama huyo anayesema eti una provisd kwa familia nyingine. Mke sio wa sehemu ila ni sehemu ya ukoo, hii ni heshima kubwa kwake. Penye shid atapata msaada, ila kw kizazi kipya hii ni kama uchawi, inaonekana haiwezekani. Kisa, maadili yamepotea, mnaishi kwa kuhofiana tu. This is biblical, nit for tjose who are worldly
 
Wakuu umuofia kwenu,

Nianze kwa kukiri kuwa hii ni mojawapo ya mada ngumu kabisa kuijadili mbele ya kizazi cha leo, yaani kizazi kipya. Najua si kila mtu ataipokea kwa mtazamo wa kupingana kwa hoja, bali wako ambao wataibuka na matusi na kejeli, kwa wakuu wa mtazamo huo, niombe tu tuvumiliane. JF where we dare to talk openly ndio motto yetu.

Nianze kwa kuelezea mtazamo wangu kuhusu mchakato mzima wa ndoa hapo awali na kisha nioanishe na kile kinachofanyika hii leo.

Mtazamo wa awali
Ndoa ilikuwa na pande mbili, kwanza kabisa ni muunganiko wa ukoo wa mwanamke na mwanamume, halafu pia ilikuwa ni muunganiko wa mume na mke na kuwa familia moja, ama mwili mmoja. Kwa kawaida mwanamke alitakiwa kusubiri nyumbani kwa wazazi wake mpaka pale atakapochumbiwa, kisha kutwaliwa na mume. Wazazi wa mume ndio waliokuwa na jukumu la kuchagua kati ya mabinti wengi ili kumpata ambaye walidhani ataweza kuendana na kijana wao kwa kuzingatia jinsi walivyomlea.

Kijana yeye alionyeshwa tu kuwa tunataka uoe binti wa familia fulani, naye alipokea kwa mikono miwili. Wazazi walishafanya uchunguzi wote kujua ni familia gani inafaa, binti ni mwenye adabu na kujua malezi, hakuna magonjwa ya kurithi kwenye ukoo husika (mfano ukoma) n.k. Taratibu za posa zilifanyika, mahari ikatolewa na harusi ikapangwa. Binti kwa upande wake hakuwa na hoja ya kujadili, wazazi wake walichunguza ukoo na familia iliyoleta posa kuona kama ni wenye maadili na wachapa kazi, ili asije akapata dhiki mara aolewapo, hakuna magonjwa ya kurithi n.k. Ndio maana ilikuwa kawaida kuambiwa tutawapeni majibu siku zijazo, mtupe muda wa kutafakari.

Sasa katika dunia ya leo utaratibu huu unaweza kudhaniwa kuwa ni wa kipuuzi na kandamizi. Mtazamo huu hasa umejengwa kwenye jamii za kiafrika na wale wa kipato chini huko ulaya na Marekani. Nasema hivyo kwa sababu mfano jamii za kihindi bado wana mchakato huo mpaka sasa, ndio maana sio rahisi kwa mmakonde kuoa binti wa kibaniani. Ndivyo ilivyo kwa familia tajiri huko ulaya na marekani, binti hawezi kukurupuka tu kuolewa na mwanamume yeyote. Sasa jambo hili lina sababu muhimu sana kwa jamii hizi:

1. Vijana wadumu katika ndoa
Sikumbuki ni mara ngapi nimesikia maharusi kutoka koo tajiri wametengana. Siongelei wasanii ambao maisha yao ni usanii, naongelea matajiri wanaojulikana hivyo, waliotulia vema na familia zao. Hawa huhakikisha watoto wao wanaoa na kuolewa kwenye familia zinazoeleweka na vijana wenye maadili. Kama familia ni tajiri lakini wana sifa mbaya (mfano wauza unga) basi wazazi hukataa posa. Wanawalinda watoto wao.

2. Kukwepa magonjwa ya kuambukiza
Wazazi walikuwa makini kuona magonjwa ya kurithi hayaingizwi kwenye ukoo. Hili lilikuwa jambo la muhimu sana kwa magonjwa kama asthma, sickle cell anaemia, reprosy n.k.

3. Kulinda mali za ukoo/ familia
Kwa sababu wazazi waliwandaa watoto wao wa kiume kulingana na shughuli wanazofanya, kijana alitarajiwa aje kuwa mrithi wa kuendeleza mali za ukoo. Wazazi walihakikisha legacy yao haifi na kwa kuwa wanadamu muda wetu ni mfupi, ilikuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa kijana anakua katika misingi ya kuendeleza hilo.

4. Kuendeleza kizazi bora
Utaratibu wote huu ulilenga kuhakikisha mwanamume anajenga kizazi bora kabisa kama mwendelezo wa ukoo. Kama mwanamke hakuwa na sifa za kuwa mke hangeweza kuolewa kwani uzao wake ungekuwa usio na maadili. Mwanamke ndiye mwalimu mkuu wa watoto katika familia.

5. Kupunguza uwezekano wa kutokea migogoro
Kwa sababu wazazi walitazama tabia na mwenendo wa mwanamke na mwanamume, hii ilipunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kutokea migogoro mikubwa isiyoweza kupata suluhu.

6. Kumfanya mwanamke kuwa sehemu ya ukoo
Mwanamke aliyeolewa kwa utaratibu huu alifanywa kuwa sehemu ya ukoo. Alibadili jina lake la mwisho kuwa la ukoo alikoolewa na ilikuwa heshima kubwa kwake. Ukoo mzima ulimpokea kama mwanafamilia na alikuwa na haki sawa na wanaukoo wengine. Kwa muktadha huu, hata matatizo yaliyojitokeza kwenye kati yake na mumewe, kimbilio la mke ilikuwa ni kwa wazazi wa mumewe (ukoo wake mpya) ambako alisikilizwa zaidi kuliko hata mumewe. Mke hakupaswa kupeleka shauri lolote kwao bali kama kungekuwa na tatizo kubwa la kuweza kufikia kushirikisha wazazi wake, basi wazazi wa mume wangehusika katika hilo, sio mwanamke ama mume wake.

Ndoa za siku hizi
Siku hizi ndoa si kati ya koo mbili, mchakato umetekwa na watoto. Mtoto anatafuta mke wake mwenyewe, anampeleka kwa wazazi wake kumtambulisha. Sasa mke wa namna hii hawawezi kamwe kuchangamana na wazazi wa mume, ndivyo ilivyo pia kwa upande wa wazazi wa mwanamke, hawawezi kwenda sawa na kijana muoaji.

Utakuta mtazamo wa ndoa kwa kijana ni tofauti kabisa na wazazi. Kinachofanyika ni wazazi kuamua kuruhusu tu waoane ili kuepusha lawama za kizazi kipya. Wazazi wa binti wataruhusu binti aolewe hata bure kwa sababu anaweza kuzalia nyumbani, kwani mara nyingi inapoletwa posa, ujue watu hao walishachomana sana tu. Sasa wamelewa penzi, ndipo wakaamua watafute ushahidi kwa jamii kwamba wanalala pamoja.

Sasa athari za ndoa ya aina hii
1. Hakuna muunganiko kati ya mke na wazazi wa mume
Mara nyingi muunganiko huu haupo kabisa. Wazazi hawaafikiani na mwenendo wa mwanamke na hivyo kuona mwana wao amepotea. Wakati binti akiolewa hapo zamani ilikuwa kawaida kabisa kumtembeza kwa ndugu mbalimbali ambako alipewa heshima kubwa na kutambulika rasmi kama mmoja wa wanaukoo. Lakini kwa mfumo wa kisasa, si ajabu kwa mwanamke kujulikana na wazazi wa mume tu, nasema kujulikana na si kuchangamana.

2. Hakuna muunganiko kati ya mume na mke
Kwa sababu wamekutana na kujenga mahusiano kwa kuzingatia mambo ya juu juu (false premises), pindi mambo hayo yanapoyumba ufa hutokea. Kila mmoja ana namna ya ku-react pale hali inapobadilika, hawana tabia zinazofanana. Sasa ijulikane kuwa ndoa sio mali bali ni character. Kama hamuendani kwenye tabia na mitazamo, basi ndoa haiwezi kuwa na maisha marefu. Ndipo tulipopata ule msemo ndoa ni kufanana, sio kufaana!!

3. Wazazi wanapoteza imani na kijana wao
Kama hapo juu, kwa vile wazazi wamemhesabu kijana wao kama amepotea, basi ni ushahidi kwao kuwa hana uwezo wa kujenga ukoo bora na pia kusimamia mali za familia. Hawawezi kukubali kamwe kumwamini katika hilo na pia hata mke watamwona kama ni mporaji tu. Wanaanzaje kuwa na imani na mwanamke ambaye hata historia yake hawaijui wala ukoo aliotoka?

4. Mume atatatoka kwao lakini mke atabaki kwao
Wakati mwanamume anatarajiwa kuwaacha wazazi wake akiambatana na mkewe wakaendeleze ukoo, ukweli ni kuwa mke atabaki kwa wazazi wake na mumewe atakuwa part time. Ni kawaida kwa mwanamke huyu pale akipishana na mumewe kusema sijafukuzwa kwetu, kama umenichoka nirudishe n.k. Huyu sio mwajiriwa wa kudumu, ni kibarua tu ndani ya ndoa asiye na mkataba. Kwani hata akiona mambo yamekuwa magumu kimaisha hachelei kumwacha mumewe kwa sababu hana muunganiko wa kweli naye. Tena anaweza hata kuanzisha project za siri akishirikiana na watu wa kwao (akimwibia mume). Ni aina ya mwanamke ambaye mara tu anapoingia kwenye ndoa huanza kujiandaa kutoka.

5. Mke atakuwa adui wa kudumu wa ndugu wa mume
Mwanamke wa namna hii huwa ugomvi wa kudumu na ndugu wa mumewe, hasa wanawake wenzake. Hii hutokana na ama mafundisho potofu kuwa usiruhusu ndugu wa mume wakuzoee watavunja ndoa, ama sababu ya kutokubalika kwake ndani ya ukoo. Jambo hili litampelekea mwanamume kutothaminiwa na ndugu zake na hivyo wengi wa wanaume hujikuta wakijipambanua zaidi na ukoo wa mwanamke na hivyo wao kuolewa. Nyumba hugeuka kaa la moto kwa ndugu wa mume huku ndugu wa mke wakikaa kwa nafasi, mwanamume kwa vile hajui maana ya ndoa huona kuwa jambo la kawaida huku aliwatupia lawama ndugu na wazazi wake.

Vipi kuhusu mali?
Kufuatia mazingira ndoa za zamani, mwanamke hakuhitaji kurithi mali kwa sababu tayari alikuwamo kwenye ukoo wa mumewe. Hata kama mumewe angefariki, wazazi/ndugu wangesimamia mali hizo pamoja na matunzo ya mwanamke na watoto mpaka watoto wa kiume wapate ufahamu. Mwanamke kama mwolewaji asingeweza kurithi mali za ukoo kwani mali kwenda kwa mwanamke ni kuhamishia kwenda ukoo wake. Hata mtoto wa kike hakurithi kutoka kwa baba yake kwa sababu ataolewa kwenda kujenga ukoo mwingine. Pia kama mambo yangemshinda alipaswa kurudi nyumbani kwao ambako mali za ukoo zilitunzwa.

Mazingira ya namna hii yaalipelekea wazazi kuacha mali zao zisimamiwe na watoto wao wa kiume kwani walijua ziko kwenye mikono salama. Lakini leo hii hakuna mzazi anakubali kutoa mali zake kwa mtoto wa kiume kwa sababu ya mwenendo usiofaa. Kwa sababu ile misingi ya kuendeleza mali imekiukwa, vijana wamekuwa wanahisa kwenye ndoa, asilimia 50 kwa 50, hakuna muoaji wala muolewa. Vijana wanaanzisha koo zao wala si kuendeleza ukoo, yaani kilichobaki ni kujitambulisha kwa majina tu, mimi ni ukoo wa Lizarazu lakini kiuhalisia ni ukoo mpya kabisa. Ni kawaida siku hizi kuwaonyawazazi wasiingilie mahusiano ya watoto, tena mada hizi fitinishi zikitokea mpaka kweenye nyumba za ibada. Wazazi wako waliojinyima kukujengeamaisha ya baadaye unawatosa kwa sababu ya tamaa za kimwili. Baada ya kujidhiki ili mtoto wao awe na maisha bora, anakuja kuwalinganisha na mali na kuona hawaenei. Dunia inakwenda kasi sana.

Wako wanaojipambanua kudai wao wametafuta mali peke yao wakiwa na wake zao, hivyo mali hizo ni zao. Hawa huanzisha ukoo mpya kwa kutazama mali ambazo ikitokea zikaisha, wao ama watoto wao hutaabika sana kwa kukosa ndugu wa kuwa karibu nao. Walitumainia mali kuliko kuwekeza katika kuendeleza ukoo. Ndio maana siku hizi kumeibuka vita kubwa ya kugombea mali punde mume anapofariki. Hebu waza tu kwa akili ya kawaida, marehemu mzee wetu alietuacha màjuzi halafu mali zote zirithiwe na mke na hivyo ukoo wake kupotea kwenye ramani ya matajiri, kuna usawa hapo? Mwanamke atahamisha mali kwenda kwa ukoo wake.

Hizi ni baadhi ya sababu kwa nini mwanamke hakuwekewa kurithi mali tangu enzi. Tusubiri hoja za Mh Makonda kama zitaleta mabadiliko ya sheria.
Kwa changamoto nilizopitia kutoka kwa ndugu, bora apewe mke wangu na watoto
 
Kwa leo inaonekana ni upuuzi kwa kuwa hakuna ndoa, ni usanii tu
YAANI HUFAI KUWA HAKIMU wala MSULUHISHI sembuse Mwl labda ni wale Maalim wa DINI au Wachungaji wa Kilokole
Hadithi yako ni ya kizamani ya Mfumodume
Kifupi tu Wanawake wana mali na wana waoa wanaume sasa hapo Mzee mzima akachukue eti Mali za Irene Uwoya alzozitafuta kwa sababu tu wewe ni Baba wa Dogo janja
au mwanao kamuoa mke wa Diamond mwenye mali tangu akiwa Uganda
Kuna Mawaziri wana wake, Wakuu wa Wilaya huko Kisarawe kwani hawataolewa?
je Mwanao akiolewa na Kidoti utavimbisha tumbo uukahoji makochi au shuka pkitokea msiba
HEBU ACHENI MILA Z AJABU MSIWAINGILIE KABISA WATOTO unakuwa km Mama wa Bilionea leo anataka mali za wajukuu km ni za majini au dhuluma
Kaeni pembeni jama
 
Inaonekana wazaziwako hawakukulea vema, asante kwamtazamo wako. Ni kawaida kwa kizazi kipya kutoelewa mada
kubaliana na upande wa pili usiwe BIAS tu wakati mali si zako, watoto walivyozipata ni zao hata km umewarithisha vijana wengi Marioo hamtataka waoe au wakioa na ninyi mnajisogea muoe ukoo mzima kwa vile Ben Paul katokea Dodoma kao Nairobi, akifiwa na mke nendeni Kenya mkakione
Badilikeni
 
Hujaelewa, uko tofauti na nilichosema. Integration sio ku provide. Think big.

wewe ndio hujaelewa,kama sio natural ku provide kwa familia isiyo yako..nini kinachokupelekea kuiacha familia yako kwa mtu mwingine..???...
 
Mhh ama kweli ndo mana Lowasa alisema vipaumbele vyake ni Elimu Elimu Elimu..
Mpaka hapa umeonyesha ulivyo na taarifa hafifu juu ya jambo hili.

Hiyo elimu unayodai unayo ni dhahiri unayo nusu nusu, hafifu.

Nakwambia hivi kwa sababu huna elimu ya mwanaume ni nani na mwanamke ni nani? Hujui hawa watu wawili ni nani.

Aidha, huna elimu ya mali ni nini, hutoka wapi na hupatikanaje.

Vile vile hujui ni nani anastahili kuendeleza au kurithi mali endapo mwenye mali akifariki.

Narudia kukuhakikishia kwamba, taarifa ulizonazo juu ya mwanaume, mwanamke, mali na urithi ni nusu nusu, hafifu na za uzushi.

Tazama mwili unavyofanya kazi. Jinsi hii ya viungo vya mwili unavyofanya kazi huitwa mfumo. Mwanaume pekee ndiye amepewa uwezo wa kutengeneza mfumo.

Mwanaume akiwa ndiye aliyepewa uwezo wa kutengeneza mfumo, ndivyo hivyo hivyo anawajibika kumfundisha mwanamke.

Wanawake wameumbwa wakapewa uwezo wa kusimamia mfumo.

Hivi ndivyo unaweza kuona ulimwenguni wanawake wakiwa na hali mbalimbali.

Kumbuka: elimu nzuri ni "maarifa". Tafuta maarifa usitafute elimu. Utajua ukweli.
 
Mali zangu nikifa kama nina mke wakati huo zote anabeba mke, sio ndugu wala nani mwingine, hadi tumependana na kuoana means I trust her 100% na ni my other half, nikiondoka kila kitu anabaki nacho. Kama nina watoto wakati huo najua sitooa jinga la kuwatupa, atawajali vizuri tu,
Kwa utaratibu wa vijana wa sasa wa kukutana barabarani, kuanza uzinzi na kuamua muoana, si rahisi kupata mke wa aina uliyoizungumza! Kwa mfumo wa zamani wa koo kuchunguzana, uwezekano wa kumpata mke wa aina hiyo ulikuwa mkubwa.

Nakubaliana na wewe kuwa unamwachia mali mkeo, ni sawa kwa kuwa umesema utakuwa hukuoa mwanamke mjinga wa kuwatupa watoto!
Je kama mke akiamua kuolewa na mwanamme mwingine? Unasemaje hapo - mali ulizomwachia zinaenda kutunza watoto wako? na je kama huyo mme mpya ana watoto, si zitatunza watoto wake pia. Kumbuka mme mpya akimkoleza sawasawa, mali zote anapewa na watoto wanabaki wakiwa kabisa! Hapo utaona umuhimu wa ukoo kama alivoeleza mtoa mada.
Hii ya wanawake kuolewa tena ndio mtindo wa kisasa.
Zitakuja hoja hapa kuwa mbona mwamamme naye anaweza kuoa pindi mke akitangulia? Ni kweli, kuna tofauti, mke atakuja ndani na kwa mfumo dume hata huyo mke wa pili hatarithi mali. Je mke aliyeyefiwa atakubali kuondoka kwenye mali za marehemu akaolewe kwingine au atamleta mme mpya ndani!
 
Mpaka hapa umeonyesha ulivyo na taarifa hafifu juu ya jambo hili.

Hiyo elimu unayodai unayo ni dhahiri unayo nusu nusu, hafifu.

Nakwambia hivi kwa sababu huna elimu ya mwanaume ni nani na mwanamke ni nani? Hujui hawa watu wawili ni nani.

Aidha, huna elimu ya mali ni nini, hutoka wapi na hupatikanaje.

Vile vile hujui ni nani anastahili kuendeleza au kurithi mali endapo mwenye mali akifariki.

Narudia kukuhakikishia kwamba, taarifa ulizonazo juu ya mwanaume, mwanamke, mali na urithi ni nusu nusu, hafifu na za uzushi.

Tazama mwili unavyofanya kazi. Jinsi hii ya viungo vya mwili unavyofanya kazi huitwa mfumo. Mwanaume pekee ndiye amepewa uwezo wa kutengeneza mfumo.

Mwanaume akiwa ndiye aliyepewa uwezo wa kutengeneza mfumo, ndivyo hivyo hivyo anawajibika kumfundisha mwanamke.

Wanawake wameumbwa wakapewa uwezo wa kusimamia mfumo.

Hivi ndivyo unaweza kuona ulimwenguni wanawake wakiwa na hali mbalimbali.

Kumbuka: elimu nzuri ni "maarifa". Tafuta maarifa usitafute elimu. Utajua ukweli.
Umepanic
 
Back
Top Bottom