Je, ni busara serikali kuipatia pesa Precision Air?

Je, ni busara serikali kuipatia pesa Precision Air?

Dah mood yangu yoote imeisha. najuta kusoma hii thread, hivi hawa watu huwa wanafikiria kwa kutumia nini!!!!!!!!!!!!!! kichwa au...............???????!!!!!!!!!!!!!!
 
This can only happen in a country where its leaders have no sense of priorities!!! Air tanzania is in urgent need of capital injection so that it can at least manage its domestic routes but this government which is the 100% owner of the Airline thinks it is better to bail out its competitor precision Air than its own airline!!! There is no economic rationale for such a decision and Kikwete should veto it. Wakina Mramba warudishe fedha walizoficha Uswiss waisaidie Airline yao badala ya kutuumiza sisi walipa kodi.


It will be a crazy decision for the government to inject capital to ATCL, we are not that rich to throw away taxpayers money to a business which is certain not going to survive, I am telling you, in five years to come, KQ will be following on its knees.
 
This is insanity so to speak. Air Tanzania, 100% owned by the government is on its deathbed, why not try to waken it instead of this other privately owned airline co.? I cry for my country Tanzania.
kaka kuna watu ndani ya wizara walitaka kuifufua Air Tanzania, waulize walipata vikwazo gani ...
 
Kwenye mfumo wa kibepari tuliokubali, bailout kwa kampuni binafsi na pesa za umma siyo dhambi ili mradi tu kuwe na sababu na masharti mahsusi ya kuzirejesha pesa hizo.

Wakongwe wa mfumo huu (Marekani) wanayafanya haya. Huko Marekani kwenye usafiri wa anga hakuna shirika hata moja ambalo linamilikiwa au Serikali ina hisa hata moja, lakini kila yakiingia kwenye matatizo (ambayo ni ya kawaida katika biashara hii) usaidiwa - ikiwemo kwa kutumia mfumo wao wa kuwekwa chini ya uangalizi maalumu (Chapter 11).

Maoni ya mtoa mada mengine ni sahihi lakini si kweli kuwa matatizo ya Precision Air yanatokana na ushindani na hasa kutoka kwa FastJet. Kwa wale walioko katika sekta hii watakueleza kuwa wateja wengi wa FastJet siyo wale waliokuwa wateja wa Precision air. Kiukweli idadi ya wateja wake haijateteleka.

Tatizo lao kubwa ni kutokuwa makini katika uwekezaji wao na kiwango cha ukuwaji ambao haukuzingatia uwezo wa kampuni.

kaka are u coming from mars???? personally i am frequent flier na nilikua naitumia sana precision lakini ni kweli kinachowasumbua sasa ni ushindani tu wa kibiashara!!! kwanza nauli za precision ziko juu sana... cha kujiuliza kwa nn fast jest waweze kwa nauli ndogo kupata faida na kulipa european pilots(i assume salary zao ni kubwa kuliko local pilots) na wao precision washindwe??? wapunguze bei tu hakuna namna kwani nauli unaingia tu kwenye net unaona nauli ya precision na ya fast jet big difference!!!!

kwa kifupi walikua wanaoperate ktk unrealistic condition... just put a fare watalipa tu nakumbuka nshawai lipa dar-kia-dar laki 540,000/- wakat fast jet maximum utalipa 300,000/- but at times as low as 200,000/- go and return!!!

as for serikali wanatakiwa wawekeze izo pesa kwenye airtanzania basi hawa waachwe mpaka akili ikiwakaa sawa wakajua jinsi ya kuoperate effectively at a competitive prices!!!
 
Mngewajua ni akina nani wanaomiliki hii kampuni wala msingejiuliza maswali mengi hivi...
 
Kwenye mfumo wa kibepari tuliokubali, bailout kwa kampuni binafsi na pesa za umma siyo dhambi ili mradi tu kuwe na sababu na masharti mahsusi ya kuzirejesha pesa hizo.

Wakongwe wa mfumo huu (Marekani) wanayafanya haya. Huko Marekani kwenye usafiri wa anga hakuna shirika hata moja ambalo linamilikiwa au Serikali ina hisa hata moja, lakini kila yakiingia kwenye matatizo (ambayo ni ya kawaida katika biashara hii) usaidiwa - ikiwemo kwa kutumia mfumo wao wa kuwekwa chini ya uangalizi maalumu (Chapter 11).

Maoni ya mtoa mada mengine ni sahihi lakini si kweli kuwa matatizo ya Precision Air yanatokana na ushindani na hasa kutoka kwa FastJet. Kwa wale walioko katika sekta hii watakueleza kuwa wateja wengi wa FastJet siyo wale waliokuwa wateja wa Precision air. Kiukweli idadi ya wateja wake haijateteleka.

Tatizo lao kubwa ni kutokuwa makini katika uwekezaji wao na kiwango cha ukuwaji ambao haukuzingatia uwezo wa kampuni.
Naona kama wewe umeongea points za msingi hapa. kufeli kwa kampuni yeyote inayofanya biashara ni kitu cha kawaida sana duniani kote. na once inapotokea serikali huingilia kati kukopesha makampuni haya ili kuzuia yasife kabisa especially kama kampuni husika ina save public interest. jambo kama hili liliwahi kutokea marekani kwa mabenki makubwa kuelekea kufilisika ila serkali ikaingilia kati kuyanusuru pia kwa General motor ya marekani kilitokea kitu hicho hicho. sasa kwa precision nafikiri ni muda muafaka kwa serikali kuingilia kati kunusuru kampuni ile isife kabisa maana kwa muda huu ndio kampuni pekee ya ndege ambayo inaoperate locally na inamilikiwa na watanzania. mtoa mada naona kama ana interest binafsi na Kenya Airways (KQ) na Fastjet. maana precision ikifa hapa watanzania ndio tutakaopata shida maana haya mashirika mengine watakuwa wanatamba kama wanavyotaka na bei zitakuwa juu sana as wana masoko mengine huko watokako na hawatakubali kupeleka ndege zao kwenye viwanja vibovu vya mikoani kama wanavyofanya precision kwa sasa. so Serikali msisite kuwasaidia shirika hili la precision kwa manufaa ya watanzania.haya ni mawazo yangu kulingana na uelewa wangu mdogo wa biashara
 
Shirima aliwaamini sana wakenya sasa kilio. Ukiwa na monopoly ya soko lote la nchi, KQ walikuwa wa nini?

Mkuu,...lol

Nadhani pengine pale mwanzo Shirima alikubali hiyo partnership kwa ajili ya msaada wa capital injection kutoka KQ na pia kurahisisha upatikanaji wa ndege (i.e leasing of airlines requires substantial backing)...

Cha msingi ni kampuni kutengeneza mazingira ambayo pesa za shareholders ziko secure..until then, hiyo bail-out ni kwa ajili ya mifuko ya watu kadha wa kadha tu na it will only be a matter of time before they ask for another one.
 
Mngewajua ni akina nani wanaomiliki hii kampuni wala msingejiuliza maswali mengi hivi...
Ndiyo wale wale walioua Reli ya kati ili malori yao yapate tenda kusafisha mizigo ndani na nje ya nchi kama Rwanda, Burundi na Zaire!!

Tulia uliwe!!
 
I wonder bail out money is always available, as for TZ govt, but not for development plans.
 
Shirima aliwaamini sana wakenya sasa kilio. Ukiwa na monopoly ya soko lote la nchi, KQ walikuwa wa nini?

Lol....

Nadhani Shirima alikuwa amekubali ushirika na KQ kwa sababu ya initial capital injection mkuu. Hii pia ilimsaidia wakati wa kupata ndege za kuanzia (i.e leasing of commercial aircrafts requires substantial backing)

Ila nadhani cha msingi sana kwa sasa ni kutengeneza mazingira ambapo pesa za wawekezaji zitakuwa salama. Bila effective operational and financial controls, hiyo TZS 51 billion itakwenda moja kwa moja kwenye mifuko ya wajanja. It is a lot of money for just one company.
 
Kwenye mfumo wa kibepari tuliokubali, bailout kwa kampuni binafsi na pesa za umma siyo dhambi ili mradi tu kuwe na sababu na masharti mahsusi ya kuzirejesha pesa hizo.

Wakongwe wa mfumo huu (Marekani) wanayafanya haya. Huko Marekani kwenye usafiri wa anga hakuna shirika hata moja ambalo linamilikiwa au Serikali ina hisa hata moja, lakini kila yakiingia kwenye matatizo (ambayo ni ya kawaida katika biashara hii) usaidiwa - ikiwemo kwa kutumia mfumo wao wa kuwekwa chini ya uangalizi maalumu (Chapter 11).

Maoni ya mtoa mada mengine ni sahihi lakini si kweli kuwa matatizo ya Precision Air yanatokana na ushindani na hasa kutoka kwa FastJet. Kwa wale walioko katika sekta hii watakueleza kuwa wateja wengi wa FastJet siyo wale waliokuwa wateja wa Precision air. Kiukweli idadi ya wateja wake haijateteleka.

Tatizo lao kubwa ni kutokuwa makini katika uwekezaji wao na kiwango cha ukuwaji ambao haukuzingatia uwezo wa kampuni.
Getstart, maneno yako yalikuwa na ukweli labda miezi minane iliyopita lakini si sasa. Fastjet walipoanza ilionekana ndege ya walalahoi. Ilikuwa na first timers wengi sana, Watz walipanda ndege na watoto zao na maids wao etc. Baadaye Precision wakaanza ku-mess. Watu wakaanza kuwakimbia polepole. Sasa hivi watu wengi sana wamekimbia Precision. Watu hao ni wa makundi mawili: kundi la kwanza ni wale waliokimbia bei za kutisha za Precision (sasa wamepunguza). Kundi la pili ni wanaokimbia delays zisizo na kikomo. Hao wengi wameanza kukimbia miezi 5 iliyopita. Ni wengi sana. Mimi mmojawapo. Hali ya Precision ni mbaya sana, na wameshindwa kuweka mikakati mizuri. Delays ndo zinaua Precision sasa, maana kila mtu anakimbia.
 
Shirima aliwaamini sana wakenya sasa kilio. Ukiwa na monopoly ya soko lote la nchi, KQ walikuwa wa nini?

Lol....

Nadhani Shirima alikuwa amekubali ushirika na KQ kwa sababu ya initial capital injection mkuu. Hii pia ilimsaidia wakati wa kupata ndege za kuanzia (i.e leasing of commercial aircrafts requires substantial backing)

Ila nadhani cha msingi sana kwa sasa ni kutengeneza mazingira ambapo pesa za wawekezaji zitakuwa salama. Bila effective operational and financial controls, hiyo TZS 51 billion itakwenda moja kwa moja kwenye mifuko ya wajanja. It is a lot of money for just one company.
 
Kwa kawaida, ukiomba mkopo, hasa toka kwenye taasisi za fedha kama Benki, utatakiwa utoea maelezo juu ya shughuli unayotaka kufanya na hiyo fedha, na kama ni biashara basi utaonesha mapato na matumizi pamoja na mipango ya baadae.

Precision Air (kama ni kweli wanaomba bailout ya serikali) ni kwamba wanaomba fedha toka kwa wananchi. Kodi ya Watanzania ndiyo itatumika kuwasaidia. Lakini kabla ya hili zoezi la kukopeshana halijanyika, Precision Air wanatakiwa waweke wazi vitabu vyao ili Watanzania wajiridhishe kuwa huyu mkopaji ana uwezo wa kuendelea kufanya hivyo biashara na kurudisha mkopo. Kuna mambo kadhaa ya kuangalia:

1. Business model ya Precision Air (kama ipo!)
2. Mapato na matumizi (at least kwa miaka 3 iliyopita)
3. Dalili za kampuni kuishiwa hela zilianza lini? (wakiangalia kwenye mahesabu watagundua hilo)
4. Ni lini mara ya mwisho kwa Board of Directors kulipwa Dividends (hii ni muhimu sana maana upo uwezekano wa mkulima kula mbegu)
5. Uwezo wa management
6. Kubwa zaidi, serikali - kwa niaba ya walipa kodi wa Tanzania, wanatakiwa wajiridhishe kuwa kweli Tsh 51 bilioni zitatua matatizo ya Precision Air. Kama matatizo ya PrecisionAir yatagharimu zaidi ya hiyo Tsh 51 bilioni, je, nani mwingine anachangia hicho kiasi? Na kama Tsh 51 bilioni zinatosha, je, Precisio Air wao watachangia kiasi gani? Lakini pia ulipaji wa mishahara hasa kwa mabosi waliofikisha hiyo kampuni kibla, utabakia pale pale au utapunguzwa?

Kwa mtazamo wangu, Precision Air wanahitaji zaidi ya Tshs 51 ili watoke kwenye tope walilomo. Na ningekuwa na maamuzi ya mwisho kwenye hili, nisingewapa Precision Air hata senti moja kwa sababu hawana uwezo kwa kuhimili ushindani na wala hawaelekei kuwa na mikakati mizuri ya kibishara. Their business model is fundamentally flawed, na hela wanazoomba hazitasadia chochote kama hawakufumua shirika zima.

Precision Air amekuwa na monopoly kwa miaka mingi sana, lakini ukuaji wake umekuwa ni wa kimagumashi. Wamekuwa wanafanya biashara kwa utashi wa kisiasa zaidi na ndio maana wanakuja na huu upuuzi wa kujiita 'national carier'. Na huu utashi wao wa kisiasa ndio wamekuwa wanatumia kuweka mizengwe ili kusiwepo na ushindani. Fastjest wamekuwa na wahanga wa hawa watu. Badala kukaa chini na kuandaa mikakati mizuri ya kibishara, Precision Air wamekuwa busy wanapiga umbea ili kusiwepo na ushindani, na wakati huo huo wanaendelea kula Dividends utadhani shirika ni zima! Air Tanzania imekufa hawakuweza kutumia fursa hiyo adimu ipasavyo. Sasa Shirima anamlalamikia mkurugenzi aliyeondoka? Ina maana muda wote huo Baord haikuona chochote?

Serikali ya Tanzania, na watanzania wenyewe hatapoteza chochote kwa Precision Air kufa. Let me them die. Kama wamevurunda fursa waliyokuwa nayo (monopoly) kwa miaka yote hiyo, hawawezi kufanya la maana with just Tshs 51 billion. Hizi hela wanazoomba kwangu mimi ni kama watazitumia kununua vile vibiscuti vya Azam wanavyowapa abiria kwenye ndege zao. Haziwezi kutatua matatizo ya hili Shirika hata chembe, na muda si mrefu watarudi tena kuomba billioni nyingine kadhaa kwa wimbo ule ule wa 'national carier!

Kama serikali wataona ugumu wa kuwaambia NO, basi watoe fedha kwa masharti yafuatayo kwa kipindi chote ambacho serikali itakuwa inachukua makato ya hii bailout:

1. Board yote iliyofikisha kampuni kitanzini ikae pembeni
2. Iundwe management ya mpito (interim management)
3. Waandae upya business model, na iwe ya kiuhalisia tofauti na sasa wanafanya mambo kisiasa. Huu wimbo wa kuwa 'national carier' should stay where it belongs -dustbin.
4. Hakuna kulipana dividends hadi serikali ipate fedha yote itakayotolewa (51 bilioni).
 
It will be a crazy decision for the government to inject capital to ATCL, we are not that rich to throw away taxpayers money to a business which is certain not going to survive, I am telling you, in five years to come, KQ will be following on its knees.

Inaelekea huifahamu vizuri ATCL; tatizo lake ni kwamba hawa hawa wenye Precision ndio waliokuwa wanawatumia watu wao walioko serikalini kuiua ili PC ibakiwe na monopoly!! Huwezi amin,i kwani walikuwa na watu wao makao makuu ya wizara ya uchukuzi na hazina ambako walihakikisha kuwa maamuzi mengi ya kuhusu kuiwezesha ATCL yalikuwa yanacheleweshwa na hivyo kuiathiri kampuni, hata hizo fedha walizokuwa wanaipa zilikuwa zinatolewa kwa mafungu ambayo yasingewezesha Airline kufanya vizuri!!! Mramba na masalia yake were responsible for all the intrigues. Atcl ikiwa well capitalized itasaidia sana usafiri wa ndani!!
 
Tatizo lao kubwa ni kutokuwa makini katika uwekezaji wao na kiwango cha ukuwaji ambao haukuzingatia uwezo wa kampuni.

Mkuu,..sasa hao wanaopewa hizo TZS 51 bilion si ndio hao hao walioshindwa ku-manage resources za kampuni yao? Tutegemee nini kuhusu urejeshwaji wa hizo fedha?
 
Waingereza wanamsemo kuwa IF YOU CANNOT STAND THE HEAT DO NOT STAY IN THE KITCHEN; sasa kama precison wameshindwa kazi ya usafiri wa ndege wawaachie wale wanaoweza, kama vile kwenye biashara ya usafiri wa mabasi SCANDINAVIA na sasa SUMRY wamefilisika wamewaachia wengine wanaendeleza libeneke la usafiri wa mabasi nchini, wala hawakuomba msaada kutoka serikalini!!! Sasa kama umuhimu ni usafiri basi serikali ingeonesha njia kwa kuzibail out hizi kamapuni za mabasi zilizofilisika pia. The government should be consistent in its decision making in order to have a modicum of credibility!!!
 
Same reason - Precision Air leo ikifa tutakuwa hatuna Shirika la Ndege kabisa! Kwa hiyo impact yake ni kubwa kwenye sekta hiyo. Kuhusu ATCL sijui kwa nini, lakini nafikiri haikuhitaji bail out kwani ilikuwa inapata pesa toka Serkalini wakati wote. Swali litakalobaki ni ikiwa pesa walizokuwa wanapewa zilitosha na kusimamiwa vizuri.

Sasa mkuu,

Kwani fast jet si wapo hapa? Tena umesikia wanaexpand operations zao kwa kuwa na new destinations kuelekea nje ya nchi. This is exactly what Precision was doing. Unamaanisha nini unaposema tutakuwa hatuna shirika la ndege kabisa?
 
Nchi hii ina wenyewe, na wenyewe ndio wala nchi wenyewe.
Hata wasipo ipa PW hela, watazipeleka kwa mademu zao na nyumba ndogo zao
 
Precision+airplane.jpg


I happened to be going through a front page news item on the citizen today. This was on nothing other than the Government of Tanzania’s seemingly intent to bail-out Precision Air Services Limited, a DSE listed company, currently in a god-knows-how-we-got-here sort of financial turmoil. According to Citizen, the bailout is expected to be of approximately TZS 51 billion, yes, tax payer’s money.

I should say I completely believe that this, if it happens, will have been another case of absolute misuse of public funds. There are several reasons to this.

First, in its current operations, Precision is almost completely falling short of its current immediate competitors fast jet, whose coming has meant sleepless nights to Precision. I am yet to see precision come up with its own business survival strategy. Since the coming of fast jet, it has all been a down-hill-fall for PW.

What does one call a stock-listed company that could not resist even one year of competition in a market that it had solely controlled since forever? I remember 2011 when I would cautiously encourage prospective investors to buy precision air stocks only because it had been a monopoly in local flight destinations. I realized that such would not necessarily be the case if a strong competition arose.

Secondly, and even more importantly, in a very strange way, Precision seems to be lacking a knowledgeable board of directors. It is shames to have had the company’s Chairman of the board, Mr. Michael Shirima admittedly say that the board has been irresponsible for the company’s failure.

precision-air-staff-295x295.png



I fail to know which board will now be managing the bail-out funds from the Government. In his interview with the Citizen, Mr. Shirima, blamed the former CEO of the Company, Mr. Kioko of leading the company to its current state of affairs.

“He (Kioko) deserves credit for steering the airline during a long transition period, but he had some weaknesses which are to blame for the problems we are now encountering” Mr. Shirima said. He cited as an example the ambitious plan that saw the airline lease three Boeing 737 jets to fly to new destinations in Africa, adding that the decision did not take into account the risks involved
.

Well, here I am, thinking, could the CEO have taken the business expansion decisions on his own? Did the members of the board review the proposed plans before approval? Is it the same board that is going to sit and approve how the TZS 51 billion, Tanzania tax payers’ money will be utilized too? I see a bubble growing.

This case reminds me of what happened in 2005 when a shadowy company going by the name of Tan Power Resources limited managed to undertake a number of Government-guaranteed deals which ultimately ended up being a loss to the nation.

Tan Power Resources Limited, having managed to have the whole of Kiwira Coal & Power Limited (KCPL) sold to it by the Government of Tanzania for a tiny TZS 700 million, went on to acquire from CRDB, PSPF and NSSF, Government-guaranteed loans amounting to $ 15m (including accrued interests only up to year 2008).

As those who had visited the mine site since its privatization will tell you, there has never been a capital investment done on the mine, even though such huge sums were summoned by Tan Power Resources Management. Strange? That is how smart people rob a nation. A friend of mine once said, the best way to rob a bank is to actually own it.
hatuna shirika la ndege kubwa zaidi ya hili...kwa hiyo ni sahihi kabisa
 
Kuna mambo mengine ukiyasikia yanakutia hasira kiasi kwamba unatamani uwakute hao viongozi wanaoidhinisha huu upuuzi, uwasambaratishe kwa bakora huku matusi yakikutoka mfululizo!

Yaani tumefikia hatua hii kwamba Viongozi hawaogopi wala hawaheshimu walipa kodi kwa kiasi hiki! And nobody senior to them bothers to intervene this. Halafu ukiwasema wanakuambia wewe ni mchochezi, ni mpinzani kutoka CHADEMA, na hata kesi ya ugaidi wanakupikia.
Kwani ndo mara ya kwanza kufanya hivo? Mbona serikali ilishatoa billion kadhaa kuwafidia wanunuzi wa pamba waliojifanya kupata hasara kutokana na economic recession ilhali ikiwaacha patupu wakulima wenyewe?
 
Back
Top Bottom