Je, Mungu ni muweza wa yote?

Mto Songwe

JF-Expert Member
Jul 17, 2023
6,017
12,306
Je, Mungu ni muweza wa yote?

Kama jibu ni ndiyo, basi tukubali mema na mabaya yote yake, yote mema na mabaya yanayo endelea ulimwenguni kote yeye ndio muhusika.

Ukiona unamchagulia yapi anafanya na yapi hafanyi kwa kutazama mazuri na mabaya basi tambua huyo Mungu sio muweza wa yote bali wa machache tena yale tu yanayo kufurahisha.
 
🤣🤣🤣
Kwahyo umeamishia Mada huku HOJA MBALIMBALI..
Umeitoa Jamii intelligence 🤣🤣
Ngoja nimuite mwenzangu Kiranga ..

Unatakiwa kwanza utupe Definition ya Mungu kazi zake na uwezo wke ndo tuchangie
😃😃 Huu ni mjadala huru mkuu walengwa watakuja tu hapa kutetea imani zao mimi ni host tu.

Kiranga atapambana nao 😃
 
Mungu ametengeneza Universe na vilivyopo, akavipa mipaka (guidelines) ya utendaji wake. Akavipa akili ili viweze kujiendesha na kufanya maamuzi vyenyewe.

Ninacho maanisha ni kuwa, hapa Duniani tupo kwenye mtihani; na kwa bahati nzuri mtihani wenyewe tumepewa na majibu (marking scheme); Ukitaka kupata majibu ya mtihani tuliopewa hapa Duniani, pitia Quran & Biblia. Kama huamini kuwa upo kwenye mtihani tena wa muda mfupi (miaka 60 - 100) Subiri siku ya malipo (day of judgement!) ndio utajua hujui...
 
Mungu ametengeneza Universe na vilivyopo, akavipa mipaka (guidelines) ya undendaji wake.
Akavipa akili ili viweze kujiendesha na kufanya maamuzi vyenyewe
Ninacho maanisha ni kuwa, hapa Duniani tupo kwenye mtihani; na kwa bahati nzuri mtihani wenyewe tumepewa na majibu (marking scheme); Ukitaka kupata majibu ya mtihani tuliopewa hapa Duniani, pitia Quran & Biblia. Kama huamini kuwa upo kwenye mtihani tena wa muda mfupi (miaka 60 - 100) Subiri siku ya malipo (day of judgement!) ndio utajua hujui.....
Tutimize wajibu wetu
Tumpende Mungu na wanadamu wenzetu
 
Ukiona unamchagulia yapi anafanya na yapi hafanyi kwa kutazama mazuri na mabaya basi tambua huyo Mungu sio muweza wa yote bali wa machache tena yale tu yanayo kufurahisha.
Mkuu, kwa nini umesema hivyo? Je, umefikiri kwa kina na mawanda yote kuhusu hii mantiki yako?

Hakika kamanda ili swali huwa linanifanya nisiende kanisani
Sasa iwapo hutaki kwenda huko yanakopatikania majibu, utaokokaje?

Unashindwaje mtihani hivyo hata kabla ya kuanza kuufanya?

Ninacho maanisha ni kuwa, hapa Duniani tupo kwenye mtihani
Mtihani huo ni matokeo ya Adamu na Hawa kushindwa mtihani wa awali alioagizwa asile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

Ukifeli mtihani wa Mungu, anakupa mtihani mwingine wa SUP (ambao kimsingi huwa mgumu na tekniko kidogo kuliko ule wa awali!)

Kimaandiko hiyo inaitwa rehema ya Mungu. Kila mtu amepewa nafasi ya pili.

Ikiwa mwanadamu ataichezea hiyo nafasi, basi kwa jinsi hiyo anakuwa amethibitisha kutofaa kwake kuishi maisha yanayolingana na maisha ya Mungu Mwenyewe--umilele.

Uajabu mwingine wa Mungu ni uwezo Wake wa kutupatia sie wadhambi rehema na haki kwa wakati mmoja.

Haki ya mdhambi ni kufa milele (mshahara wa dhambi), ilhali rehema ya Mungu ni uzima wa milele kwa wale wamwaminio.

Ili kubalansi mlinganyo huo wa kiungu, ndiposa kigezi (factor) cha Yesu Kristu kinaingia hapo kati ya haki ya Mungu na rehema Yake.

Pasipo kifo cha Yesu Kristu Bwana wetu msalabani Kalvari, sie ni wapotevu tusiokuwa na tumaini.

^Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kutuletea Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye Kristu Yesu asipotee bali awe na uzima wa milele.^ ~ Yohana 3:16
 
Je, Mungu ni muweza wa yote ?

Kama jibu ni ndiyo.

Basi tukubali mema na mabaya yote yake, yote mema na mabaya yanayo endelea ulimwenguni kote yeye ndio muhusika.

Ukiona unamchagulia yapi anafanya na yapi hafanyi kwa kutazama mazuri na mabaya basi tambua huyo Mungu sio muweza wa yote bali wa machache tena yale tu yanayo kufurahisha.
Mbaya zaidi kuna mchizi kafa kaadhibiwa kwajili ya wanadamu. wao wanaamini hivyo alafu cha ajabu bado wanaenda kuabudu wakati tayari wamekombolewa.

Mimi nikila bangi naiona Pepo yangu karibu Sana.
 
Je, Mungu ni muweza wa yote ?

Kama jibu ni ndiyo.

Basi tukubali mema na mabaya yote yake, yote mema na mabaya yanayo endelea ulimwenguni kote yeye ndio muhusika.

Ukiona unamchagulia yapi anafanya na yapi hafanyi kwa kutazama mazuri na mabaya basi tambua huyo Mungu sio muweza wa yote bali wa machache tena yale tu yanayo kufurahisha.
Kasi ya kumuandama Mungu inaongezeka kila leo
 
🤣🤣🤣
Kwahyo umeamishia Mada huku HOJA MBALIMBALI..
Umeitoa Jamii intelligence 🤣🤣
Ngoja nimuite mwenzangu Kiranga ..

Unatakiwa kwanza utupe Definition ya Mungu kazi zake na uwezo wke ndo tuchangie
Wameufuta ule uzi?
Narudu na refresh hola. Mbona hakukuwa na baya zaidi ya majadiliano🤔🤔
 
Je, Mungu ni muweza wa yote?

Kama jibu ni ndiyo, basi tukubali mema na mabaya yote yake, yote mema na mabaya yanayo endelea ulimwenguni kote yeye ndio muhusika.

Ukiona unamchagulia yapi anafanya na yapi hafanyi kwa kutazama mazuri na mabaya basi tambua huyo Mungu sio muweza wa yote bali wa machache tena yale tu yanayo kufurahisha.
Mungu alituumba tusijue jema na baya. tukaasi agizo lake tukala mti wa ujuzi wa mema na mabaya, ndio maana unateseka sasa. Yeye alitaka tuishi rohoni asilimia 100, ila tukaanguka, sasa tunaishi nafsini na mwilini, ndio maana ni tabu tupu. Ashukuriwe Mungu, Baba yetu aliyemtoa Mwanawe pekee Yesu, afe msalabani ili kupitia Yeye tupate UKOMBOZI na wokovu, kisha uzima wa milele.


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
nishalinena hili kitambo sana ila wale jamaa ni vichwa ngumu!,kuamini hizi dini zilizopo ni ugomjwa wa akili mmoja mbaya sana!.

mantiki ya Mungu kuweza kila kitu nakuumba kila kitu inaleta mkanganyiko sana tena sana!... na isitoshe wanasema yeye ndio chanzo cha kila kitu na hapohapo wanamsema shetani ndio chanzo cha mabaya!!..
so sifa ya ubaya shetani aliitoa kwanani ikiwa Mungu ndie chanzo cha kila kitu..?
kama ubaya haukutoka kwa Mungu basi Mungu sie chanzo cha kila kitu inamaana kuna vitu vinatokea hajui vimetokea wapi!,hivyo inapinga sifa yake ya Umungu kuwa yeye ndie chanzo cha kila kitu!.

pili sifa yake ya uumbaji na uweza wa kila kitu inakuja kuleta tafrani ikiweka ile mantiki ya kuumba kitu anachoweza kukibeba na vilevile asiweze pia!.
hivyo vitabu vya dini ni ulaghai kabisa hamna kitu mule na ndio maana kila siku watu wanaomba na shida ziko palepale!,nani hataki raha..?
unafikiri nani anapenda magonjwa..?
kama huyo Mungu angekuwa anatatua shida zetu kuna mtu asingemuabudu..?
yani aniponye magonjwa,anipe mahitaji yangu yote,afya,ulinzi,chakula na uhakika wa maisha ya milele huko peponi baadae. halafu nisimuabudu basi nitakuwa zwazwa la mwisho..😂

lakini kwa staili hii anayoenda najua kabisa hakuna Mungu wa namna yake labda yupo wa tofauti ambae hata hakuamua kijitapa kama huyo wa kwenye vitabu,ye alitenda kazi yake akamaliza akaendelea na mishe nyengine..😂😅
 
Mungu alituumba tusijue jema na baya. tukaasi agizo lake tukala mti wa ujuzi wa jema na baya, ndio maana unateseka sasa. Yeye alitaka tuishi rohoni asilimia 100, ila tukaanguka sasa tunaishi nafsini na mwilini, ndio maana ni tabu tupu. Ashukuriwe Mungu, Baba yetu aliyemtoa Mwanawe pekee afe msalabani ili kupitia Yeye tupate UKOMBOZI na wokovu, kisha uzima wa milele.


JESUS IS LORD&SAVIOR
hivi unafikiria kupitia ubongo gani ndugu yangu..!?
kama unaona ulichoandika kipo sawa hongera sana ndugu ila si bure nyie watu mlioshikwa na hizi dini kuna ubongo mwengine mnautumia si huu ubongo wa binadamu!🤣
 
images (11).jpeg
 
Back
Top Bottom