Balqior
JF-Expert Member
- Jun 8, 2021
- 1,709
- 5,697
Habarini wadau,
Binafsi naamini Mungu yupo, ni mwema, ndo aliumba vyote, anajua vyote past present and future, na ni muweza wa vyote, hakuna alie zaidi yake.
Uislamu na ukristo unafundisha kuwa mwisho wa sisi wenye dhambi ni kwenye moto wa milele, sasa mimi najiuliza.
1)Mungu akituchoma sisi kwenye moto wa milele, ataongezeka nini, na kufaidiwa nini? Asipotuchoma atapungukiwa nini?
2)Mungu atavumiliaje kuona sisi binadamu tukiwa kwenye maumivu ya kuchomeka milele na milele? ikiwa mimi mwenye dhambi siwezi vumilia kuona adui yangu akiteseka kwa mda mrefu sana?
3)Asingetuumba kuna mtu angemuuliza kwanini hajatuumba wakati yeye ni muweza wa yote?
4)Mahubiri, na vitabu vya Mungu, na shuhuda za mbinguni walipo watenda mema, na kuzimu wanakoteseka waliokufa kwenye dhambi, vikituambia sisi tulio hai kuhusu moto wa milele, ili tuache dhambi tuokolewe, je tukiwa wacha Mungu, uhusiano wetu sisi binadamu na Mungu utakuwa ni wa kweli unaotoka moyoni? au ni uhusiano utakaozaliwa kutokana na hofu, yani unamtumikia Mungu ili usiende motoni, ingawa kiuhalisia adhabu ya moto isingekuepo, ungeendelea kufurahia dhambi na kuacha kusali.
Sina nia ya kukufuru ila nimejaribu kuwaza tu, nipate ufahamu kwenye mambo haya , fundisho kuhusu adhabu ya kuchomeka kwenye moto wa milele, wakati umefanya dhambi ndani ya miaka 75, linanipa wasiwasi kuhusu asili na tabia ya huyu Muumba wetu kwakweli. Nahisi hio adhabu ni too much kuliko makosa yaliyofanyika. Kwenye vitabu vya dini Quran na biblia, malaika wa mbinguni wanakiri hukumu za Mungu ni za haki na kweli, labda kuna vitu ambavyo sivijui.