Je, Mungu yupo au hayupo?

Je, Mungu yupo au hayupo?

Powell Gonzalez

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2023
Posts
1,554
Reaction score
2,717
Njoo hapa unithibitishie kuwa mungu hayupo kwa hoja zako nami nitazijibu kishupavu. Ila kwanza pitia haya maelezo machacge hapa chini. Soma ikiwa tu una uelewa kidogo kuhusu quantum physics, ikiwa Huna uelewa basi pita huu uzi uache, kasome kwanza quantum physics, kisha rudi siku nyingine, maana utaleta haja za kitoto.

Watu wengi leo wanaosema mungu hayupo wanatumia hoja za kisayansi ambazo nyingi zimebase kwenye quantum physics, hapa utakutana na relativity theory ya Einstein, special and general theory of relativity.


Binadam wanataka wanataka kumjudge Mungu kwa kutumia laws za universe, yaani gravity, time, quantum fields, au thermodynamics.

Lakini swali la kwanza la kujiuliza ni hili:

Hizo laws zipo ndani ya nini?
Sayansi inabase kwenye Matter, Energy,Space, Time.
Lakini classical definition ya Mungu ni:
" The cause of space, time, matter, and energy" Mungu ndiye kaumba kila kitu, kaumba space, time, matter and energy.

Kwahiyo logically:
Kama Mungu ndiye chanzo cha space na time, huwezi kumpima kwa tools zinazotegemea space na time.

Ni sawa na kutumia thermometer kupima muda.😅

Tunazo laws na principles kwenye quantum physics ambazo haziwezi kuvunjwa, I agree with that.
Lakini...?
Why is the universe mathematically structured?
Kwa nini ina obey consistent laws?
That itself is mysterious.

Kuna deep rational structure nyuma ya reality.
Quantum Physics haimuondoi Mungu
Quantum mechanics inaonyesha:
-Reality at small scales is probabilistic
-Particles behave like waves
-Observer effect exists
-Vacuum is not empty — it has quantum fluctuations.

Kwa kutumia Quantum Physics pamoja na theology, naweza kujibu maswali haya kutoka kwa Atheists wote ambao wanaamini sayansi na wanaamini, there's no God.

👆🏼👉🏿MUNGU ALIKUWA WAPI KABLA HAJAUMBA ULIMWENGU, NA YUPO WAPI KWA SASA?
Hapa nitumie English kidogo, to say "where was God before" ni swali ambalo Halina maana, kwa sababu: "where" (wapi) haikuwepo kabla dunia (space) kuwepo, kwa hivyo mungu ndio chanzo cha hiyo 'where" kwa sababu ''where" inakuwepo baada ya space, sasa kabla mungu hajaumba "space" vipi utumie where kumpima mungu?
The same to "when" and "before" which only existed after God created Time.
MUNGU HAPIMWI KWA "WHERE" wala 'WHEN" KWA SABABU AMEIUMBA MWENYEWE.
Hata science inasema mwanzo wa dunia ni Big Bang – Mwanzo wa Space na Time.
Modern cosmology says:
Space and time began at Big Bang
Before that, “before” and "where" doesn’t even make sense physically

Stephen Hawking alisema:
" Asking what was before the Big Bang is like asking what is south of the South Pole"
Exactly.

Kama space-time ilianza, basi cause yake haiwezi kuwa ndani ya space-time, kwahiyo science kupitia quantum physics inasema;
Source of time, energy and space lazima iwe:

1.Timeless
2.Non-material
3.Beyond physics laws(it can break all physical laws of universe and space)

Hicho ndicho classical description ya Mungu.

Mungu si “Object ndani ya universe”
Watu wengi wanamfikiria Mungu kama:

1.Kiumbe kikubwa sana
2.Kinaishi somewhere
3.Kina shape
4. Kilianza siku fulani
Damnnn...wtf?

Huwezi kumuona mungu kwa sababu hajaumbwa atoms kama wewe na other material things.
Unatumia mwanga( light) kuona lakini light was created by God himself, so how can it be used to watch him?
Huwezi kumuona kw kutumia Telescope inayotumia physical photons.

Mungu hagusiki, ni Timeless, space-less, when-less, material-less.
Kiufupi utabaki kuamini mungu hayupo ikiwa utatumia vitu vilivyopo ndani ya universe kumpima, hivi vitu ameviumba mwenyewe kwa hivyo haviwezi kutumika kumpima kama wewe unavyompima rafiki yako, Juma...
Juma anaishi mwanza...
Juma Alizaliwa 2002...
Juma Ana uzito wa 68kg...
Juma yule pale...
Juma alikuwa hapa....
Soma tena.

PRAISE THE LORD!!!!

Uliza chochote....
 
Wanaosema mungu yupo ndio wanaopaswa kuthibitisha, wanaosema hayupo(wakanushaji) hawana wajibu wa kuthibitisha.

Onus probandi incumbit ei qui dicit, non ei qui negat.
 
Hawapaswi na hakuna ulazima huo.
Kama bado haijulikani au hujui chanzo cha Ulimwengu au hujui jambo lolote hakuna tatizo na wala sio dhambi kusema HUJUI.
Kwamba ukipewa karatasi ujibu kwanini unapinga uwepo wa Mungu utashindwa kuandika chochote mkuu
 
Kwamba ukipewa karatasi ujibu kwanini unapinga uwepo wa Mungu utashindwa kuandika chochote mkuu
Swali la kwa nini mtu anapinga uwepo wa mungu ni tofauti na swali la uthibitisho wa kutokuwepo mungu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom