Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Hivi wewe brother Kiranga umefanya kitu gani hapa duniani hasa.hasa mkoani kwako tu au nyumbani kwako cha kuishangaza familia,majirani na ndugu zako hadi ufikie hatua utake uthibitisho wa Mungu alipo!!
 
Mkuu nashukuru kwa majibu yako na nimeelewa sana,ila nataka nikuulize maswali yanahusu meditation

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante,je nikitaka kuanza meditation ni vitu gani natakiwa niachane navyo ili niweze kufanikisha hilo zoezi?
Je nikweli huwa inaongeza nguvu za kiroho kama kuja kufanya miujiza mfano kuponesha wagonjwa?
3je kuna uwezekano wa kuingiwa na mapepo kama wadau wengine wanvyosema?
huwezi kurukwa na akili ukawa chizi?
Kuna uwezekano wa kufa wakati wa meditation? niliskia kuna viumbe unaweza ukakutana navyo vikanga'ngania roho yako ukapotea hukohuko.tuanze na hayo kwanza nisikuchoshe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekusoma lakini ingelipendeza zaidi kama ingelikua private au inbox zaidi. Any way kwa kuwa umeniuliza nitakujibu.

Ni Meditation gani unataka kufanya, Spirutual au Hizi kwa ajili ya mazoezi ya akili. Kama ni spiritusl or PATH inhitaji;

1. Guidance na preparation, hivyo tafuta group la watu wanaofanya meditation, watakupa mongozo. Lakini kifupi na mazoezi ya maandali na changing of life style. Including kutokula chakula fulani, kuacha ulabu, kuipenda kwa dhati.

2. POWER: Hutokea kwa wachache kuamsha uwezo na vipaji vilivyojificha kwa kuwa na uwezo kuwa na contacts na higher level of consciousness. Lakini yeyote atake ku guide through your path, atakushauri usizipractize, kwani zitzkuletea majivuno, EGO. Ni kitu kimoja hakitaki kabisa kitakacho kuletea kikwazo sana kufika mwisho wa njia yako ya ukamilifu.

3. Pepo ni Roho iliyokosa mwili, Meditation inakujengea Roho yako kuwa will power kubwa (aura), kiasi kwamba hamna Roho itayowekupush around. Hii Aura ni kipimo cha nguvu ya knowldge or exeperience au wengine wznaita utakatifu, nadhani ukiona picha Yesu kwenye vitabu vya dini amezungukwa mwanga fulani ule mwanga ndio unaitwa Aura, kila mtu anao


Nitaishia hapo kasijajibu maswali yote nitaendelea another time.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana, nadhani tuendelee private.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uwezekano wa kufa? Hapana. Watu wengi waliokufa sio kwa meditation, walikuwa wana practise zile power. Na hasa power moja ya kutoka nje ya mwili inaitwa Astray body projection, inamuwezesha muhusika kuona mambo yalifanyika huko nyuma. Kwenye group let tulikuwa na mtu wa namna aliweza tusimulia hata mapiramidi yalijegwaje lakini hakufa na alimaliza path yake. Labda kwa kuwa alifanys kwa manufaa sio kwa ubinafsi. By the way hivi unamua Bruce Lee, alikufa wakati akifanya Astray Body projection?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ndipo huwa nampenda Mungu

Na ninataman kufanana nae ,najua aliniumba kwa mfano wake,hivyo nikijibiidisha ntaweza.

Mungu sio kama mume anae muachisha kaz mke wake ,et ili asichepuke,au anae acha kumuhudumia na kumpendezesha mke na kumpa uhuru kwa kisingizio kuwa atachepuka

Ni mfano wa mume anae mpa vitu vyote mke wake na uhuru wote kabisa.

Anataka umpende na umuheshimu kwa sababu yeye ni Mungu,sio kwa sababu yoyote ile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana story nnzozikia kwamba wazungu walikuwa na wivu na zile movie ndo wakamuua lakin haikuniingia akilini.kwaiyo wewe ulifundishwa kabisa na wataalam?je unaweza kuwa mwalimu utoe ulichopata?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu sio Monopoly japo ana nguvu ,uweza na mamlaka ya kuwa monopoly

Nina assume unajua Faida na hasara za Monopoly economy na za opposite of it

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana story nnzozikia kwamba wazungu walikuwa na wivu na zile movie ndo wakamuua lakin haikuniingia akilini.kwaiyo wewe ulifundishwa kabisa na wataalam?je unaweza kuwa mwalimu utoe ulichopata?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nilipractice early 80's nimesha staafu, Uzuri wa Path ina mwanzo na mwisho, mimi nilichagua kustaafu public nafanya private. Ila ukitaka naweza kupa contact mbili tatu maana wengine ndio life yao.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siri zipo hapa gusa hapa Vatican Inamiliki Dunia - JamiiForums
 
1.Ikiwa kabla ya shetani kuasi hakukuwa na dhambi yoyote ile,tena alikuwa mbinguni kwenye utukufu wa MUNGU,Je shetani alishawishiwa au alitoa wapi mawazo ya uasi ikiwa hakukuwa na shetani yeyote mwingine?
*****************************

Inasemekana chanzo Cha Lucifer kumkosea BWANA MUNGU ni kuumbwa kwa Adam na Ever/Hawa.
Aligoma kumpa heshima Adam ambaye alikuwa ni mfano wa sura na utukufu wa Mungu.
MUNGU aliwaambia Malaika wamsujudie (hapa haimaanishi kumwabudu) Adam maana alikuwa mfano wa MUNGU.
Malaika Michael alianza yeye kutii agizo la MUNGU Kisha akawakusanya Malaika wengine ili watekeleze Hilo agizo.
Alipomwendea Lucifer,Lucifer akagoma kutii akisema haimpasi yeye kumsujudia Adam ambaye ni mdogo kuliko yeye ila inampasa Adam kumsujudia Lucifer maana Adam alikuta tayari Lucifer ameshaumbwa.Baadhi ya Malaika walimuunga mkono Lucifer nao wakagoma.
Hapo ndipo BWANA MUNGU akamlani shetani na hao Malaika wengine,akaamuru watupwe duniani.

Kwa maelezo hayo Ni dhahiri kwamba Chanzo Cha uasi wa Lucifer/shetani Ni uwepo wa Adam.
Pia shetani hakushawishiwa na MTU au kitu chochote kumkosea BWANA MUNGU.Ni kiburi chake tu ndio kilichomponza.
 

Kwanini sasa Mungu amemuumba huyo lucifer awe na kiburi kisha amuadhibu, wakati aliweza kumuumba akiwa hana hata chembe ya ukiburi (mnyenyekevu)?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini sasa Mungu amemuumba huyo lucifer awe na kiburi kisha amuadhibu, wakati aliweza kumuumba akiwa hana hata chembe ya ukiburi (mnyenyekevu)?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza kabiasa,Lucifer alikuwa mnyenyekevu sana kwa Mungu kabla ya kuumbwa Adam.
Pili,kiburi cha Lucifer hakijatokana na Mungu.Sio mpango wa Mungu Lucifer kumuasi.
Lucifer kutokutii agizo la Mungu ni utashi wake mwenyewe kama ilivyokuwa kwa Michael na wenzake walivyotumia utashi wao vizuri na kutii agizo la Mungu.Hapo Mungu hahusiki na hao malaika kutii au kutotii agizo lake.Wote wasingetii ingewagharimu na wote wangetii mambo yangekuwa shwari tu kama ilivyokuwa.
Lucifer hakutaka kujishusha kwa Adam maana aliona kuwa ni dharau kwa kuwa yeye ni mkubwa kuliko Adam.Malaika Michael alimsisitiza sana Lucifer kutii agizo maana matokeo ya kutotii ni mabaya.Lucifer hakutii na akasimamia hoja yake.Hapo Mungu anayaona yote hayo ila aliacha kila mmoja ajichagulie hatima yake.
Mwishowe Lucifer akakaidi kabisa na akapewa haki yake.Angetubu angeweza kusamehewa au kupunguziwa adhabu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbukumbu la torati 29:29
Mambo ya sirini ni ya Bwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ikiwa viumbe vyote vimeumbwa na mmoja, kipi kinachopelekea utashi wa kila kiumbe utofautiana na kiumbe mwenzie? Je Mungu wakati anamuumba lucifer hakujua kwamba kutokana na utashi aliokuwa nao lucifer atakuja kuhasi/ kwenda kinyume nae? Kama alijua, kulikuwa na ugumu gani kumrekebisha wakati anamuumba, ili huo utashi wake usichague kuhasi? Na kama alijua halafu kaacha hivyo hivyo inamaana Mungu amepanga hilo tukio lije kutokea kwa makusudi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Je,unatambua kuwa unatumia utashi ulionao kuuliza haya maswali uliyopost?Inawezekana kupitia haya Maswali una asi au vilevile unafanya vizuri.Lakini yote kwa yote unatumia utashi wako kufikiri na kuchambua Mambo mbalbali.Je,kosa La MUNGU ni kukupa wewe utashi au kosa ni wewe kwenda kinyume na maagizo yake ili baadae useme isingekuwa utashi aliokupa usingeasi?
Utashi una faida na hasara zake.Na MUNGU Hilo alilijua Sana tu.Hasara Ni kwamba,ukiutmia vibaya unakuwa huna thamani mbele ya MUNGU,na Hilo kosa si la MUNGU.Utashi Ni zawadi kubwa kwa wale wanaoutumia kwa kufuata amri za MUNGU.

MUNGU aliona kuwapa Malaika utashi Ni vyema machoni pake kwa maana unawawezesha kutekeleza maagizo yake kwa Uhuru bila ya kuwalazimisha.
Lucifer alitumia huo utashi kubishana na Michael kwenye swala la kumsujudia Adam.Michael alitumia jitihada zake zote kumshauri mwenzake asitumie utashi wake vibaya maana utamgharimu lakini hakutaka.Je kosa hapo Ni kupewa utashi au ni kutumia utashi vibaya?
Utashi ndio unatuwezesha kuamua kufuata au kutokufuata sheria za Mungu.Usipofuata kosa Ni lako Ni si la MUNGU.
 
Hadithi njoo utamu kolea....

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…