Je, mtu unaweza kufunga ndoa kanisani bila kusaini lile karatasi?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,069
40,732
Tunaambiwa kwamba kuendelea kuishi pamoja na kuzaa watoto bila kufunga ndoa kanisani ni uzinzi na kumchukiza Mungu.

Sasa na mimi nauliza, naweza kwenda kanisani kufunga ndoa bila kusaini chochote? Yaani taratibu zoote za kanisa na mashahidi wawepo kushuhudia ndoa, ila sitaki kusaini chochote, inawezekana?
 
Utakuwa hujafunga ndoa bali maonyesho ya ndoa.
Ndoa ni jambo la kisheria na ndoa inafungwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ile karatasi ni ya kiserikali isipokuwa inafungwa kwa mujibu wa imani yako ya kikristo
 
Tunaambiwa kwamba kuendelea kuishi pamoja na kuzaa watoto bila kufunga ndoa kanisani ni uzinzi na kumchukiza Mungu.

Sasa na mimi nauliza, naweza kwenda kanisani kufunga ndoa bila kusaini chochote? Yaani taratibu zoote za kanisa na mashahidi wawepo kushuhudia ndoa, ila sitaki kusaini chochote, inawezekana?
Either ufunge au usifunge ndoa baasi! Mimi nimetia saini ila ikitokea kuna mazingira ya yanayolazimu kuachana tutaachana hakuna anayeweza kukuzuia kuishi maisha ya uhuru. Talaka imeruhusiwa (kasome mwanzo 2:24)

Pia, Ndoa halali ni ndoa ambayo wanandoa wametia saini kama hamjatia saini hiyo si ndoa halali haitambuliki mbele za Mungu na sheria wewe na mwenzi wako mtabaki kuwa wazinifu.
 
Utakuwa hujafunga ndoa bali maonyesho ya ndoa.
Ndoa ni jambo la kisheria na ndoa inafungwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ile karatasi ni ya kiserikali isipokuwa inafungwa kwa mujibu wa imami yako ya kikristo
Lengo langu sio kutimiza masharti ya kisheria ya ndoa, nataka tu kutimiza yale masharti ya ndoa ya kanisa ili masimango ya kumzalisha mtu bila ndoa na kwamba tunafanya uzinzi yaondoke, basi, sitaki kingine
 
Jaribu kuongea na mkuu wako wa dini.
 
Either ufunge au usifunge ndoa baasi! Mimi nimetia saini ila ikitokea kuna mazingira ya yanayolazimu kuachana tutaachana hakuna anayeweza kukuzuia kuishi maisha ya uhuru. Talaka imeruhusiwa (kasome mwanzo 2:24)

Pia, Ndoa halali ni ndoa ambayo wanandoa wametia saini kama hamjatia saini hiyo si ndoa halali haitambuliki mbele za Mungu na sheria wewe na mwenzi wako mtabaki kuwa wazinifu.
Yaani Mungu asitambue ndoa iliyofungwa kanisani kwa taratibu zooote, na kutubu nimetubu kabisa, kisa wino kwenye karatasi?! Hebu nifafanulie the logic behind!
 
Mbele za Mungu...hapana.
Tusiwe wepesi kumtaja Mungu bure.
Ndoa ni jambo la kimwili tu...kutiana na kukidhi tamaa ya mwili tu.
Isaka alisaini wapi?
 
Lengo langu sio kutimiza masharti ya kisheria ya ndoa, nataka tu kutimiza yale masharti ya ndoa ya kanisa ili masimango ya kumzalisha mtu bila ndoa na kwamba tunafanya uzinzi yaondoke, basi, sitaki kingine
Naona kama unataka kuichenga nafsi yako mwenyewe, unataka kuwaridhisha watu. Ndio maana nawasisitiza vijana kila siku tuwajengee watoto wetu wa kike confidence, tuwape elimu waweze kusimama na kuamua maisha yao. Wewe ndugu yetu unataka kumfanya mwanamke kama zuzu yaani uingie nae mkataba feki wa ndoa ambayo mahakama wala dini haitambui.
 
Jaribu kuongea na mkuu wako wa dini.
Wapo humu, nijibiwe in advance..., nimechoka masimango ya kijinga..., kitu chenyewe kwenda kanisani tu.., nipo tayari, ila sitaki kusainishwa takataka yoyote!
 
Yaani Mungu asitambue ndoa iliyofungwa kanisani kwa taratibu zooote, na kutubu nimetubu kabisa, kisa wino kwenye karatasi?! Hebu nifafanulie the logic behind!
Hueleweki mkuu unawezaje kusema umefuata taratibu zote wakati hujatia saini, huo wino kwenye karatasi kwa macho ya kawaida ila kwa macho ya ziada ni commitment kati ya mume na mke.
 
Back
Top Bottom