Je, ni busara serikali kuipatia pesa Precision Air?

Je, ni busara serikali kuipatia pesa Precision Air?

Hawapewi bila masharti na mojawapo linaweza kubadilisha menejiment na serikali kuweka mtu wake kwenye bodi.

Hicho hasa ndicho muhimu Mkuu..lakini twende mbele na kurudi nyuma, hao watu wenye uwezo wa kusimamia operations za PA wakati huu ikiwa chini ya bail-out ya serikali tutawatoa wapi?! ATCL au?!...Lol

Ndio maana kwenye mada yangu nimetoa pia mfano wa nyakati ambazo serikali imewahi kutoa ama kudhamini pesa ambazo zilitolewa bila umakini wa kutathmini hakika ya urejeshwaji wake. Ninakuhakikishia, this will be the case this time too.

Precision kama wana mpango thabiti wa biashara waupeleke benki wapate pesa.

There is no risk whatsoever if precision air goes under.
 
niliwahi kuandika uzi nikiilaumu serikali kuacha hospitali na shule zake zikiwa hoi na kufadhili hospitali na shule za kanisa baada ya kuingia mkataba mwaka 1992 maarufu kama mou of 1992. wengi mliunga mkono jambo hilo na kutoa mfano wa kcmc na bugando....... kama mliunga mkono mou ya ufadhili wa miradi ya makanisa, sioni ubaya kwa precision kusaidiwa huku atcl ikiwa hoi bin taaban. TUACHE kutanguliza maslahi binafsi. leo ponda napopigwa risasi na watu wakaunga mkono, kesho akipigwa kiongozi wa chadema, cuf au nccr na polisi, je mtaunga mkono vilevile? tafakari!!!!!!!!!!!!! c.c. remote, genekai
 
Haya ni matumizi mabaya ya pesa za walipa kodi, kuanzia hao waliamua kukaa bagamoyo eti kujadili kuipa pesa Presionair, yaani yaani nchi hii inakwenda wapi , haingiii akilini kampuni ambayo inamilikiwa kwa hisa 51% na wakenya, Serikali ya Tanzania itoe pesa kuibail out, their heads need to be examined! halafu at the same time wanashindwa kuipa capital kampuni ya taifa ATCL ambayo iko hoi baada ya serikali yenyewe kuiingiza hasara kwa kuilazimisha kuiingia ubia na shirika la ndege la Afrika ya kusini wakati huo lilosababisha hasara kubwa kwa ATCL, licha ya wafanyakazi wa ATCL kushauri kuwa ubia huo ulikuwa haufai! lakini serikali ikaziba masikio mpaka mambo yalivyoenda mrama,Sasa Serikali labda ituambie what is the status of ATCL , kwa sababu serikali ndio inalipa mishahara ya wafanyakazi hao kila mwezi kupitia hazina , itawalipa mpaka lini, kama haina mpango wowote wa kuikwamua.
 
It is simple, ATCL will not wake up from its deathbed no mater how much fund will be injected to it, it is better to bail out PW because at list there are great signs of recovering. All in all Airline is a risk business especially in today's business environment. Most Airlines have closed their businesses while others have been restructured. Even Kenya Airways, is in a turmoil, it has been recording loses over the past two years. Emirates and Quarter are surviving because of their countries oil money. Precision Air should change its strategy and become a budget airline, that is the only way it can compete with the fast growing Fast Jet.




  1. Naona wameanza kuchepusha fedha za uchaguzi wa 2015 kwani milango upande mwingine haionyeshi dalili za kufunguka soon.
  2. Hata serikali wakiisadia Precision mwisho wa siku itakufa tu
  3. Viongozi wetu wamesahau kuwa biashara ni ushindani, ukishindwa unakaa pembeni wanye uwezo wafanye kazi
  4. kuna ongezeko kubwa la mashirika ya ndege duniani ambayo yanatafuta masoko kama hili lililopo Tanzania hivyo precision siyo shirika la kubebwa tena.
 
Tafiti kidogo kujua tofauti ya makampuni haya mawili. Precision air ina watanzania wenye hisa na FastJet 100% foreign. Tazama vilevile mfumo wa biashara ya kimatifa ya usafiri wa anga utanielewa.

Hivi vipaumbele vya taifa ni vipi? Yaani kweli unatetea hiyo pesa kutumika kwaajili ya hiyo kampuni ilhali ingeweza kuleta tofauti kubwa sana kama ingepelekwa kwenye huduma mbalimbali za jamii!!

Hivi watanzania wangapi wanapanda ndege mpaka hilo la kuwa bail out PW kuwe ni jambo la kuzingatiwa kwa sasa?

Unaweza kutuambiwa mchango wa PW katika taifa hili? Kiasi gani cha kodi shirika limechangia serikalini?!? Lisipokuwepo sisi kama taifa tutapata athari zipi kubwa za kutufanya tusiende mbele?!?

Hivi unaweza kutuambia ile bail out ya pamba ilileta faida zipi?

Kama bail out, nguvu zote zingeelekezwa kwa ATCL tu.
 
Same reason - Precision Air leo ikifa tutakuwa hatuna Shirika la Ndege kabisa! Kwa hiyo impact yake ni kubwa kwenye sekta hiyo. Kuhusu ATCL sijui kwa nini, lakini nafikiri haikuhitaji bail out kwani ilikuwa inapata pesa toka Serkalini wakati wote. Swali litakalobaki ni ikiwa pesa walizokuwa wanapewa zilitosha na kusimamiwa vizuri.
Hee!kwani fastjet nayo itakuwa imekufa natural death?Discpline ya matumizi ya pesa za walipa kodi wanyonge lazima izingatiwe,kwa nini tunakosa hata chembe ya huruma kwa wengi ambao hata mlo mmoja wa siku ni mitihani kwa kisingizio cha bailout.What a motherf...kind of bailout!
 
..if i were the decision making party from the TZ government side...i would go for majority of precision air shares as a condition for bail......let the TZ government acquire shares from people like mr.Shrima et al...who own majority of shares in the company.....this could save as collateral...in case they fail to pay back the bail out money(if they will get it at all).....
 
Kaka hoja yako ya 1. ndio sahihi wameshaanza, kuna harafu ya tunakupa na sisi je? ile ni kampuni ya wakenya kwa asilimia 51% leo inakuwaje ipewe hela na serikali ya Tanzania.
 
Hakika hii ni kichefuchefu.Jamani kumbuka unapokula na kipofu usimguse nkono!atasusa na hata anaweza kupindua sinia lenyewe ili wote msile.
 
Hivi Nape upo hapo kwani moja ya ilani ya chama tawala katika kile kitabu chetu maarufu imeandikwa ni kuendeleza kampuni ya ndege ya taifa ATCL iweze kuleta maisha bora kwa watanzania, hii imenyofolewa na kuwekwa Presionair? ingia jamvini utujuze.
 
It is simple, ATCL will not wake up from its deathbed no mater how much fund will be injected to it, it is better to bail out PW because at list there are great signs of recovering. All in all Airline is a risk business especially in today's business environment. Most Airlines have closed their businesses while others have been restructured. Even Kenya Airways, is in a turmoil, it has been recording loses over the past two years. Emirates and Quarter are surviving because of their countries oil money. Precision Air should change its strategy and become a budget airline, that is the only way it can compete with the fast growing Fast Jet.
Pwc become a budget airline ? Are aware that even the so called budget airpine also uses jet fuel?
 
Hii ni dhihaka kwa walipa kodi,kumbuka ATCL tuna ndege moja na wafanyakazi 200 ambao mishahara yao ni kodi zetu.how is behind precision air?CCM wanapaswa kuhukumiwa na wapiga kura hapo 2015.siku zote silaha ya mnyonge ni umoja tuungane wote katika hili.
 
Hawa ndio walioiuwa Air Tz sasa wanaomba msaada serikalini. Tz ndio uijuavyo mwisho wa siku hela hazirudi then unasikia habari mbofumbofu hii pia ni janja ya CCM kupata hela kwa ajili ya uchaguzi. Mengi tutayasikia
 
Nimeisoma mada na baadhi ya posts na kuona kuwa, kwanza mweka mada kwanza hajatoa maelezo ya kutosheleza huu mjadala.
Kwanza hizo pesa zianzotaka kutolewa na serikali ni mkopo au ni msaada?
Kama ni mkopo sioni ubaya wowote kwa sababu hili ndilo shirika pekee la ndege lenye wazawa kama shareholders.
Hii siyo ruzuku kama inayotolewa kwa mashirika ya Umma ambayo hairudi.
Kwanza PA imekuwa trusted na mabenki ya nje (European Investment Banks) na kupewa mikopo mikubwa ilitumika kupanua kampuni. Hivyo siyo ajabu na serikali yetu kama inaweza ikawekeza pia kwenye hii kampuni.
Sioni mantiki yoyote ya kuacha shirika kama hili liporomoke na kutegemea Fastjet ambalo ni la kigeni.
Nadhani serikali haitaki kurudia makosa yaliyofanyika kampuni ya wazalendo ya Kibo Breweries ilipomalizwa kwa makubaliano kati ya Kenyans na South Africans.
Ni vizuri watanzania wakajenga utamaduni wa kujivunia vitu vinavyojengwa na watanzania wenzetu. Tusiwe na wivu wa kijinga unaosababisha tuwaabudu wageni na vitu vyao tukadharau vyetu.
Angekuwa ni mhindi au mwarabu ndiye mmiliki waswahili wangekuwa wanasifu tu kutokana ulimbukeni.
nawajalia PA mafanikio mema watoke katika hali ngumu ya sasa wazawa na wazalendo wa nchi wasonge mbele na kumiliki njia zote muhimu wa uchumi wa nchi yetu.
 
What can the government do; if it invests the money to air tanzania it is just like throwing money to a bottomless pit. What can they do to ensure air travel in the country? precission should sought money from the market otherwise we hope for more fastjets.
 
This is insanity so to speak. Air Tanzania, 100% owned by the government is on its deathbed, why not try to waken it instead of this other privately owned airline co.? I cry for my country Tanzania.

Precision sio privately owned
ni public listed company
which means ni kampuni ya umma pia..
watanzania wananunua hisa zake sokoni...
 
..if i were the decision making party from the TZ government side...i would go for majority of precision air shares as a condition for bail......let the TZ government acquire shares from people like mr.Shrima et al...who own majority of shares in the company.....this could save as collateral...in case they fail to pay back the bail out money(if they will get it at all).....

exactly....
 
Hebu wawape tu, shirika lisimame lizalishe kwa faida, hisa zetu zipone lol!
Nimeshangazwa sana
jamaa wamekaa bagamoyo ati kujadili kama waipe ama wasiipe pesa..na
wakaishia kukubaliana kwamba hiyo pesa itolewe. Kwanini tusianze kwanza
kui-bailout Air Tanzania?
 
Back
Top Bottom