Je, Mungu ndiye aliyeumba dhambi?

Hebu nisaidie ni vp uliweza kujua kuwa hakuna Mungu?
 
Niliwahi kuwailiza wachungaji na mashekhe kuhusu maswala haya nilionekana kama muasi, na hawana majibu zaidi ya kukwambia Akili ya mwanadamun
inapoishia ndipo ya Mungu inapoanzia. Umeeleza na kudafanua vizuei kwa mytindo wa maswali. Thanks.
 
Sote tungejifunza kuwa Mungu si wakichezea. Na dhamhi tungeziepuka.
Yaani mtu anampiga risasi mwezake au anamchoma visu mwenzake au kwa mateso mengine yogote makali. Halafu unasema wewe ni Mungu na kwamba mtu huyo mwenye kumtesa na kunyanyasa wengine kwa makusudi kabisa akitubu uamsamehe?? Huyo Mungu ni wa ajabu sana.
 
Space haiumbwi. Labda nitumie neno lingine ni kwamba kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu, Mungu alikuwa anaishi kwenye sehemu iliyowazi/tupu (hakukuwa na chochote kile zaidi ya yeye mwenyewe tu)
Kwahiyo hapa unakubali kwamba kuna vitu Mungu hakuumba, kama vile space.

Na kama unakubali au kuamini kuwa space haiumbwi, kwanini usiamini au kukubali pia kuwa ulimwengu hauumbwi?

Na pia swali lingine, kwa kabla ya kuumba ulimwengu huu(ambao kitheologia unakadiriwa kuwa na umri wa miaka 6000 tangu kuumbwa kwa dunia mpaka sasa). Hapo kwenye space Mungu alikuwa anafanya nini kwa makarne na makarne?!
 
Hebu nisaidie ni vp uliweza kujua kuwa hakuna Mungu?
Mkuu Tz mbongo, kwa nilivyomuelewa huyo mdau ni kwamba, kadiri ya mahubiri na hadithi zinazomuhusu huyu Mungu, akizichanganua kimantiki, anagundua kuwa Mungu huyo hayupo. Hata mimi hapo namuunga mkono.

Binafsi ninaamini kuwa yawezekana Mungu ni kweli yupo ila si wa sifa hizi tunazohubiriwa na Abrahamic Religion (hasa ukristu na uislamu).

Ni vigumu sana kuamini kuwa Mungu huyu anaupendo mkuu usiomithirika ilihali watu wasiokuwa na hatia(mfano watoto wachanga) wanakufa kwa majanga ya asili kama vile tsunami nk.
 
Nitajie kinachokufanya uone kuwa inawezekana Mungu kuwa yupo? Unapinga sifa zinazoelezwa kumuelezea Mungu ila unadhani kuwa Mungu anaweza kuwepo,hebu nieleze ni yapi yenye kukufanya uone kuna uwezekano wa kuwepo Mungu?
 
Mkuu, imani ni kukubali ukweli wa jambo lisiloweza kuthibitika.
Rejea maana ya imani katika Wikipedia.

Kwahiyo, kwa ujumla kusema kwamba Mungu yupo au hayupo zote hizo ni imani kwa sababu hakuna anayeweza kuthibitisha.

Tatizo linakuja, wale waaminio kuwa Mungu yupo, wanapochanganua sifa za Mungu huyo, ndio hapo wanapoibuka watu na kusema logically Mungu wa sifa hizo hayupo. Kwa sababu sifa zile zinakuwa zikijichanganya kimantiki.

Ni sawa na mimi niseme, ninapenda kunywa kinywaji ambacho ni cha baridi sana (mpaka sentigrade -30), na wakati huo huo ni cha moto sana (mpaka sentigrade 100). Kwa kweli kinywaji hicho hakipo, hata kama hamjawahi kukiona!![emoji4]
 
Nitajie kinachokufanya uone kuwa inawezekana Mungu kuwa yupo? Unapinga sifa zinazoelezwa kumuelezea Mungu ila unadhani kuwa Mungu anaweza kuwepo,hebu nieleze ni yapi yenye kukufanya uone kuna uwezekano wa kuwepo Mungu?
Lakini pia yawezekana hayupo.

Tunapozungumzia uwezekano, maana yake ni kutokuwa na uhakika. Sina sababu hasa za kibinafsi zinazonifanya niamini au nisiamini kuwa Mungu yupo au hayupo. Kwa sababu sijui ukweli ni upi.

Lakini kwa nyie mnaosema kuwa yupo, na kuzitaja sifa zake ndipo hapo ninaposema kuwa wa sifa hizo mnazozitaja hayupo.
 
Hao watu tatizo lao lingekuwa ni sifa tu za Mungu ndio wanazopinga basi haya majadiliano yangepata hitimisho,ila kilichopo ni kwamba wao wanasema hakuna Mungu kabisa hivyo wao hawaamini kabisa Mungu wa aina yeyote yule,hizo hoja za kwamba maelezo ya kuhusu sifa za Mungu yanajipinga hutumia tu kutetea msimamo wao na si kwamba ndio sababu za wao kutukuamini Mungu.
 
Sasa mkuu mbona unajichanganya tu,wewe unasema inawezekana Mungu akawepo(huna uhakika) halafu hapohapo unasema huna sababu zilizokufanya uone huo uwezekano wa kuwepo Mungu!!!!!

Kama Mungu jinsi anavyoelezwa kumekufanya useme haiwezekani kuwepo,iweje tena uje kusema Mungu anawezakuwepo ila bila sababu ya kukufanya uone uwezekano huo?
 

Kila mtu ana uelewa wake kuhusu neno Mungu. Mungu maana yake ni kianzilishi/chanzo (source) cha ulimwengu kuwepo. Hata kisayansi huwezi kuambiwa ulimwengu umejitokeza bila kuwa na chanzo kama vile energy, n.k kwahiyo ile chanzo cha kutokea ndio inatumika neno Mungu kwa maana kilichosababisha/anzisha uwepo wa ulimwengu.

Swali lako la pili ni kwamba muda unaanza kuhesababika baada ya tukio na sio kabla ya tukio kwahiyo huwezi kusema kuwa imepita makarne na makarne wakati hakukuwa na hesabu yoyote ya muda. Inawezekana ikawa hata sekunde haikupita Mungu akaumba ulimwengu hapo hapo. Au mwenzangu unaweza kuniambia Mungu kakaa muda gani kisha ndio akaumba ulimwengu? Au ni karne ngapi zimepita ndipo akaumba ulimwengu?
 
Mkuu, mimi sijajichanganya sehemu yoyote. Kusema kwamba yawezekana mungu yupo, au yawezekana hayupo, huko si kujichanganya. Ila ni kuthibitisha jinsi gani sijui. Kwa kifupi mimi sijui kiuhakika kama Mungu yupo au hayupo.

Ila nyie ambao mnasema kwamba mna uhakika Mungu yupo ndio hapo tunahitaji mtuhakikishie au mtuthibitishie.

Mnaposema Mungu yupo na anaupendo mkuu kwa viumbe vyake, ilihali baadhi ya viumbe wake wasio na hatia wanaangamia kwa majanga ya asili yaliyo ndani ya uwezo wake kuyadhibiti, hapo ndio mnatuchanganya kabisa.

Mnaposema kaumba kila kitu kasoro space (rejea jibu la mmoja hapo juu), kumbe kuna vitu hajaumba, sasa ni nani kaumba space!? Bado mnatuvuruga!!

Tuthibitishieni na tuone kwamba Mungu ndio mwenye sifa hizo, ili wote tuamini kuwa yupo!!
 
Mkuu, unafahamu vizuri habari ya spacetime!?

Mi pia siifahamu kiundani lakini angalau inamaanisha kwamba space na time ni vitu pacha, vinaendana na havitenganishwi!!

Unapozungumzia space (ambayo kadiri ya jibu ni kuwa haijaumbwa) basi unazungumzia time(ambayo bila shaka nayo itakuwa haijaumbwa).

Sasa katika space hiyo, Mungu alikuwa anafanya nini kabla ya kuumba ulimwengu!?

Mungu mjuzi wa yote: inamaanisha alijua angetuumba, malaika wema wangemuasi na kuwa waovu, adam na hawa wangekula tunda na mwishowe hawa angempa adhabu ya kuzaa kwa uchungu na adam kuhangaishwa na maisha.

Anaweza vyote na anatupenda sana, Je hawezi umsamehe mara moja shetani na kumfanya kuwa mwema tena!?
 
Nafikiri wanamaanisha zaidi Mungu wa sifa hizo mnazozitaja. Kama kuna Mungu wa sifa nyingine basi awekwe ili sifa zake zidadavuliwe.

Kama naye hayupo, inamaana Mungu hayupo!!

Kama Mungu yupo ni Mungu gani!?

Kama Mungu ndio chanzo cha ulimwengu, je bado yupo!? (Chanzo hicho bado kipo). Maana ulimwengu ulianza muda mrefu umepita
 

Nimekuuliza swali je unaweza kunitajia huo muda ambao Mungu amekaa ni wiki, miezi, miaka, au ni karne ngapi zimepita ndipo akaumba ulimwengu? Au imepita kipindi za miaka mingapi ndipo ulimwengu ukajitokeza? Haiwezekani nikakutajia shughuli gani alikuwa anafanya pasipo wewe kunitaji muda.

La pili ni kwamba mimi nazungumzia uwepo wa Mungu, usichanganye kati ya uwepo wa Mungu na sifa/tabia ya Mungu. Mimi sipo kwenye kuzungumzia sifa na tabia za Mungu ambavyo hivyo vitu utavikuta kwenye vitabu vya dini. Mimi ninaamini uwepo wa Mungu kama kisababishi cha kuwepo kwa vitu vyote vilivyomo ulimwenguni. Mimi sio mwamini wa vilivyomo kwenye vitabu vya dini na ndio maana kuna maswali niliuliza post namba 184 na 186 kwa mmoja wa mtu anayeamini Mungu wa kwenye vitabu.
 
Mkuu asante kwa jibu lako fikirishi lakini naweza kujibu kama ifuatavyo:

La kwanza, kama kweli Mungu amekuwepo milele na milele maana yake kabla ya kuumba kitu chochote amekuwepo hapo kwenye space(kadiri ya mdau mmoja hapo juu, kuwa Mungu alikuwa kwenye space kabla ya kuumba chochote) kwa muda infinity(maana yake hana mwanzo). Sasa swali linakuja kwa wanaomuamini, katika Muda huu infinity, Mungu alikuwa anafanya nink hapo kwenye space peke yake? (Kumbuka hiyo ni kabla hajaumba chochote hata malaika)[emoji23]

La pili, mkuu hauwezi ukasema kuwa Mungu yupo pasi na kutanabaisha sifa zake. Yaani sifa ni kama identity ya uwepo wake, kwa mfano, wewe unaamini kuwa mungu ni chanzo cha vitu vyoote. Tayari hiyo ni sifa unayoamini anayo, na hapohapo swali linazuka, Je kama Mungu ni chanzo cha vyoote, je Mungu ni chanzo cha shetani, dhambi na uovu uliomo duniani!?
Nadhani utaona ni jinsi gani watu wanatumia sifa wampazo Mungu kupinga uwepo wake![emoji856]
 

Tatizo linakuja palepale haiwezekani kutaja shughuli gani aliyokuwa anafanya pasipo kupata muda halisi kabla ya kuumbwa vilivyomo ulimwenguni. Embu fikiria pengine labda kaumba vilivyomo ulimwengu baada ya sekunde moja tu au baada ya dakika moja tu je? Kwanza tupate huo muda halisi kisha ndio tupate kuona Mungu kapoteza miaka mingapi ndipo akaumba hivi vilivyomo, na ndipo tujadili sasa kwamba je ndani ya hiyo miaka kadhaa aliyopoteza alikuwa akifanya nini.

Hoja yako ya pili ni kwamba habari ya shetani na dhambi vinapatikana kwenye simulizi za vitabu vya dini kitu ambacho nilishakujibu ya kwamba mimi siviamini.
 
Mkuu wewe Unaweza kuwa ulisoma chuo kikubwa kama havard au Cambridge,,lakini ukija kutafuta kazi hapa tz au popote lazima ufanyiwe interview.

Swali ni je unapofanyiwa ile interview ina maana kile chuo kikubwa ulichosoma kilikupa cheti ukiwa hujakamilika??

Je, huyu anaekupa mtihani wa interview ana level inayostahili kukupa mtihani kumlinganisha hata na tutor wa pale havard au Cambridge?

Kitu kizuri hujaribiwa ili kuthibitisha ubora wake?

La sivyo wewe na cheti chako cha havard havard ungekuwa unaingia Kazini moja kwa moja maana uko 100% perfect
 
Mkuu Achimwene-Masasi ukihusisha ile miti na mapenzi au Mambo ya uchafu kama ulawiti unakuwa umeacha maswali mengi zaidi ya majibu.Ukipata kujua ile miti ikiwakilisha nini utapata majibu ya maswali mengi sana.
 
Asante mkuu kwa kujibu!

Kwanza kabla ya kutoa hoja zangu, namimi niseme kitu!
Unajua mkuu, haya mambo ukiyajadili bila kuegamia upande wowote yanaleta raha sana. Kwa kweli kwangu mimi ni burudani tosha hii ninapoona watu kila hoja inayotolewa lazima ihojiwe. Safi sana na huu ndio u great thinker, hakuna kukubali kirahisi rahisi.[emoji28][emoji28][emoji28]

Sasa niende kwenye hoja!
Hili la kwanza unalozungumzia, ni kuwa kadiri ya wanaoamini Mungu, ni kuwa Mungu hana mwanzo wala mwisho, maana yake ni wa milele. Yaani kabla ya kuumba hata kitu kumoja, tayari alishakuwepo kwa kipindi Infinity kurudi nyuma. Sasa atuwezi tukasema kipindi infinity ni muda gani kwa kutaja kwa namba!! Yaani ni muda usiotamatika!![emoji1787][emoji1787]. Ona ilivyongumu ku visualize!![emoji23][emoji23]

Hoja yako ya pili, mkuu kadiri ya imani yako ni kuwa Mungu ni chanzo cha vitu vyooote. Sasa hapa pia tutahitaji utuelezee, Je, chanzo cha chanzo hicho ni kipi!?
Ndio, kila chanzo kina chanzo, angalia mfano huu, labda tuseme Chanzo cha kifo cha John Doe ni ajali, chanzo cha ajalu hiyo ni mwendo kasi wa dereva, chanzo cha mwendo kasi huo ni kulewa, chanzo cha ulevi wa dereva ni stress, chanzo cha stress, ni usaliti wa mkewe, chanzo cha usaliti wa mkewe ni... chanzo chanzo chanzo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mpaka mwisho, na kujirudia rudia humohumo[emoji28][emoji28].

Mambo haya yanafurahisha sana!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…