Je, mtu huyu nimfungulie kesi ya aina gani?

Capt Tamar

JF-Expert Member
Dec 15, 2011
11,655
14,492
Habari za shughuli ndugu zangu,

Naombeni mnishauri kwa jambo hili ambalo naona nalazimika kulifanya, nilipata msiba kwa kufiwa na mke wangu wa ndoa mwanzoni mwa mwaka huu, baada ya mazishi kuna kikao cha ndugu kilikaa kujadili mustakabali wa familia kama ilivyo desturi sasa kwenye kikao kile, wengi walikuwa ni ndugu wa mke wangu.

Wengi wao hata nilikuwa siwafahamu, kikao kikamteua shemeji yangu ambaye ndiye kaka mkubwa wa mke wangu awe msimamizi wa mirathi, mke wangu alikuwa na mali alizochuma yeye mwenyewe kabla hatujaoana, na mimi nilikuwa na zangu binafsi.

Na kuna kiwanja alikinunua kwa kaka yake huyohuyo wakati tukiwa tunaishi pamoja, higher kiwanja tukajenga nyumba za kupangisha, na tukapata mpangaji mmoja aliyepanga vyumba vyote 8, wakati huo mimi nilikuwa nipo nje ya mkoa kikazi.

Kwa hiyo, hata wakati ujenzi unaendelea, mimi sikuwepo, mtu aliyekuwa akisimamia ujenzi ni huyo kaka wa mke wangu, kwakuwa hakuwa na shughuli yoyote kipindi hicho hivyo nikawa namlipa asaidie kusimamia ujenzi na hata shughuli nyinginezo za ujenzi kwenye nyumba nyingine niliyokuwa naijenga mtaa mwingine ambayo ndiyo tunayoishi hata sasa, sasa tabu imekuja baada ya yeye kukabidhiwa jukumu la kusimamia mirathi.

Kwanza alikosana na yule mpangaji hali iliyomlazimu mpangaji yule kuhama mimi nikiwa sipo, kisha akawapangishia wapangaji wengine bila kunitaarifu.

Baadaye kodi ikaanza kusumbua, mara anitumie mara asitume, nikaamua kumfuata ili anieleze tatizo ni nini, baada ya kufokeana sana akaniambia yeye ndiye msimamizi wa mali zote kwa hiyo sipaswi kumpangia.

Ni takriban miezi mitano sasa hajaleta kodi ya nyumba, wale wapangaji sijui aliwaseti vipi, maana kila nikijaribu kuwafata huwa wananikwepa, nadhani hajafungua mirathi mahakamani kwani kuna vielelezo ambavyo angepaswa kuvipata kutoka kwangu ila hakuwahi kuniomba nimpatie, sasa nafikiri nimpeleke mahakamani, ila huko sina nijualo especialy kwa kesi ya aina hii.

Naamini hapa kuna wajuzi wa mambo kama haya. Hivyo naomba mchango wenu wa mawazo ili niweze kuilinda haki ya familia yangu nikiwa na ujasiri.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
 
Mkuu Capt Tamar pole sana!.

Ila nina maswali kadhaa napaswa kukuuliza.

1. Je wewe ni mume halali wa marehemu?(mmefunga ndoa?)

2. Mlibahatika kupata watoto wewe na mkeo?

3. Ilikuwaje kaka mtu akawa msimamizi wa mirathi ya dada yake wakati wewe mume wake upo?

Naomba tafadhali unijibu mkuu maana sielewi!
 
Msimamizi anachuguliwaje na wakwe zako wakati mume upo hai?

Hapo ndo pakuanzia! Ulibugi hapo kwenye hatua ya kwanza.
Hapo nakubali kweli nilibugi,ila kutokana na hali niliyokuwa nayo wakati huo sikufikiria athari ambayo ingeweza kujitokeza baadaye,na tayari tatizo limejitokeza,ndiyo maana leo nipo hapa kuomba busara zenu ndugu zangu ili nijikwamue kutoka hapa,mbaya zaidi kuna vyumba vingine nilianza kuvijenga baada ya msiba,kwenye eneo hilohilo,na vipo kwenye hatua za ukamilishaji,ila amepiga makofuli vyote,kwa hiyo hata siwezi kuviendeleza,msaada jamani.
 
Mkuu Capt Tamar pole sana!.

Ila nina maswali kadhaa napaswa kukuuliza.

1.Je wewe ni mume halali wa marehemu?(mmefunga ndoa?)

2.Mlibahatika kupata watoto wewe na mkeo?

3.Ilikuwaje kaka mtu akawa msimamizi wa mirathi ya dada yake wakati wewe mume wake upo?

Naomba tafadhali unijibu mkuu maana sielewi!
Mkuu UMUGHAKA ni mke wangu wa ndoa kabisa,ndoa ya kanisani,na vyeti via ndoa ninavyo,tumejaaliwa watoto wawili,wote wapo shule na vyeti vyao vya kuzaliwa ninavyo,mke wangu tulimzika nyumbani kwangu,hapa hapa ninapoishi sasa.
 
Jibu hayo maswali muhimu hapo juu.

Huenda Kaka Mtu na hao ndugu wengine wa Mke walishaona udhaifu mahali ndio maana ame take advantage.

Ila cha muhimu tafuta Mwanasheria hapo jirani, au kama kuna unayemfahamu kisha hakikisha unamueleza a to Z ya hali ilivyo naye atakupa muongozo...maana haiwezekani ukaanika kila kitu humu,
 
Jibu hayo maswali muhimu hapo juu.

Huenda Kaka Mtu na hao ndugu wengine wa Mke walishaona udhaifu mahali ndio maana ame take advantage.

Ila cha muhimu tafuta Mwanasheria hapo jirani, au kama kuna unayemfahamu kisha hakikisha unamueleza a to Z ya hali ilivyo naye atakupa muongozo...maana haiwezekani ukaanika kila kitu humu,
Maswali nimeyajibu mkuu May Day
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom