Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 707
Tatizo katika uwekazaji wao ni lipi? Busines driver kubwa ni soko (wateja). Kama huna uhakika wa kupata wateja (yaani kuongeza market share) unawekeza ili iewje? Ndiyo kosa lenyewe hilo. Kununua au kukodisha madege mengi kabla hujalisoma soko na nyakati vizuri. Kwa vile PW ni public company (i.e quoted on DSE) kwa nini wasitafute market na business solutions kama ku-down size, ku-retrench staff, kufukuza management committe na board, n.k. badala ya kukimbilia kuchota pesa za walipa kodi? Na serikali ina uhakika gani kuwa pesa hizo zitarudi? Nakumbuka walipo-float share zao DSE mwitikio haukuwa mzuri. The IPO was undersubscribed. That shoudl have told them how investors feel about them and their prospects. But did they have the sense to see the signs? May be Kioko new what he was doing all along.Kwenye mfumo wa kibepari tuliokubali, bailout kwa kampuni binafsi na pesa za umma siyo dhambi ili mradi tu kuwe na sababu na masharti mahsusi ya kuzirejesha pesa hizo.
Wakongwe wa mfumo huu (Marekani) wanayafanya haya. Huko Marekani kwenye usafiri wa anga hakuna shirika hata moja ambalo linamilikiwa au Serikali ina hisa hata moja, lakini kila yakiingia kwenye matatizo (ambayo ni ya kawaida katika biashara hii) usaidiwa - ikiwemo kwa kutumia mfumo wao wa kuwekwa chini ya uangalizi maalumu (Chapter 11).
Maoni ya mtoa mada mengine ni sahihi lakini si kweli kuwa matatizo ya Precision Air yanatokana na ushindani na hasa kutoka kwa FastJet. Kwa wale walioko katika sekta hii watakueleza kuwa wateja wengi wa FastJet siyo wale waliokuwa wateja wa Precision air. Kiukweli idadi ya wateja wake haijateteleka.
Tatizo lao kubwa ni kutokuwa makini katika uwekezaji wao na kiwango cha ukuwaji ambao haukuzingatia uwezo wa kampuni.