Mbunge ahoji Mashine za X-Ray na Ultrasound kukaa miaka 7 bila kutumika Kituo cha Afya Upuge

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,988
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 33 leo Mei 25, 2023.


Mbunge ahoji suala la mashine za xray na ultrasound kukaa kwa miaka saba kwenye makasha ya kusafiria bila kutumika Kituo cha Afya cha Upuge

Alikiuliza swali Mbunge Athman Maige kwa Waziri wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kuwa serikali haijali kuona mashine zilizokaa katika makasha ya kusafiria kwa miaka 7 zinaweza kuharibika? Lakini pia Serikari ina ushauri gani kwa wagonjwa wanaousubiri huduma ya vifaa hivyo kama hata katika hospitali ya wilaya ambayo ipo km 5 kutoka Upuge huduma hazipatikani sababu ya kukosekana kwa mhudumu wa kutumia mashine hizo?

Akijibu swali hilo Naibu Waziri ofisi ya Rais (TAMISEMI) Deogratius J. Ndejembi aomba kuongozana na Mbunge Maige mpaka Kituo cha Afya cha Upuge wakiwa pamoja na wataalamu wa afya kuona namna gani ya kuchukua hatua sababu haikubaliki vifaa hivyo kukaa kwa miaka saba bila kutumika na kwamba changamoto nyingine zitatatuliwa pindi watakapofika kwenye kituo hicho cha afya.

Halima Mdee: Mawaziri hamna nia ya kutatua migogoro ya ardhi kwa kuwa mnanufaika nayo

Halima Mdee amedai Mawaziri wa Ardhi hawana nia ya kutatua migogoro ya ardhi kwa kuwa wanaitumia kama dili la kujipatia fedha kutumia ziara kuzunguka maeneo yenye migogoro.

Amesema Wanasema tu kuwa wanashughulikia migogoro ila ukweli ni kweli hawana nia hiyo.

WAZIRI WA ARDHI: HATI ZA HAKI MILIKI ZA KIMILA NI HALALI KISHERIA
Akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Makadirio na Matumizi ya Wizara yake kwa Mwaka 2023/2024, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula.

Amesema hadi Mei 15, 2023 mikopo ya Tsh. Bilioni 60.1 imetolewa na taasisi za fedha kwa kutumia hati za haki miliki za kimila, jumla ya Wananchi 1382 kutoka Wilaya mbalimbali wakinufaika kwa mikopo hiyo.


VIBARUA 126 WASIO NA MIKATABA WALIKABIDHIWA KUSIMAMIA MIRADI YA ARDHI DODOMA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula amesema Migogoro ya Ardhi 815 ilipokelewa #Dodoma, kati ya hiyo 429 (52.6%) ilipatiwa ufumbuzi.

Ameeleza wamebaini vyanzo vikubwa ni milki pandikizi, madai ya fidia, Wananchi kutoridhika na upimaji shirikisho, uwepo wa watumishi wengi wa kujitolea waliokosa uratibu na usimamizi na ukosefu wa maadili kwa baadhi ya watumishi.

Amesema “Tulibaini kuna vibarua 126 hawana mikataba na wanafanya kazi za Halmashauri wakiwa wamekabidhiwa miradi, hawalipwi posho, hao ndio wamekuwa chanzo kikubwa cha migogoro, tumewaondoa wote na tunafanya upembuzi.”
 
Back
Top Bottom