NgomaNgumu
Senior Member
- Nov 20, 2010
- 194
- 24
Tunampongeza Mh Tibaijuka kwa kazi anayoifanya ya kujribu kufuata taratibu zinazohusiana na plan ya jiji kama lilivyotakiwa liwe na wizara ya ardhi. Ambalo linatia wasiwasi kidogo ktk shughuli yake ni pamoja na kukumbushana kua kunatofauti kubwa kati ya mazingira ambayo waziri huyo alichukua experience yake ya kazi na yale yaliyopo Tanzania. Hilo linaweza kumfanya awe muangalifu zaidi wakati anaposhughulikia baadhi ya kesi. Kwa mfano mwananchi anapokua na hati halali ya kumiliki ardhi ktk eneo fulani, baadae akafahamishwa kua eneo hilo halikupaswa kujengwa.
Kwa haraka kinachofahamika ni kua uwezekano wa makosa unaweza kua umetendeka ktk pande mbili, upande wa mnunuzi au wizara ya ardhi. Sasa uamuzi unaochukuliwa hivi sasa wa kumvunjia mwananchi nyumba unaonekana kama umeadhibu pande moja tu kua ndio yenye makosa ambayo ni upande wa mwananchi. Swali linalojitokeza ni kua kama mfanyakazi wa ardhi nae alihusika na tatizo hilo ima kwa kula rushwa au kitu kingine chochote, hakuna adhabu yoyote anayoipata na hivyo kumuhamasisha kuendelea kufanya hivyo tena na tena.
Ukirudi ktk hali ya nchi, waTanzania waliowengi kama amebahatika anaweza kupata nafasi ya kujenga nyumba mara moja tu ktk umri, sasa utakapomvunjia nyumba ktk sehemu ambayo alielezwa kua ni halali yeye kujenga, baadae ikabainika vinginevyo, je atakua kweli huyu mwananchi ametendewa haki? Na kweli itakua hii ni kumsaidia mwananchi au kumkandamiza? Tunanomba mchango wenu ktk hili.