Je ni halali kumvunjia mtu nyumba ambae ana hati miliki halali bila fidia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je ni halali kumvunjia mtu nyumba ambae ana hati miliki halali bila fidia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NgomaNgumu, Dec 23, 2010.

 1. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunampongeza Mh Tibaijuka kwa kazi anayoifanya ya kujribu kufuata taratibu zinazohusiana na plan ya jiji kama lilivyotakiwa liwe na wizara ya ardhi. Ambalo linatia wasiwasi kidogo ktk shughuli yake ni pamoja na kukumbushana kua kunatofauti kubwa kati ya mazingira ambayo waziri huyo alichukua experience yake ya kazi na yale yaliyopo Tanzania. Hilo linaweza kumfanya awe muangalifu zaidi wakati anaposhughulikia baadhi ya kesi. Kwa mfano mwananchi anapokua na hati halali ya kumiliki ardhi ktk eneo fulani, baadae akafahamishwa kua eneo hilo halikupaswa kujengwa.

  Kwa haraka kinachofahamika ni kua uwezekano wa makosa unaweza kua umetendeka ktk pande mbili, upande wa mnunuzi au wizara ya ardhi. Sasa uamuzi unaochukuliwa hivi sasa wa kumvunjia mwananchi nyumba unaonekana kama umeadhibu pande moja tu kua ndio yenye makosa ambayo ni upande wa mwananchi. Swali linalojitokeza ni kua kama mfanyakazi wa ardhi nae alihusika na tatizo hilo ima kwa kula rushwa au kitu kingine chochote, hakuna adhabu yoyote anayoipata na hivyo kumuhamasisha kuendelea kufanya hivyo tena na tena.

  Ukirudi ktk hali ya nchi, waTanzania waliowengi kama amebahatika anaweza kupata nafasi ya kujenga nyumba mara moja tu ktk umri, sasa utakapomvunjia nyumba ktk sehemu ambayo alielezwa kua ni halali yeye kujenga, baadae ikabainika vinginevyo, je atakua kweli huyu mwananchi ametendewa haki? Na kweli itakua hii ni kumsaidia mwananchi au kumkandamiza? Tunanomba mchango wenu ktk hili.
   
 2. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwann upewe hati wakati unaona ni eneo la wazi au hifadhi ya barabara?acheni ujinga nyie ndo mnatapeliwaga kwa kuuziwa misikiti na makanisa
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Cha msingi ni je ulipewa kibali cha kujenga eneo hilo? Kuwa na hati halali hakumaanishi kuwa eneo hilo unaruhusiwa kujenga chochote unachotaka. Kama ulipewa kibali cha kujenga na hati ya kuruhusu kuhamia kwenye jengo basi una haki ya kushtaki mamlaka iliyokupa vibali hivi.

  Amandla......
   
 4. BIN BOR

  BIN BOR JF-Expert Member

  #4
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  hati halali katika sehemu isiyo halali!
   
 5. B

  Biro JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 27, 2010
  Messages: 331
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 60
  jamani mbona maeneo yapo mengi sana huko kisemvule? unaona kabisa eneo hilo toka enzi ya hizo limetengwa kama open space, unalobby kwa madiwani uchwara na maafisa ardhi wenye njaa unapewa hati akija mwenye akili timamu utabomolewa tu, kama si leo miaka kumi ijayo, utaanza kulalamika kuwa na yule afisa ardhi aadhibiwe laikini haitakurudishia jengo, imekula kwako! subiri uombwe radhi na waziri.
   
 6. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #6
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mategemeo yangu makubwa yalikua ni kwamba utatoa mawazo ya maana ktk kutatua hili tatizo, badala yake umeamuamua matusi. Naomba ujibu hoja zilizo tolewa kwani sio kua maeneo yote ya wazi kila mtu anajua yeye mwenyewe tu kua hili eneo ni la wazi na ndio maana tuna wizara ya ardhi. Haina haja ya ya raia kua mjinga au mjanja ili apate haki yake.
   
 7. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #7
  Dec 23, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ni kweli unavyosema. Sio kila mwananchi anajua maeneo ya wazi. Hii ni kutokana na kuwa ramani za maeneo haziwekwi wazi. Hii imesababisha wajanja wachache kuzichezea wanavyotaka. Watu wanauziwa viwanja na kupewa offer lakini baadaye wanagundua kuwa hiyo sehemu haikukusudiwa kwa ajili ya makazi. Si kila mwenye kulalamika ana ubavu wa kunyakuwa sehemu ambayo imeachwa wazi dhahiri na kuizungushia fence. Kwa bahati mbaya offer si hati halali ya umiliki wa sehemu. Hati halali ni title deed na hii inatolewa ikiambatana na ramani ya eneo lililopimwa. Ninavyoelewa mimi ni kuwa mwenye mamlaka ya kufuta title deed ni mheshimiwa Rais peke yake. Lakini pamoja na kuwa na title, nyumba yako inaweza kuvunjwa kama ujenzi wake haukufuata taratibu, ikiwa na maana ya kuombewa kibali cha ujenzi. Kabla ya kukupa kibali hiki, mamlaka husika ilitakiwa kuhakikisha kuwa hiyo sehemu inaruhusiwa kujenga makazi ya kuishi au la. Kama walipitisha ramani yako na kukupa kibali cha kujenga basi, Mkuu, una haki ya kupelekana hadi kwa Pilato. Lakini kama ulijijengea tu ili mradi una hati basi autakuwa na pakukimbilia.

  Amandla.......
   
 8. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,080
  Likes Received: 4,663
  Trophy Points: 280
  Wala rushwa wengi sana wizara ya ardhi, na hii utakuta wale wenye fedha ndio watoa rushwa ili wapate hata sehemu ambayo si wazi au ya kujenga,
  so wanapewa kibali feki, mama Tibaijuka acha awakomeshe, ili nidhamu irudi, na kumbuka umesema eti mtnzania anaweza kujenga nyumba moja kwa maisha yake yote, hapa hakuna maskini aliyevunjiwa nyumba ukiangalia ni mafisadi au wenye uwezo wa kutoa rushwa kupata vibali feki,
  so imekula kwao, na tunataka hata CDM ingechukua nchi mitambo kama Dowans ni kuitaifisha na mmiliki kumkamata quickly
   
 9. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,625
  Trophy Points: 280
  hayo ni matokeo ya kupata hati kwa nguvu ya pesa.Tiba usichoke kusafisha uchafu wa hao miungu watu...
   
 10. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2010
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,809
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  mimi nilishasema humu kuwa Kiwanja kisichopimwa, chenye plan ya kunjunga hata kwa macho utajua sikinunui hata kiuze senti 50 ya kiTZ au bure sikitaki, utaona mijitu inashabikia kununua kiwanja kisichopimwa kwa zaidi ya Tshs 2M wakati kilichopimwa kipo na ni chini ya Tshs 2M halafu wakivunjiwa wanalalamika, Tuna nini sisi WATZ.......................??????!!!!!!!!
   
 11. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ivi Mkuu umetumwa kumtetea mtu humu???

  Mkondo wa sheria mkiupindisha kwa faida yenu mwasema hawa ni kuwapa kidogo tu na watanimalizia kazi yangu sasa pale sheria inapo jirudi na kujiangalia kama ilichokitoa ni sawa na ulijua fika ilikuwa sio sawa sasa waaanza lalama kwa vyombo vya habari ati ni hati halali kivipi?

  Na tatizo lingine pale sheria inapo fuata mkondo wake bado mwalalama mwataka iweje sasa si mliisema hiyo wizara imeoza na ianarekebishwa sasa mwaanza kulia kumbe ndio nyie mlioshiriki kuichafua hiyo wizara si ndio maana machungu yanatokea wapi kama hukua muhusika mkuu wa kuifanya hiyo wizara kunuka rushwaaa.

   
 12. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #12
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ikumbukwe kwamba anaetetewa hapa ni raia wa kawaida na sio fisadi au hao matajiri wanaodhaniwa, kwani kwa kawaida hao matajiri wanaozungumziwa huwa hawapati nafasi ya kujenga mara moja ktk umri.

  Anazungumziwa raia ambae hakupata information za kutosha kutoka wizara ya ardhi na akaingia ktk makosa sio kwa kukusudia. Kama nilivyosisitiza mwanzo kua haina haja ya raia kua mjanja au mjinga ili apate haki yake.

  Ni kweli kua hiyo wizara imeoza na inahitaji marekibisho ndio maana nilianza kwa kumshukura Mh Tibaijuka kwa kazi anayoifanya, ingawa marekibisho ni lazima yambebeshe majukumu raia na mfanyakazi wa ardhi sawasawa ili uadilifu uchukue mkondo wake. Kwa uamuzi unaotolewa sasa wa kumvunjia mtu nyumba tu na bila kuchukua hatua yoyote kwa mfanyakazi wa ardhi, hauonekani kua unamfanyia uadilifu mtu alietapeliwa.

  Ikumbukwe kua uadilifu ndio nguzo kubwa ya demorasia na hiyo ndio inayofanya watu kupiga makelele mengi nchini yakiwemo yale ya kutaka katiba ibadilishwe. Itakua ngumu kupata maendeleo ya kweli kama raia bado haoni umuhimu hata wa kutendewa haki yake na kudhani kua kinachofanyika na wizara yoyote kimakosa basi wa kulaumiwa ni raia tu kwa kua ni mjinga.
   
 13. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,828
  Likes Received: 930
  Trophy Points: 280
  Ardhi ni mali ya serikali kwa hiyo hata ukiwa na hati 100, serikali ikiamua inakunyanganya na inabomoa sio lazima kiwe cha magumashi, la msingi ni watu wa ardhi kuwa wastarabu na waadilifu na pia na sisi tusitoe rushwa ili tupendelewe ndio mwanzo wa haya yote.
   
 14. N

  NgomaNgumu Senior Member

  #14
  Dec 24, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tunakubali wote kua ardhi ni mali ya serikali lakin kama waliuza ardhi kihalali baadae wakiihitaji hiyo ardhi kwa maslahi ya taifa ni lazima watoe fidia ili huyo mwananchi ajenge sehemu nyingine au apatiwe sehemu ya kuishi. Vingenevyo kusingekua na maana kutaja kua kuna maeneo ya wazi na yasiokua wazi. Ambacho watu wanajribu kukijadili ni uwezekano wa kutendeka haki kwa pande zote.
   
 15. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2010
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kupewa hati halali hakukifanyi kiwanja cha wazi au kisicho halali kiwe halali kwa ujenzi.
   
 16. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #16
  Dec 24, 2010
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kama ulinunua iyo ardhi kihalali utalipwa fidia kwa mujibu wa sheria, lakini leo hii ununue kiwanja kwenye eneo la wazi/hakijapimwa/hifadhi ya barabara kwa rushwa kikichukuliwa usitegemee fidia. Kuna mchezo niliuona miaka ya nyuma watu wananunua viwanja karibia na barabarani alafu wanakimbilia kujenga haraka haraka wanategea pindi nyumba zitakapowekewa alama ya x walipwe fidia ya mamilioni.
   
Loading...