Mimi sio msomi sana, sielewi quantum physics lakini;
Ninaposema siamini kwenye uwepo wa Mungu, simaanishi kwamba najua chanzo cha ulimwengu. Kwa kweli sijui.
Siamini kwenye hii miungu iliyotungwa na wanadamu(Yahweh, Allah nk.) kwasababu kuna mikinzano mikubwa kwenye maelezo yao.
Vile vile, sidhani kama dhana ya uungu ina maana moja kote duniani. Kila mtu anamtafsiri Mungu kulingana na tamaduni zake na mapito yake.
Kwahiyo je, ulimwengu una muumbaji? Labda. Na sijui kama atakuwa na sifa za uungu zilizoandikwa kwenye vitabu.
Tunatumia neno
"atheist" kwasababu limezoeleka zaidi ila kuna aina nyingi za kutokuamini. Kuna
"agnostics",
"ignostics" na wengine wamechanganya vyote. Labda
Kiranga ataweza kufafanua zaidi hapa, mimi sielewi elewi... Ila zingatia hili mkuu.