Je, Naweza kuishi Dar kwa mshahara wa laki tatu?

Tafadhali Husika na kichwa Cha Uzi Huu.

Mimi ni Job seeker, nimepata kibarua Cha laki tatu Dar es Salaam. Sijawahi kufika Dar ila nasikia maisha ya huko ni Magumu kwa sababu ya bei ya vyakula, Pango na Usafiri. Naomba kuuliza, kwa kiasi hicho tajwa, nitamudu maisha ya Dar?!

Ahsante.
Kumudu inategemea unaishi eneo gani! Kwa kinondoni hutaweza ila kwa Ilala walau unaweza na kwa Temeke ndio uhakika kabisa😅
 
Utaishi tena maisha ya amani sanaaa, kuliko hata mwenye take home ya zaidi ya 5k aloko dsm

nakutabiria utatoboa maisha hadi utakuja kutuelimishaaa

pia anzisha kabiashara ka kuuza karanga apo utakapoishi na nyingine peleka ofisini wauzie wenzioo ... kg = 3500 (brand nzurii) ukifunga kwa mifuko na kuongeza thamani kwenye kg 1 utapata faida ya buku 2.

2000*21 (siku za kazi) = 40,000 --- hiii inakutosha matumizi madogomadogo

hahaaaa welcome bongo landiii
Kuna kale ka msemo kuwa biashara zote zinalipa ila tu ukiwa unasimuliwa. Kafanye sasa
 
Apate 300,000 na saving iwe 270,000!! Matumizi kwa mwezi 30,000 meaning
  • Hali dinner assuming anapewa chakula kazini
  • Hanywi maji
  • Hanunui sabuni
  • Hanunui mafuta ya kujipaka
  • Hanunui vocha ya simu
  • Hanunui mshumaa
  • Nauli
Analeta usanii
 
Hahahahah noma baab uliuza sana utu for a living?
Acha tu mkuu, nilikuwa sijui stress maana yake ni nini. Ushauri wa wengi ulikuwa toka kwenye hiyo nyumba kapange chumba cha elfu hamsini kwanza ili ujipange. Fikiria kutoa vitu vyako kwenye nyumba ya laki tatu ambavyo ni vyingi unde kuvipanga kwenye chumba cha 50, haya maisha haya
 
Back
Top Bottom