Mitazamo yao na maisha yetu

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Kwahiyo ubao ni ule ule, chaki ni zile zile, mwalimu ni yule yule ila somo limebadilika.

Leo tutajifunza kitu kingine kabisa, leo nitakufundisha na kukutahadharisha juu ya maisha yako na muingiliano wa mawazo ya watu juu yako.

Katika sayari hii ya kupwa na kujaa kwa chuki na upendo, ukweli ni kwamba huwezi kuishi maisha safi sana kiasi kwamba usisemwe wala huwezi kuishi maisha mabaya sana pia usipendwe.

Binadamu ni wale wale, ukiwa bora watakusema hata ukiwa dhaifu watakusema hivyo chaguo ni lako usemwe kwa udhaifu wako au kwa ubora wako.

Kubali kutopendwa na wote (The mountain is you, By Brianna Wiest.Page no. 185).

* NDIO. Ikiwa unahitaji kuishi maisha yenye amani na furaha basi ni lazima uwe tayari kutopendwa na watu wote. Hii haimaanishi kwamba utaishi maisha yenye kuwachukiza wengine hapana, lakini inamaanisha kwamba bila kujali ni kipi utafanya au jinsi gani utaishi binadamu watakujadili na kukusimanga tu.

Hakuna njia kwenye maisha ambayo ipo free tu ukapita bila kuchukiwa hivyo iweke akilini mwako ili usichukizwe na matendo ya wanadamu wa dunia hii.

Uhuru wa maisha yako unataka wewe kujitenga na mitazamo ya wanadamu. Wanadamu wanafki wa dunia hii ya unafki, dunia ambayo mtu akikusifia unashindwa kuelewa huyu ananisifu kweli au ananinafkia.

Somo litaishia hapa kwa kuhitimisha na sentensi kwamba "kama unataka kuwa na amani na furaha, basi kuwa tayari kuchukiwa na mtu yeyote yule, muda wowote ule kwa sababu yoyote ile bila kujali lolote lile"

Rudia kuisoma aya iliyoandikwa NDIO ili unielewe vizuri zaidi.
Mjukuu wa Dimile kaandika makala haya ??

#amanidimile #hekimayadimile #tusomevitabu #tungomaridadi
1691421362473.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom