Je, ni halali hatima ya maisha yetu kuamuliwa na miungu?

Una uthibitisho upi kuwa Mungu anaweza na miungu haiwezi?
Anyway nani kaumba hao miungu? Na lipi ni lengo la kuumba miungu ikiwa kuna Mungu mmoja?
miungu ni kazi ya shetani Hana uwezo wa kuumba hata sisimizi, shetani Hana uwezo wa kutoa roho ya mwanadamu,miungu ni mingi ila soko Mungu ni mmoja tu
 
Jiamulie mwenyewe, nani alikuzuwia?
We siku zote nakutambua kama kilaza wa maandiko ya kile unachokiamini, Na kama siyo naomba uniambie aya hii kutoka katika Qur'an inamaanisha nini.

Katika Qur'an, kuna aya kadhaa ambazo zinazungumzia kuhusu Qadar. Moja ya aya hizo ni Surat Al-Qamar, aya ya 49:

"Kila kitu tumekiumba kwa kipimo na kimeandikwa katika Kitabu kilichokwisha tangulia." (Qur'an 54:49)
 
Kila mmoja na ajiulize swali hili kwa dhati yake tokea moyoni; je ni halali kupangiwa maisha yako na kiumbe mwingine asiye wewe tokea kuzaliwa kwako mpaka kifo na kama haitoshi mpaka na adhabu pia juu ya matendo yako aamue yeye?

Kuna watu wameumbiwa shida na mateso yasiyo mithilika na taabu za kutosha tokea kuzaliwa mpaka kufa, halafu ukiuliza chanzo cha yote hayo utaambiwa ni mipango ya Mungu na mapenzi yake yahimidiwe, hivi tunaposema hivi huwa tunamaanisha kweli au tunazungumza kinafki ili mradi kumfurahisha huyu Bwana asituadhibu kwa kumwonesha ghadhabu yetu waziwazi kwa matokeo ya matendo yake.

What deadly sin did we commit to go through such pain?

Hatukukuomba kutuumba wala kutuleta duniani inasemekana ni mapenzi yako. Kwahiyo raha yako ni kututesa nakutufanya tukunyenyekee huku tukililia huruma yako, je hii inaingia akilini kweli?

To be honest, who is the one who tied us together in this fate!

Kuwa kuna matajiri na wapo masikini, wapo wenye mamlaka na wapo watumwa na kuna wenye vyote, kwani wale wanaokula raha maisha yao yote na wala hawana dhiki yeyote katika sehemu ya maisha yao wao waliwapa miungu kitu gani hata hawa fungu la kukosa wawe na uhalali wa kutaabika mpaka wayarudiapo mavumbi?

Even if we argue; the gods don't know, either fate is random, there is no reason behind it. The gods only throw the dice. They don't know who will get a one or a six.

Miungu ucheza pata potea na maisha yetu kiufupi hawana conscious ya kujua ni namna gani matendo yao yanatuumiza na wala hawana sababu ya msingi kwanini wanatutendea binadamu hivyo.

"So irresponsible!"

Only human beings attach reason and imbue meaning for their given fates.

"So sad!"

Kwa wale wote wanaotegemea matumaini na bahati njema kutoka kwa viumbe hawa nadhani wamepotoka na ni vyema kujisahihisha tena, kama ikiwa upo ulazima wa binadamu kuamuliwa hatima (destiny) na miungu wasio na uchungu nae, ambao wakishakubetia maisha ya aina fulani piga ua wewe ni wa hivyo hivyo tu hata ufanye nini, yaani hata uwatembelee viongozi wa kiroho, wabashiri, wasoma nyota au viganja, wachawi na vigagula majibu ni yaleyale, Sasa kama si ukichaa ni nini?

Ikiwa hatima yako ushaandikiwa kama ni dhiki ni dhiki na kama ni kufia dhambini ni dhambini kwanini waendelea kumlilia, kumsifu kwa mabaya yake, na kumwomba kwa unyenyekevu huku ukijua kabisa kuwa hatima yako haibadiliki na akishaamua au kusema lake huwa halibadiliki.

Mwisho wa siku," do not believe in good fortune too much you were all the culprits"
Hao miungu au Mungu unaweza kuthibitisha wapo kweli nje ya hadithi za watu tu?
 
We siku zote nakutambua kama kilaza wa maandiko ya kile unachokiamini, Na kama siyo naomba uniambie aya hii kutoka katika Qur'an inamaanisha nini.

Katika Qur'an, kuna aya kadhaa ambazo zinazungumzia kuhusu Qadar. Moja ya aya hizo ni Surat Al-Qamar, aya ya 49:

"Kila kitu tumekiumba kwa kipimo na kimeandikwa katika Kitabu kilichokwisha tangulia." (Qur'an 54:49)
1697023087006.png

49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo. 49

Hayo niliyokuwekea rangi nyekundu umeongezea wewe, hakuna kwenye Qur'an.

Unapata faida gani kuzuwa?

Qur'an hata tafsiri ukiongeza maneno yako weka kwenye mabano, orijino ya Kiarabu ndiyo haiongewi wala kupunguzwa hata nukta.
 
miungu ni kazi ya shetani Hana uwezo wa kuumba hata sisimizi, shetani Hana uwezo wa kutoa roho ya mwanadamu,miungu ni mingi ila soko Mungu ni mmoja tu
Kwa hiyo unapingana na maandiko ya Mungu wako mwenyewe anayetambua kuwa kuna miungu mingine inayoabudiwa kama yeye na anaonya wafuasi wake kupitia amri kuu ya kwanza wasiwaabudu? "..usiwe na miungu mingine ila mimi..." Na kama haitoshi anajimwambafai kuwa yeye ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana.
 
Hao miungu au Mungu unaweza kuthibitisha wapo kweli nje ya hadithi za watu tu?
Ndiyo maana andiko langu halikubaliani na utimamu wa nadharia hizi kwa kuwa nje ya kukosa uthibitisho, jumbe zake haziakisi uhalisia wa maisha yetu na ubebaji wa majukumu kikamilifu kwa huyo anayedai kuwa incharge wa kila kitu, kwa maana uwezi dai niko huru wakati huo huo unaniambia kila kinachotokea maishani mwangu ulishaniamulia yatokee.
 
Kwa hiyo unapingana na maandiko ya Mungu wako mwenyewe anayetambua kuwa kuna miungu mingine inayoabudiwa kama yeye na anaonya wafuasi wake kupitia amri kuu ya kwanza wasiwaabudu? "..usiwe na miungu mingine ila mimi..." Na kama haitoshi anajimwambafai kuwa yeye ni Mungu wa miungu na Bwana wa mabwana.
Nimekupa sifa za miungu na Mungu hata ukitaka kuabudu chura ukamfanya mungu ni wewe
 
Ndiyo maana andiko langu halikubaliani na utimamu wa nadharia hizi kwa kuwa nje ya kukosa uthibitisho, jumbe zake haziakisi uhalisia wa maisha yetu na ubebaji wa majukumu kikamilifu kwa huyo anayedai kuwa incharge wa kila kitu, kwa maana uwezi dai niko huru wakati huo huo unaniambia kila kinachotokea maishani mwangu ulishaniamulia yatokee.
Naam.

Mungu ni chaka tu tumeliumba sisi wenyewe, ili swali lolote likitushinda, tuwe tunalitupia kwenye hilo chaka kuubwa la Mungu wa kutungwa na sisi wenyewe, halafu tuseme "kazi ya Mungu ni fumbo kubwa, haina makosa" na uongo mwingine kama huo wa kuficha ukweli kwamba hatuna majibu ya mambo fulani.

Na kadiri tunavyoweza kupata majibu wenyewe, ndivyo umuhimu wa hilo chaka la Mungu linavyokosa umuhimu.
 
View attachment 2778760
49. Kwa hakika Sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo. 49

Hayo niliyokuwekea rangi nyekundu umeongezea wewe, hakuna kwenye Qur'an.

Unapata faida gani kuzuwa?

Qur'an hata tafsiri ukiongeza maneno yako weka kwenye mabano, orijino ya Kiarabu ndiyo haiongewi wala kupunguzwa hata nukta.
Ukiachana na mikwara na ubabaishaji mwingi kuhusu maandiko ambayo siku hizi huwezi kuyaficha tena, tufanye huko sahihi kwa yale uliyoyakata si sahihi, sasa tufanye hayo yaliyobakia pekee yake. "Kwa hakika sisi tumekiumba kila kitu kwa kipimo" yaani Allah na washirika wake wamekiumba kila kitu kwa usahihi, je haya mapungufu tunayoyaongelea hapa yalitoka wapi?
 
Hao "washirika" wake ulimpa wewe?
 
Mimi kwa maoni yangu Mungu hapaswi kuombwa anapaswa kushukuriwa tu !! kwa sababu yeye anajua Hatima ya kila mmoja na hata kama ukiomba bado yeye ndo ana list ya mibaraka na majaribu ambayo alishakuwekea kwenye mkeka wako na mara zote huwa hatupi tunachokitaka huwa anatupatia tunachostahili

Mfano unaomba gari 2023 ila ukaja kuipata 2027 may be mtoto unataman tu baada ya ndoa upate ila anakuvutia mpaka miaka mitano mbele !! tunaona kwa baadhi ya manabii mfano ibrahimu na mkewe wamekuja kupata mtoto uzeeni na hawa ni miongoni mwa viumbe ambavyo kama kweli mbingu ipo hawa majamaa watakua karibu na Mungu hatuwezi wote kumuaccess equally wote hata kama tutaenda mbinguni naamini kuna watu wa special seat mazee yaan kama pale magogoni Rais ni wa watanzania wote ila sio wote tunaweza kugonga nae glass na kuna wanaoweza kumpigia simu akiwa amelala 🤣🤣 !!

Fikiria watu wa kariba hiyo ambao wengine wamevishwa kwamba ni marafiki wa Mungu walikua tu wanasubiri maoni yake tu mkeka wao unasemaje au scenario ya David machalii wote walitolewa ila bado aliyekua anahitajika hakuwepo ikabidi afuatwe ! sio kwamba kaka zake hawakua mahiri laah! ni yeye tu alikua anamtaka tu huyo !!

Na hata kama unaomba unapewa hapo hapo basi sio kwamba ni maombi yamefanya kazi ! Ni yeye kwenye ratiba yake alijua kwamba siku ya leo atakufungulia na huenda alijua utaomba tarehe fulani!

Sasa msiniulize maswali kwamba kama anajua hatima yetu ni kwanini kuna dhambi mfano ukimuua mtu kwanini iwe dhambi wakati alijua kabisa hatima ya huyo mtu atauwawa na atakayemuua ni fulani kwanini tena uadhibiwe kwa makosa yaliyoandikwa !! mfano kesi ya Jesus Christ je wale wahuni wote waliohusika waliadhibiwa na Muumba maana hata mshikaji alikijua kifo chake hata kabla lakini iihitajika awepo watu wa kukamilisha hilo zoezi.

Shallom
 
Naam.

Mungu ni chaka tu tumeliumba sisi wenyewe, ili swali lolote likitushinda, tuwe tunalitupia kwenye hilo chaka kuubwa la Mungu wa kutungwa na sisi wenyewe, halafu tuseme "kazi ya Mungu ni fumbo kubwa, haina makosa" na uongo mwingine kama huo wa kuficha ukweli kwamba hatuna majibu ya mambo fulani.
Hakika umenena vyema, nakubaliana na wewe katika hili.
 
Hao "washirika" wake ulimpa wewe?
Hata kipofu anajua utofauti wa nafsi ya umoja "Mimi" na wingi "Sisi" ni vitu viwili tofauti, ni mapenzi yako kwa dini yako ndiyo yamekutia upofu kiasi cha kujifanisha kuwa hata kitu kama hicho kinahitaji ufafanuzi hili kuleta tafsiri tofauti.
 
Mimi kwa maoni yangu Mungu hapaswi kuombwa anapaswa kushukuriwa tu !! kwa sababu yeye anajua Hatima ya kila mmoja na hata kama ukiomba bado yeye ndo ana list ya mibaraka na majaribu ambayo alishakuwekea kwenye mkeka wako na mara zote huwa hatupi tunachokitaka huwa anatupatia tunachostahili

Mfano unaomba gari 2023 ila ukaja kuipata 2027 may be mtoto unataman tu baada ya ndoa upate ila anakuvutia mpaka miaka mitano mbele !! tunaona kwa baadhi ya manabii mfano ibrahimu na mkewe wamekuja kupata mtoto uzeeni na hawa ni miongoni mwa viumbe ambavyo kama kweli mbingu ipo hawa majamaa watakua karibu na Mungu hatuwezi wote kumuaccess equally wote hata kama tutaenda mbinguni naamini kuna watu wa special seat mazee yaan kama pale magogoni Rais ni wa watanzania wote ila sio wote tunaweza kugonga nae glass na kuna wanaoweza kumpigia simu akiwa amelala 🤣🤣 !!

Fikiria watu wa kariba hiyo ambao wengine wamevishwa kwamba ni marafiki wa Mungu walikua tu wanasubiri maoni yake tu mkeka wao unasemaje au scenario ya David machalii wote walitolewa ila bado aliyekua anahitajika hakuwepo ikabidi afuatwe ! sio kwamba kaka zake hawakua mahiri laah! ni yeye tu alikua anamtaka tu huyo !!

Na hata kama unaomba unapewa hapo hapo basi sio kwamba ni maombi yamefanya kazi ! Ni yeye kwenye ratiba yake alijua kwamba siku ya leo atakufungulia na huenda alijua utaomba tarehe fulani!

Sasa msiniulize maswali kwamba kama anajua hatima yetu ni kwanini kuna dhambi mfano ukimuua mtu kwanini iwe dhambi wakati alijua kabisa hatima ya huyo mtu atauwawa na atakayemuua ni fulani kwanini tena uadhibiwe kwa makosa yaliyoandikwa !! mfano kesi ya Jesus Christ je wale wahuni wote waliohusika waliadhibiwa na Muumba maana hata mshikaji alikijua kifo chake hata kabla lakini iihitajika awepo watu wa kukamilisha hilo zoezi.

Shallom
Qur'an 40:60.
Na Mola wenu Mlezi anasema: Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike. 60
 
Hata kipofu anajua utofauti wa nafsi ya umoja "Mimi" na wingi "Sisi" ni vitu viwili tofauti, ni mapenzi yako kwa dini yako ndiyo yamekutia upofu kiasi cha kujifanisha kuwa hata kitu kama hicho kinahitaji ufafanuzi hili kuleta tafsiri tofauti.
Wale ambao walienda shule kusomea ujinga hawajuwi "majestic plural" ni nini, sikushangai.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom