Je, ni halali mke arithi mali mumewe akitangulia?

Je, ni halali mke arithi mali mumewe akitangulia?

Mwandishi umeandika, lakini ulichoandika huna taarifa sahihi.
Umeandika mambo msingi katika maisha ya binadamu. Hapa umeandika Ndoa, Mume na Mke, Mali na urithi.
Ingefaa ukaelewa kama kila mume na mke wanaoishi pamoja ni ndoa?
Aidha, ungejiuliza: mume na mke wana sifa sawa? Ukweli ni kuwa, mume na mke wameumbwa tofauti hivi kwamba, mke ni msaidizi wa mume.
Kwa maneno mengine, na hapa nisieleweke kama nadharau wanawake la hasha! Kwa sababu hivi ndivyo walivyoumbwa. Mwanamke hana uwezo wa kumiliki mali, bila mwanaume!
Kuhusu mali hili ni suala ambalo lina misingi yake. Mali ili uipate na ili wengine waweze kuindeleza inahitaji sifa au sheria. Bila ya hizo sifa au sheria hakuna mali pia hakuna kurithi au kuendeleza mali.
Naona unachanganya vitu!huyo wa juu wa kwanza amenukuu moja ya sehemu ya Qur'an inayojibu mada yako kama ulivyoandika kichwa cha habari.
 
Hapa tunatazama mali kwa mapana yake, si nyumba wala gari mbili ama pikipiki, tunatazama mali iliyowekezwa, mfano kiwanda.

Anayepaswa kulea watoto na mke ni ukoo, najua hili litakushangaza. Mke anatakiwa atunzwe kwa taratibu za ukoo kwani ji sehemu ya ukoo na hii ni kama watoto ni wadogo bado (kwa mujibu wa swali lako). Mali oia zitatunzwa kwa ajiri ya watoto na kumsaidia mama katika siku zake akiwa hapo nyumbani. Why?

Hutokea mke akaamua kuolewa ama akapata mtu wa kumuoa ili akajenge ukoo wa mwanamume huyo, kama alisimama kuwa mrithi wa mali za mume wa kwanza, basi mali hizo huhama na kwenda kuwa mali za mume wa pili. Hii inaweza kabisa kuwakosesha haki yao watoto wa marehemu kwa sababu ya malengo ya yule mwananmume wa pili. Hivyo mali ni za watoto na sio za mke na mume, wote wanatafuta kwa ajili ya watoto wao.
Hivi, hao ndugu wa ukoo wako watawajali watoto wako zaidi ya mama yao? Wao hawana watoto wao? Kwa hiyo wewe unaishi hapo ukitaraji kuwa ukifa ndugu zako watalea watoto wako, si ndio? You are so late. Muwezeshe mamaao kiuchumi, huyo ndio mwenye jukumu. Mke ni wako sio wa ukoo, unless kama mlishirikiana kumuoa
 
Wakuu umuofia kwenu,

Nianze kwa kukiri kuwa hii ni mojawapo ya mada ngumu kabisa kuijadili mbele ya kizazi cha leo, yaani kizazi kipya. Najua si kila mtu ataipokea kwa mtazamo wa kupingana kwa hoja, bali wako ambao wataibuka na matusi na kejeli, kwa wakuu wa mtazamo huo, niombe tu tuvumiliane. JF where we dare to talk openly ndio motto yetu.

Nianze kwa kuelezea mtazamo wangu kuhusu mchakato mzima wa ndoa hapo awali na kisha nioanishe na kile kinachofanyika hii leo.

Mtazamo wa awali
Ndoa ilikuwa na pande mbili, kwanza kabisa ni muunganiko wa ukoo wa mwanamke na mwanamume, halafu pia ilikuwa ni muunganiko wa mume na mke na kuwa familia moja, ama mwili mmoja. Kwa kawaida mwanamke alitakiwa kusubiri nyumbani kwa wazazi wake mpaka pale atakapochumbiwa, kisha kutwaliwa na mume. Wazazi wa mume ndio waliokuwa na jukumu la kuchagua kati ya mabinti wengi ili kumpata ambaye walidhani ataweza kuendana na kijana wao kwa kuzingatia jinsi walivyomlea.

Kijana yeye alionyeshwa tu kuwa tunataka uoe binti wa familia fulani, naye alipokea kwa mikono miwili. Wazazi walishafanya uchunguzi wote kujua ni familia gani inafaa, binti ni mwenye adabu na kujua malezi, hakuna magonjwa ya kurithi kwenye ukoo husika (mfano ukoma) n.k. Taratibu za posa zilifanyika, mahari ikatolewa na harusi ikapangwa. Binti kwa upande wake hakuwa na hoja ya kujadili, wazazi wake walichunguza ukoo na familia iliyoleta posa kuona kama ni wenye maadili na wachapa kazi, ili asije akapata dhiki mara aolewapo, hakuna magonjwa ya kurithi n.k. Ndio maana ilikuwa kawaida kuambiwa tutawapeni majibu siku zijazo, mtupe muda wa kutafakari.

Sasa katika dunia ya leo utaratibu huu unaweza kudhaniwa kuwa ni wa kipuuzi na kandamizi. Mtazamo huu hasa umejengwa kwenye jamii za kiafrika na wale wa kipato chini huko ulaya na Marekani. Nasema hivyo kwa sababu mfano jamii za kihindi bado wana mchakato huo mpaka sasa, ndio maana sio rahisi kwa mmakonde kuoa binti wa kibaniani. Ndivyo ilivyo kwa familia tajiri huko ulaya na marekani, binti hawezi kukurupuka tu kuolewa na mwanamume yeyote. Sasa jambo hili lina sababu muhimu sana kwa jamii hizi:

1. Vijana wadumu katika ndoa
Sikumbuki ni mara ngapi nimesikia maharusi kutoka koo tajiri wametengana. Siongelei wasanii ambao maisha yao ni usanii, naongelea matajiri wanaojulikana hivyo, waliotulia vema na familia zao. Hawa huhakikisha watoto wao wanaoa na kuolewa kwenye familia zinazoeleweka na vijana wenye maadili. Kama familia ni tajiri lakini wana sifa mbaya (mfano wauza unga) basi wazazi hukataa posa. Wanawalinda watoto wao.

2. Kukwepa magonjwa ya kuambukiza
Wazazi walikuwa makini kuona magonjwa ya kurithi hayaingizwi kwenye ukoo. Hili lilikuwa jambo la muhimu sana kwa magonjwa kama asthma, sickle cell anaemia, reprosy n.k.

3. Kulinda mali za ukoo/ familia
Kwa sababu wazazi waliwandaa watoto wao wa kiume kulingana na shughuli wanazofanya, kijana alitarajiwa aje kuwa mrithi wa kuendeleza mali za ukoo. Wazazi walihakikisha legacy yao haifi na kwa kuwa wanadamu muda wetu ni mfupi, ilikuwa ni muhimu kuhakikisha kuwa kijana anakua katika misingi ya kuendeleza hilo.

4. Kuendeleza kizazi bora
Utaratibu wote huu ulilenga kuhakikisha mwanamume anajenga kizazi bora kabisa kama mwendelezo wa ukoo. Kama mwanamke hakuwa na sifa za kuwa mke hangeweza kuolewa kwani uzao wake ungekuwa usio na maadili. Mwanamke ndiye mwalimu mkuu wa watoto katika familia.

5. Kupunguza uwezekano wa kutokea migogoro
Kwa sababu wazazi walitazama tabia na mwenendo wa mwanamke na mwanamume, hii ilipunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kutokea migogoro mikubwa isiyoweza kupata suluhu.

6. Kumfanya mwanamke kuwa sehemu ya ukoo
Mwanamke aliyeolewa kwa utaratibu huu alifanywa kuwa sehemu ya ukoo. Alibadili jina lake la mwisho kuwa la ukoo alikoolewa na ilikuwa heshima kubwa kwake. Ukoo mzima ulimpokea kama mwanafamilia na alikuwa na haki sawa na wanaukoo wengine. Kwa muktadha huu, hata matatizo yaliyojitokeza kwenye kati yake na mumewe, kimbilio la mke ilikuwa ni kwa wazazi wa mumewe (ukoo wake mpya) ambako alisikilizwa zaidi kuliko hata mumewe. Mke hakupaswa kupeleka shauri lolote kwao bali kama kungekuwa na tatizo kubwa la kuweza kufikia kushirikisha wazazi wake, basi wazazi wa mume wangehusika katika hilo, sio mwanamke ama mume wake.

Ndoa za siku hizi
Siku hizi ndoa si kati ya koo mbili, mchakato umetekwa na watoto. Mtoto anatafuta mke wake mwenyewe, anampeleka kwa wazazi wake kumtambulisha. Sasa mke wa namna hii hawawezi kamwe kuchangamana na wazazi wa mume, ndivyo ilivyo pia kwa upande wa wazazi wa mwanamke, hawawezi kwenda sawa na kijana muoaji.

Utakuta mtazamo wa ndoa kwa kijana ni tofauti kabisa na wazazi. Kinachofanyika ni wazazi kuamua kuruhusu tu waoane ili kuepusha lawama za kizazi kipya. Wazazi wa binti wataruhusu binti aolewe hata bure kwa sababu anaweza kuzalia nyumbani, kwani mara nyingi inapoletwa posa, ujue watu hao walishachomana sana tu. Sasa wamelewa penzi, ndipo wakaamua watafute ushahidi kwa jamii kwamba wanalala pamoja.

Sasa athari za ndoa ya aina hii
1. Hakuna muunganiko kati ya mke na wazazi wa mume
Mara nyingi muunganiko huu haupo kabisa. Wazazi hawaafikiani na mwenendo wa mwanamke na hivyo kuona mwana wao amepotea. Wakati binti akiolewa hapo zamani ilikuwa kawaida kabisa kumtembeza kwa ndugu mbalimbali ambako alipewa heshima kubwa na kutambulika rasmi kama mmoja wa wanaukoo. Lakini kwa mfumo wa kisasa, si ajabu kwa mwanamke kujulikana na wazazi wa mume tu, nasema kujulikana na si kuchangamana.

2. Hakuna muunganiko kati ya mume na mke
Kwa sababu wamekutana na kujenga mahusiano kwa kuzingatia mambo ya juu juu (false premises), pindi mambo hayo yanapoyumba ufa hutokea. Kila mmoja ana namna ya ku-react pale hali inapobadilika, hawana tabia zinazofanana. Sasa ijulikane kuwa ndoa sio mali bali ni character. Kama hamuendani kwenye tabia na mitazamo, basi ndoa haiwezi kuwa na maisha marefu. Ndipo tulipopata ule msemo ndoa ni kufanana, sio kufaana!!

3. Wazazi wanapoteza imani na kijana wao
Kama hapo juu, kwa vile wazazi wamemhesabu kijana wao kama amepotea, basi ni ushahidi kwao kuwa hana uwezo wa kujenga ukoo bora na pia kusimamia mali za familia. Hawawezi kukubali kamwe kumwamini katika hilo na pia hata mke watamwona kama ni mporaji tu. Wanaanzaje kuwa na imani na mwanamke ambaye hata historia yake hawaijui wala ukoo aliotoka?

4. Mume atatatoka kwao lakini mke atabaki kwao
Wakati mwanamume anatarajiwa kuwaacha wazazi wake akiambatana na mkewe wakaendeleze ukoo, ukweli ni kuwa mke atabaki kwa wazazi wake na mumewe atakuwa part time. Ni kawaida kwa mwanamke huyu pale akipishana na mumewe kusema sijafukuzwa kwetu, kama umenichoka nirudishe n.k. Huyu sio mwajiriwa wa kudumu, ni kibarua tu ndani ya ndoa asiye na mkataba. Kwani hata akiona mambo yamekuwa magumu kimaisha hachelei kumwacha mumewe kwa sababu hana muunganiko wa kweli naye. Tena anaweza hata kuanzisha project za siri akishirikiana na watu wa kwao (akimwibia mume). Ni aina ya mwanamke ambaye mara tu anapoingia kwenye ndoa huanza kujiandaa kutoka.

5. Mke atakuwa adui wa kudumu wa ndugu wa mume
Mwanamke wa namna hii huwa ugomvi wa kudumu na ndugu wa mumewe, hasa wanawake wenzake. Hii hutokana na ama mafundisho potofu kuwa usiruhusu ndugu wa mume wakuzoee watavunja ndoa, ama sababu ya kutokubalika kwake ndani ya ukoo. Jambo hili litampelekea mwanamume kutothaminiwa na ndugu zake na hivyo wengi wa wanaume hujikuta wakijipambanua zaidi na ukoo wa mwanamke na hivyo wao kuolewa. Nyumba hugeuka kaa la moto kwa ndugu wa mume huku ndugu wa mke wakikaa kwa nafasi, mwanamume kwa vile hajui maana ya ndoa huona kuwa jambo la kawaida huku aliwatupia lawama ndugu na wazazi wake.

Vipi kuhusu mali?
Kufuatia mazingira ndoa za zamani, mwanamke hakuhitaji kurithi mali kwa sababu tayari alikuwamo kwenye ukoo wa mumewe. Hata kama mumewe angefariki, wazazi/ndugu wangesimamia mali hizo pamoja na matunzo ya mwanamke na watoto mpaka watoto wa kiume wapate ufahamu. Mwanamke kama mwolewaji asingeweza kurithi mali za ukoo kwani mali kwenda kwa mwanamke ni kuhamishia kwenda ukoo wake. Hata mtoto wa kike hakurithi kutoka kwa baba yake kwa sababu ataolewa kwenda kujenga ukoo mwingine. Pia kama mambo yangemshinda alipaswa kurudi nyumbani kwao ambako mali za ukoo zilitunzwa.

Mazingira ya namna hii yaalipelekea wazazi kuacha mali zao zisimamiwe na watoto wao wa kiume kwani walijua ziko kwenye mikono salama. Lakini leo hii hakuna mzazi anakubali kutoa mali zake kwa mtoto wa kiume kwa sababu ya mwenendo usiofaa. Kwa sababu ile misingi ya kuendeleza mali imekiukwa, vijana wamekuwa wanahisa kwenye ndoa, asilimia 50 kwa 50, hakuna muoaji wala muolewa. Vijana wanaanzisha koo zao wala si kuendeleza ukoo, yaani kilichobaki ni kujitambulisha kwa majina tu, mimi ni ukoo wa Lizarazu lakini kiuhalisia ni ukoo mpya kabisa. Ni kawaida siku hizi kuwaonyawazazi wasiingilie mahusiano ya watoto, tena mada hizi fitinishi zikitokea mpaka kweenye nyumba za ibada. Wazazi wako waliojinyima kukujengeamaisha ya baadaye unawatosa kwa sababu ya tamaa za kimwili. Baada ya kujidhiki ili mtoto wao awe na maisha bora, anakuja kuwalinganisha na mali na kuona hawaenei. Dunia inakwenda kasi sana.

Wako wanaojipambanua kudai wao wametafuta mali peke yao wakiwa na wake zao, hivyo mali hizo ni zao. Hawa huanzisha ukoo mpya kwa kutazama mali ambazo ikitokea zikaisha, wao ama watoto wao hutaabika sana kwa kukosa ndugu wa kuwa karibu nao. Walitumainia mali kuliko kuwekeza katika kuendeleza ukoo. Ndio maana siku hizi kumeibuka vita kubwa ya kugombea mali punde mume anapofariki. Hebu waza tu kwa akili ya kawaida, marehemu mzee wetu alietuacha màjuzi halafu mali zote zirithiwe na mke na hivyo ukoo wake kupotea kwenye ramani ya matajiri, kuna usawa hapo? Mwanamke atahamisha mali kwenda kwa ukoo wake.

Hizi ni baadhi ya sababu kwa nini mwanamke hakuwekewa kurithi mali tangu enzi. Tusubiri hoja za Mh Makonda kama zitaleta mabadiliko ya sheria.
Umenigusa.
 
Nadhani hatujaelewana dhana ya urithi. Labda niulize, watoto wako wakitafuta mali zao lakini mwosho wa siku ukifariki hizo mali zako utazikwa nazo? Hatuongelei kugawa mali kwa watoto, tunaongelea pale unapoacha mali zifanyiwe nini.

Kuna tatizo kwenye jamii ambapo watu wanatazama urithi kama kugawana mali, si kweli. Tutazame ule mwisho, sio tamaa za hivu karibuni kutaka kila mtu apate japo kijiko. Mfano una kiwanda kidogo, halafu umekufa na wosia wako kwamba watoto watafute malo zao binafsi, jna maana kiwanda kiende serikalini? Hapo ndipo ilipo hoja yangu

Uite mali, uite urithi sawa. Hapa umetoa mfano wa Kiwanda. Hicho hakikutokea kama tunavyoamini Mungu alisema "kiwe kiwanda" boom hicho. Mtu alikifanyia kazi kukiweka hapo kilipo. Watoto, na wengineo wanapaswa kulijua hilo. Hata hicho wanaweza kukichukua kwa kufanyia kazi si kupewa bure.
 
Hivi umeona Familia zinazowafanya wanawake na watoto wa marehemu akiacha Mali...unasema wanawatunzai...mbona Kama wewe Ni bwege uliekubikwa na upotofu juu wa wanawake. Bila Shaka utakua Mkurya...Bado utakuja na mada ya kukeketa watoto wa kike ni sawa.

Nahurumia kizazi chako na mkewako...Watapata taaabu sanaaaa.....NILIJUA MTU MZIMA KAMA WEWE UMEONA MENGI YA DUNIA lakini.baado Sana.
 
Basi tufahamishe anaemuongoza...

Sijui mna nini kichwani abt women..wkt hizi ni zama Mama Samia is the Vice President
Uko na mwelekeo fulani. Kwa kweli sio kosa kuelewa hivyo kama tu hauleti matatizo kwako na wengine.

Katika hoja zangu kama umesoma na kuelewa nimesema, mwanamke hana uwezo wa kumiliki mali. Lakini ameumbwa kuwa msaidizi wa mume.

Mashaka yangu ni kuwa hujaelewa maana ya neno "msaidizi". Hivyo unaelewa kwamba mimi nawakandamiza wanawake.

Binafsi naelewa ukweli na nafasi ya mwanamke katika maisha. Kwa sababu hiyo siandiki hivi kuondoa, kudharau, au kutothamini utu na ubinadamu wa mwanamke. Yeye ni kiumbe sawa mbele ya Mungu akiwa na nafasi ya " msaidizi".

Kifupi ni kuwa, mwanamke hawezi kufanya chochote nacho kwa hicho kikawa na manufaa kama hakuna mfumo wa kumuongoza na mafundisho.
 
Kwahiyo umeleta mada biased ili sisi tuinyooshe? Hukutakiwa kuwa authoritative in that case bali inquisitive
Walioelewa wanatoa maoni yako, si kila mtu ataona value ya kila jambo. Ziko mada nyingine unaweza kusoma na kuchangua pia
 
Hivi, hao ndugu wa ukoo wako watawajali watoto wako zaidi ya mama yao? Wao hawana watoto wao? Kwa hiyo wewe unaishi hapo ukitaraji kuwa ukifa ndugu zako watalea watoto wako, si ndio? You are so late. Muwezeshe mamaao kiuchumi, huyo ndio mwenye jukumu. Mke ni wako sio wa ukoo, unless kama mlishirikiana kumuoa
Nimewezesha familia yangu na iko vema, watoto wangu ni watu wazima sasa hivyo dua lako halipo kwangu. Nzuri zaidi nafuata misingi ya dini kama ilivyo kwa familia yangu hivyo hatuishi kama panya road. Kila mtu anagangaika kujenga pake na pia tunajenga ya ukoo, kama nikitangulia watoto wangu watakuwa kwenye mikono salama. Ukiona unashaka na hilo basi ujue mmeshasambaratika vibaya, mnajiita ukoo kwa kuzaliw tu ila mioyo yenu haiko huko tena. Subiri maoni ya RC yawe sheria nadhani utafanikiwa, but until then, you are wrongly informed!!
 
Uite mali, uite urithi sawa. Hapa umetoa mfano wa Kiwanda. Hicho hakikutokea kama tunavyoamini Mungu alisema "kiwe kiwanda" boom hicho. Mtu alikifanyia kazi kukiweka hapo kilipo. Watoto, na wengineo wanapaswa kulijua hilo. Hata hicho wanaweza kukichukua kwa kufanyia kazi si kupewa bure.
Kwa hiyo utazikwa nacho? Mbona huelewi? Jibu basi, ukifafa kigeuzwe NGO? Usikwepe hoja ya msingi, kama unasema watoto hawahusiki na mali zako, nipe jibu hapo!!
 
Hivi umeona Familia zinazowafanya wanawake na watoto wa marehemu akiacha Mali...unasema wanawatunzai...mbona Kama wewe Ni bwege uliekubikwa na upotofu juu wa wanawake. Bila Shaka utakua Mkurya...Bado utakuja na mada ya kukeketa watoto wa kike ni sawa.

Nahurumia kizazi chako na mkewako...Watapata taaabu sanaaaa.....NILIJUA MTU MZIMA KAMA WEWE UMEONA MENGI YA DUNIA lakini.baado Sana.
Umechelewa kuwahurumia, wako vizuri na miji yako, baki na ujinga wako kufikiri kila mtu mkurya, a fool at his best. Kama huwezi kujadili mada toka kwenye thread hii, ziko nyingine nyingi tu, huko jukwaa la wakubwa. Imekupasa uwaombe radhi wakurya kwa kuwakashifu.

Men of corrupted mind!!
 
Uko na mwelekeo fulani. Kwa kweli sio kosa kuelewa hivyo kama tu hauleti matatizo kwako na wengine.

Katika hoja zangu kama umesoma na kuelewa nimesema, mwanamke hana uwezo wa kumiliki mali. Lakini ameumbwa kuwa msaidizi wa mume.

Mashaka yangu ni kuwa hujaelewa maana ya neno "msaidizi". Hivyo unaelewa kwamba mimi nawakandamiza wanawake.

Binafsi naelewa ukweli na nafasi ya mwanamke katika maisha. Kwa sababu hiyo siandiki hivi kuondoa, kudharau, au kutothamini utu na ubinadamu wa mwanamke. Yeye ni kiumbe sawa mbele ya Mungu akiwa na nafasi ya " msaidizi".

Kifupi ni kuwa, mwanamke hawezi kufanya chochote nacho kwa hicho kikawa na manufaa kama hakuna mfumo wa kumuongoza na mafundisho.
Nimeuliza swali simple tu
Oprah Winfrey anaongozwa na nani.??
Umekuja na para ndefu sana

Na conclusion yako/para ya mwisho inajicontradict na ulichoandika mwanzoni

Km unaona mwanamke ni binadamu pia anashindwaje kufanya chochote au kumiliki mali?.
 
Ukisema anayestahili una maana gani? Unazungumzia sheria ama? Kiasili mke atalelewa na watoto wake, kwa hiyo hawezi miliki mali. Why? Vipi akiamua kuolewa baada ya mume kufariki? Umewaza hilo?
Ndio maana ikaamuliwa watakaorithi ni mke na watoto. Mke akiolewa upya baada ya kifo cha mumewe mali ya watoto itabaki kwa watoto. Ukioa mjane jielewe kabisa kuwa huna haki katika mali utakayomkuta nayo, ni ya wanae.
 
Ndio maana ikaamuliwa watakaorithi ni mke na watoto. Mke akiolewa upya baada ya kifo cha mumewe mali ya watoto itabaki kwa watoto. Ukioa mjane jielewe kabisa kuwa huna haki katika mali utakayomkuta nayo, ni ya wanae.
Nimekupata mkuu
 
Km unaona mwanamke ni binadamu pia anashindwaje kufanya chochote au kumiliki mali?.
Contradiction ni wewe ambae umeshindwa kuelewa kuwa mume na mke wote ni binadamu. Yaani huyu ni mwanaume na yule ni mwanamke. Hili nalo hujalielewa. Sasa hilo lingine utalielewaje zaidi zaidi utaona ni contradiction!
 
Mke sio wa Ukoo na hayupo kujenga ukoo wa mtu. MKE yupo kwa ajili ya kumsaidia Mwanaume katika kutengeneza Familia yao mpya. Na ndio maana Mungu baada ya kumuumba Adam alimwambia nitakufanyia Msaidizi wa kunana nawe.....

Kwangu mimi mke ni mali yangu na sio ya Ukoo na huwa sisikilizi ushauri wa mtu maana wao sijawahi washauri kuhusu ndoa zao.


Tatizo ni kuwa Umezaliwa leo afu watembea wanataka na wewe utembee kama wao, bila kusahau hata wao walitambaa kwanza
Kulelewa na ukoo zama hizi za vyuma kukaza?..

Ukae nani akulee?..shemejio ama wifi ama mamkwe ama bamkwe?.utachora chini nakuhakikishia
 
Contradiction ni wewe ambae umeshindwa kuelewa kuwa mume na mke wote ni binadamu. Yaani huyu ni mwanaume na yule ni mwanamke. Hili nalo hujalielewa. Sasa hilo lingine utalielewaje zaidi zaidi utaona ni contradiction!
Mhh ama kweli ndo mana Lowasa alisema vipaumbele vyake ni Elimu Elimu Elimu...
 
Ulipaswa kuelewa hilo mapema. Sijakujibu kwasabubu ilionyesha hata ulichoandika na kukitetea huna taarifa sahihi.
Sema hujajibu kwa kua ukijibu utadhihirisha upumbavu wako

We all know Oprah ana mali na ni mwanamke contrary na kauli yako mwanamke hawezi miliki mali
 
Back
Top Bottom